kazi nzuri kijana endeleza fani
Mkuu naomba ushauri zaidi, na kama unaweza hebu angalia hako ka logo nilikodizaini leo kama kanafaa.
Natanguliza Shukrani.
Kiganyi, JF.
Wotepamoja online magazine - wotepamoja
Hii LOGO Ipo Poa sana ila ifanye kidogo iwe kubwa na rangi zake zibadilike kidogo.
Pia maandishi yakae upande wa KULIA wa LOGO.
Hebu angalia LOGO nyingi na hata ya JF utaona ninalolisema.
Kwa haraka haraka unatakiwa ku-MIRROR Logo yote kwa 90 degree (perpendicular) na ubadilishe rangi.
Vinginevyo imekaa poa sana na HONGERA ZAKO.
hiyo logo imekaa poa kwasababu ukiitazama kuna kuna mwanaume, kuna mtoto na mwanamke halafu hizo circles zinaonesha muunganuko flani kwa hiyo zinaleta picha ya watu kuwa pamoja. Pia rangi ulizotumia nzuri kutokana na background yako japo kuwa kuna part ya maneno umetumia light green inakuwa kama imevififia sana.
Lakini still inaonesha kazi nzuri mkuu. Jitahidi ku iadvertise sana
Mkuu Shukrani sana kwa Support...
Nipe maujanja ya kuitangaza na kama vipi nisaidie mkuu!
Kwa mtazamo wa haraka haraka, naona kazi ni nzuri, ila kama walivyoshauri wadau hapo juu, kuna maneno kwene logo hayaonekani vizuri. "Unveiling news horizon" weka rangi inayoonekana zaidi hata kama ni kijani tumia iliyokolea zaidi.
Pili, naona kama umeacha nafas kubwa sana juu ya "headlines" kwenye hiyo top banner, labda unge squeeze kidogo kwa ku crop hiyo logo juu na chini.
Sina uhakika kama "Entertainment" ina plural..