Tegeta Escrow: TANESCO yashindwa kesi dhidi ya IPTL. Yaamriwa kulipa zaidi ya Sh. Bilioni 320!

Hili deni sijui litakuja na kodi gani mpya ili kufidia, ngoja tuone ila ninachoamini ni kwamba tutalilipa sisi bila wao kuingiliwa.
 
Kama sijasahau, Wakati wanakalibia kupiga deal lao la "Escrow" Governor wa Bank Kuu Prof. Ndulu aliwataka hao PAP + IPTL wasaini agreement ya "Kinga" dhidi ya serikali endapo kutatokea lolote...

Hapa sasa tuone busara za JPM

Hii mbona sikuwahi kuisikia, aliwashauri hivyo kweli? Kweli mijizi ipo kila mahali, hawa ndio wanaojiita consultants.

Na yule Profesa Muhongo nae si alisema kuwa hela si za umma?
 
Mbona DaLaLi yupo..
Wamufuate Pale offisini kwake Wizara ya Nishati na Madini..
Atalipa yeye na makanjanja wenzake..
 
IPTL ukiwaangalia vizuri Nchi za kusini wapo Tanzania tuu ni kuchaka cha kupigia hela za Tanesco, bill zipo juu kwa sababu ya hawa wachache na sisi tupo kimya tuu..
Kuna muda huwa naona ni bora kuwalipa tukaachana nao. Kila siku wanatuletea songombingo tu au tuliingia nao mkataba wa milelel??
 
Do! Inasikitisha nakumbuka siku ambayo Tibaijuka anaambiwa akae Pembeni na Mkuu wa Kaya akiwahutubia Wazee wa Dar es salaam alisema zile hela siyo za serikali,Kama wenyenazo walishachukua hawa wametoka wapi kutudai tena,Watanzania wenzangu hii issue IPTL ni ya miaka mingi kwanini kila siku watu zaidi milion 50 tumeshindwa kulipatia ufumbuzi?Hilo ni dili watu serikalini na washirika wao,Mheshimiwa Rais itisha mjadala wa kitaifa kuhusu unyonyaji huu.Wanabodi nataka kujua hao majaji kuna waafrika?na wanapatikana vipi,Tusikurupuke kusaini Maazimio ya kimataifa kuanzisha vitu kama hivi,lazima tujiulize vina faida kwetu? Hii mbinu ninamna ya mabeberu kukwapua Mali yetu kwa mlango wa nyuma kwa kushirikiana na maprofesa(wasomi)wezi tuliowaamini.
 
Baada ya kujua ishu ya IPTL mwanzoni mwa miaka ya 90 , Mwalimu Nyerere alisema, kama ushirikiano wa nchi za south South uko hivi then bora ukoloni.

( IPTL ni kampuni ya Malaysia ambayo nayo ni member wa nchi za South South
 
Naamini hata Mimi maamuma nikisimama na wakili Wa serikali au MTU anaye wakilisha tasisi ya serikali naweza kushinda kesi kiurahis sana.

mtu anayeitwa jamhuri hajawahi kushinda kesi mahali popote labda ''cha juu"cha rada kwa kuonewa huruma tu
 
Back
Top Bottom