Telekinesis


Asante mkuu, umenifungua sana mkuu,
 
Ha ha ha makaburini nenda na Madame B mie huko napaogopa

Kuna elimu ya vitendo kule very very interesting...mtu anafika kaburini analilinyooshea mkono kaburi linafunguka mtu anatoka kama hivi hamuoni kabisa ila unaona morphology yake, halafu anamfuata aliyemwamsha
Umejibanza pembeni huonekani unayashuhudia yote haya kwa macho makavu na ndipo hapo unapogundua kuwa dunia ni zaidi ya uijuavyo
 

Mmmh huku sasa kuogopeshana, unamwamsha ili? Usimwamshe alielala teh....
 

Aisee hii dunia, unaweza ukasema unajua mengi kumbe bado.Binafsi sikuwahi kuwaza wala kusikia juu ya hili
 
Kwa wakazi wa Songea mtakuwa mnamfahamu baba mmoja mmakuwa toka Masasi anajishughulisha na kutoga masikio na vipini bila maumivu.Sijajua jina lake.Huyu anaweza:
1.Akawasha sigala kwa kutumia vidole

2.Akamjua mwanaume ambaye hajatahiriwa na mwanamke bikra.

3.Akamtahiri mtu kwa kumnyoshea kidole usawa wa sehemu za siri.Nk

Anakiri kuwa haujui uchawi.
Je mshana jr hii nayo ni telekinesis au inaitwaje?
 
Last edited by a moderator:

Inawekana kabisa lakini pia yaweza kuwa ni maarifa mengine mengi ya ziada ambayo yanapaswa kufanyiwa utafiti
Telekinesis asili hufanya kazi kwenye vitu vya chums zaidi kuvipinda kuvivuta kuvisukuma nk hii manabii na mitume wa Kileo wanaitumia sana
 
Last edited by a moderator:

Nina rafiki yangu flani yeye anauwezo wa kuangalia kijiko mpaka kikajikunja, yani anazo hizi nguvu sana, ila tatizo lake ni ujana. Anapenda sana pombe hivyo kuna kipindi huwa anapoteza uwezo labda kwa kuto meditate lakini akitulia huyu dada anazo hizi nguvu. Yeye ndo mtu wa kwanza alokuwa akinishauri maswala ya meditation.
 
Sema hii mada hapa sio mahala pake, kule intelligence ndo kunafaa mada nzito kama hizi
 
Last edited by a moderator:
Asante mwalimu wetu mshana jr Mungu akubariki sana kwa kutufundisha haya mambo mazuri.
Je haya yote ni zao la zoezi la meditation ambalo huwa linanishinda?

Telekinesis ni nguvu za kiasili lakini pia kupitia meditation yoga na ushirikina waweza pia pata hizi nguvu na hata kupitia imani ya kishetani NDUKI anaweza kuja kuongeza neno hapa
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…