Telekinesis

Mshana Jr.umenifurahisha si kwa bandiko hili kwa ukweli uliousema kuhusu nguvu alizoumbwa nazo mwanadamu.Kwa wale Wakristu tunasoma katika kitabu cha Mwanzo: "...Na tumfanye mtu kwa mfano wetu..."Hii sentensi inaelezea kwa ufupi sana ukuu na uweza na nguvu alizorithishwa mwanadamu kutoka kwa Mungu.Na tumepewa uweza huo ili tushirikiane na Mungu katika kazi ya Uumbaji.Ulimwengu (the Universe) bado unaendelea kuumbwa.Na pengine alifanya hivi ili Mungu apate nafasi ya kutosha kujenga makazi yetu huko aliko."...Nyumbani mwa Baba Yangu kuna makao mengi...la sivyo ningeliwaambia...naenda kuwaandalia makao kisha nije kuwachukueni". Hayo ni maneno ya Yesu na ndio ushahidi wa kwa nini aliturithisha nguvu na uweza wake.Ni ili yeye apate muda na nafasi ya kufanya mengine.Ni sawa tu na wewe unamuachia binti wa kazi nyumbani kazi fulani fulani ili wewe upate nafasi ya ku-handle mambo makubwa na muhimu zaidi.
Kwa hiyo, binadamu laiti tungetambua huo uwezo tulio nao wala tusingekuwa tunalialia juu ya changamoto zinazotukabili maishani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…