Tembo aua Majangili wawili Mikumi

Tembo aua Majangili wawili Mikumi

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Sasa tembo wameamua kujilinda. Juzi, tembo mmoja amewaua majangili wawili waliotaka kumuua. Tukio hilo limetokea katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi-upande wa Kilosa. Mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa Mjangili hayo yalipita kijijini kwao yakielekea hifadhini kwa ajili ya kuua tembo yakiwa na silaha nzito.

Inadaiwa kuwa tembo aliyewaua majangili alijeruhiwa kwa risasi na kujifanya amekufa.Majangili waliposogea kwa ajili ya kutimiza lengo lao la kuchukua nyara,tembo husika alikurupuka na kuanza kuwashambulia majangili hao hadi kuwaua wote wawili.Halafu, akaziponda maiti na kurundika miti katika maiti hizokiasi cha kuzifanya zisionekane.

Mashuhuda waliofika katika eneo la tukio walikuta maiti hizo pamoja na silaha walizokuwa nazo majangili hao. Natoa pongezi kwa tembo wa Mikumi kwa kujilinda. Tembo wote nchini nao waige mfano huo.

Chanzo: Wananchi wanaoishi kandokando ya Mikumi,upande wa Kilosa na Askari Wanyamapori
 
Ukitaka kujua serikali ya Jk inalinda majangili hii ishu aijaripoltiwa kwenye chombo chochote cha habari hisusani vya serikali Jk ndio anayemaliza tembo na katibu mkuu wake kinana
 
Unanikumbusha Shamba la wanyama pale wanyama walipopindua serkali ya bwana Mtiki pale shamba Ibura
 
Tembo hiyo ndo tabia yake kujifanya amekufa,alimuua babu yangu hivo hivo.R I P babu.

Mh... Babu yako alikuwa jangili?? Sema tu hutokamatwa, hata kama utakuwa unamsaliti Katibu Mkuu.
Huyo tembo anastahili kupongezwa, ili apate ujasiri wa kupambana na majangili zaidi.
Wananchi mmesikia! Tembo wanajilinda, na nyie mpate akili kutoka kwa tembo.
 
sasa mtoa taarifa, hao majangiri kumbe huwa wanajulkana. kama wanapita mtaani kwenda kutungua matembo wetu na watu wanawaona. kwa nini game wasiwe wanafanye counter attack kabla hawajaingia porini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom