- Thread starter
- #21
Mimi hii kitu nimeisikia kwa ndugu zangu walioingia huko. Nilikwenda Rufiji kwa shughuli binafsi nikaambiwa hiyo TEDET haimiliki hayo mashamba ambayo watu wanaonyeshwa. Wakazi wa Wilaya si wanajua wamililki wote wa ardhi an miradi ya maendeleo iliyopo kwenye eneo lao lakini huu hata wakazi wa Rufiji wenyewe hawajui.
Nadhani hawa jamaa wanatumia style ya Deci ya kutoa matumaini ya faida nono. Wizara ya ardhi na kilimo zitoe tamko, uongozi wa wilaya nao utoe tamko.
Waandishi wa habari mpo? fatilieni hii kitu na muiweke hadharani jamani, Unjua watanzania mafisadi wametudhurumu sana, kila mtu anatamani maisha mazuri, ndo maana akitokea mtu mwenye kutoa matumaini hata kama ni badnia wengi hukimbilia huko, lakini kama mtasaidia kuweka wazi hili, mtaokoa fedha za watu wengi wanao endelea jiunga huko, ila kama ni kweli basi pia mtasaidia wengi kufaidika na hilo. Fatilieni na mtusaidie
Asanteni sana kwa mlio toa maoni yetu, hata hivo mwenye data zaidi tuna zisubili kwa hamu.