Teknohama na matumizi salama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Teknohama na matumizi salama

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Jun 14, 2010.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Jun 14, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Tangu kutua kwa mkonga wa mawasiliano kwa baadhi ya nchi za Afrika Matumizi ya Teknohama yameongezeka kwa kasi haswa baada ya baadhi ya kampuni kushusha bei na pia imechochea kuanzishwa kampuni nyingi zaidi zinazotoa huduma za mawasiliano haya kwa bei nafuu nchini , bila kusahau nafasi za ajira na fursa zingine za kibiashara zinazohusisha teknohama .


  Hawa watu wanaoingia sasa hivi kwenye ulimwengu wa teknohama kutokana na Mkonga huu wa mawasiliano wanaweza kuwa Targets mpya za wahalifu kutokana na sababu mbalimbali haswa zinazohusiana na uelewa wa masuala ya teknohama kwa ujumla  Lakini kwa wale wazoefu Mkonga Huu umeleta maendeleo sana lakini pia unaweza kupunguza kasi ya maendeleo kwa baadhi ya jamii kutokana na sababu kadhaa moja ya sababu hizi ni kwa jamii hizo kupuuza matishio mbalimbali yanayotokana na matumizi ya TEKNOHAMA au kwa kutokuelewa baadhi ya vitu haswa vinavyohusiana na ulinzi wa mali zao au kifaa chenyewe cha teknohama pale anapotumia .


  Matatizo yanayotokana na kukosea kutumia vifaa au kutokuwa na uelewa mpana wa baadhi ya vitu vya TEKNOHAMA ni mkubwa sana kwa nchi zilizoendelea ni rahisi kujua hata jinsi inavyotokea haswa kwa sababu jamii zao zina utamaduni wa kutoa taarifa kwa vyombo husika mapema ndio matatizo yao yatatuliwe au kutafuta wale wote wanaohusika na hujuma hizo moja kwa moja .


  Nchini kwetu pamoja na nchi zingine zinazoendelea utamaduni wa kupuuza matishio na mambo mengine yanayoendelea kwenye TEKNOHAMA ni wa hali ya juu sana kwa mfano unaweza kumwambia mtu umuhimu kwa kutumia Antivirus na programu zingine kwa ajili ya ulinzi wa Kompyuta yake hatoamini mpaka mkasa utakapomkuta hata akikubali basi atataka kuuziwa kwa njia za mkato .


  Tukija kwenye mashirika yetu ya ummah na taasisi zingine nyeti unapowaambia andaeni miongozo ya TEKNOHAMA kwa wafanyakazi wenu na watu wengine wanaotumia vifaa vyenu hawatafanya hivyo kwa kuamini kwamba mtandao labda haujakuwa sana na wengi sio waelewa wa mambo hayo kwahiyo hawahitaji miongozo wala sheria zozote makazini humo .


  Wahalifu wengi kwa sasa wanahama toka nchi walizomo ambazo zinasheria kali au wanabanwa sana na vyombo vyao na kuanzisha shuguli hizo kwenye nchi zingine ambazo sheria ni dhaifu au hamna sheria kabisa au watu wake hawana uelewa mpana wa baadhi ya masuala ya Kiteknohama mfano kwa sasa Wahalifu wengi wa afrika ya magharibi wamehamia nchi za kusini mwa afrika kuendesha shuguli zao tokea huko kutokana na sheria za nchi hizo kuwa dhaifu hata vyombo vyao kwa usalama .  Uhalifu wa Kiteknohama umekuwa sana kwa sasa na unalenga maeneo mbalimbali ambapo jamii zinafanyia kazi kama uko kwenye mtandao au nje ya mtandao lakini taarifa zako zinaweza kupatikana kwa urahisi na kuwa mikononi mwa wahalifu .


  Unahusisha kuiba taarifa binafsi za mtu na kwenda kutumia taarifa hizo kwenye shuguli zingine kama manunuzi ya vitu kwenye mtandao , kuhamisha fedha toka kwako kwenda kwingine ,kuharibu mawasiliano ya mtandao hata kuufanya ushindwe kufanya kazi vizuri kutokana na mashambulizi toka upande mwingine wa dunia .


  Sasa hivi nchini Tanzania kuna watu wanauza nakala za passport za watu ambazo zimekuwa scanned kwa wahalifu wengine duniani haswa wa kimataifa kwa ajili ya shuguli zao mbalimbali kwa njia ya mtandao au kwa njia nyingine lakini inayohusishwa na mtandao kidogo .


  Leo Tumepata taarifa kwamba mtu mmoja alisahau Nakala za passport yake kwenye mgahawa wa Mtandao kisha wahalifu hao wakatumia nakala hizo kwa ajili ya kuwasiliana na wanunuzi wa madini pamoja na kuingia nao mikataba minono kwa kutumia taarifa za huyo aliyesahau .


  Huo ni mfano mmoja tu kuna mifano chungu nzima ni vizuri ndugu zangu tusiwe tuna puuza au kudharau matishio mbalimbali kwenye mitandao yetu na mifumo yetu mengine ya mawasiliano siku moja itatugarimu sana .


  Tutumie Fursa zilizopo sasa za Teknohama kwa ajili ya kujifunza zaidi na kuleta maendeleo kwa nchi yetu na kupeana taarifa zinazoweza kusaidia nchi yetu na matishio mengi yanayoweza kuhatarisha usalama na maslahi ya nchi yetu Popote pale .


  USIKU MWEMA
  YONA F MARO
  MAY 2010
  WWW.ICTPUB.BLOGSPOT.COM
   
Loading...