TEDET nayo ni kama DECI? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TEDET nayo ni kama DECI?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rwabugiri, Jul 3, 2009.

 1. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kuna jamaa yangu kaniambia kwamba kuna hiyo association inaitwa TEDET (Tanzania Eco-Development Trust), kwamba inakusanya hela za wanachama kiingilio sh. laki 5 (500.000) ambayo inajumuisha kiingilio ada ya uanachama na shamba la ukubwa wa hekari 5 huko bonde la mto RUFIJI. Kasema makubaliano ni kwamba mwanachama anapewa hilo shamba heka 5, ila anakuwa analimiwa hilo shamba heka 4 mazao ya biashara na heka moja mazao ya chakula.

  Mazao ya chakula atakuwa akipewa magunia 20 ya mahindi /mpunga kwa msimu yaani misimu miwili kwa mwaka, wakati mazao ya biashara yatakuwa yakiuzwa kwa pamoja masoko ya nje na kila heka ikikadiliwa kutoa mazao ya wastani wa thamani ya milioni 1.5, lakini mkulima atakuwa akikatwa laki 2 kila heka kama garama ya uendeshaji.

  Kasema hiyo Tedeti inashirikiana na KIMUDEA umoja wa wakulima wilaya ya Kinondoni, na wakazi wa Rufiji chini ya umoja wao wa RUDIDEA na kwamba wanachama wanapelekwa kuonyeshwa mashamba huko Rufiji.

  Nilipo search goggle nikakuta kweli hiyo kitu ilikuwepo toka mwaka 2006, na mwenyekiti wake ni Dr. Mugishagwe. Na kuna pesa mamilioni mengi, toka kwa wafadhili zimekuwa zikiingia huko TEDET, taarifa zipo ukigoogle za upokeaji wa pesa hizo. Hakuna taarifa zaidi kuhusu huu umoja, kilimo hata hizo ada za uanachama.. Kasema ofisi zao zipo MASASI HOUSE KARIAKOO?

  Kweli nikaona maelezo yake ni mazuri, lakini nikapata hofu kwamba je hii haiwezi kuwa DECI ama PUFDEA nyingine? Manake hii kusanya ya kiingilio cha laki 5 kila mwanachama, na kasema wanatakiwa wanachama elfu 10,000. Na kasema wengi sana wamejiunga. Na ahadi ni kwamba wanaanza kilimo mwaka huu.

  Ndipo nikaona pengine niimwage hapa kwenye Jamvi nene labda kuna wenye datas za uhakika nisije ingia mkenge wa DECI no.2

  Na kama kweli si DECI, basi wanajamvi tuchangamkie uanachama kwani maelezo yake ni mazuri.

  Asante wakuu.

  Mod. tafadhali iacheni kwa muda hapa tupate datas
   
 2. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu

  Sina habari za undani kuliko za kwako ila......mimi pia nililisikia kwa marafiki zangu 2 wa karibu ambao wanafanya kazi wazoefu kwenye mabenki 2 tofauti hapo Dar. Sikuwa na muda wa kuifuatilia sana ila walikuwa na wasiwasi kuwa huenda ni DECI ...hitimisho lilikuwa watajiandikisha na kwamba iwapo itatokea wakaliwa hela hiyo laki 5 kwao sio kitu.
   
 3. m

  msabato masalia Senior Member

  #3
  Jul 3, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Shotikati jamani!!!!!!!!!Dk.Remmy alisema ukinywa bia usipite vichochoroni....utakabwa...........!!!!!!MKULO,Ndulu vibaka wengine hao,wafakamie kama mwewe au kama helkopta ya Mbowe.:)
   
 4. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Mazoa yasipopatikana inakuwaje? Tuseme wadaudu wamevamia shamba na kuharibu mazao. Market ya mazao isipokuwepo mwaka huo inakuaje?

  Kwa mahesabu yangu hiyo laki tano inatakiwa izalishe 1.5 x 4 = 6 mil - 800,000= 5.2 mil + magunia 20 ya mahindi.
  Ukubwa wa faidia ukifananisha na mtaji unanitia wasiwasi, lakini ni bora uongee na mtu ambaye amewahi kulima akueleze kama hizo faida zinawezekana kweli.
   
 5. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kwa maelezo ya yule jamaa make nasema ilibidi waingie darasani wafundishwe na kuelekezwa itakavo kuwa, anasema hayo mashamba yatakuwa yanakatiwa bima, ya majanga kama hayo hata ya mabadiliko ya bei kuhakikisha kwamba mkulima hakosi hiyo 1.5 kwa heka moja!

  Ukisikiliza maelezo (story behind) yanashawishi ila kwa vile wajanja wengi siku hizi ndo maana ni vyema kama kuna mtu anadata za uhakika wa hii kitu akazimwaga, ili kama ni kweli watu wachangamkie hizi nafasi.

  Alisema wana na tangazo lao redioni linasema ''kwanini unahangaika kulima kwa jembe la mkono, nenda TOPPETA? watakulimia kwa trekta'', binafsi sijawai lisikia kwani huwa sifungulii sana hiyo Redio TUMAINI alo sema lipo!
   
 6. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Mapato ya jumla ya 1.7 au Milioni 1.5 net kwa mteja/mkulima kwa hekari ni faida kubwa mno. Sababu; wakati wa msimu wa mavuno wa Mahindi (kama mfano, sijui wao wanapanga kulima nini) kwa Dar kila gunia huuzwa kati ya Shs 5000 - 8000 vijijini/mashambani ni chini zaidi. Sijui bei ya mpunga wakati wa msimu wa mavuno kwa Dar au Mashambani (mwenye info tafadhali) atusaidie.

  Kwa hesabu ya gunia 1 shs 8000 ili upate Shs 1.7 Milioni unahitani maguni 212 kwa hekari..!!! Au kama ni kuvuna mara 2 kwa mwaka basi kila mavuno upate Magunia 106 kwa hekari..!!! Huo utakuwa muujiza.

  Najilaumu kwa nini sikuwafuata ofisini kwao niwasikilize kwa makini.
   
 7. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu...hii sio shotikati ni sawa na umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu...au??

  Hela inawekezwa na kuzaa na sio kuwekwa kwenye chungu ili izae kwa miujiza.
   
 8. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #8
  Jul 3, 2009
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  hii inatia matumaini kidogo kuliko deci kwa sababu angalau wanachotaka kukifanya kipo wazi na kina ingia akili ....japo kuwa faida inaonekana kubwa mno kwa mtaji mdogo.
   
 9. H

  Hekima Ufunuo JF-Expert Member

  #9
  Jul 3, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 220
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naona kila mmoja anaongea kwa hisia na labda nyingi sana. mimi pia ninazo habari za huu mradi na nilienda ofisini kwao kueleweshwa vizuri.

  Kwa kuwa kuna maswali mengi na majibu yake mengine ni more technical kwetu sisi sote na kwa kuwa mtoa mada anatoa pia ushauri kwa wanajamii kuchangamkia hii oppotunity, nashauri yafuatayo\;

  1. badala ya kuendelea na hisia, wenye nia njema waende ofisini kwao karibu na mnazi mmoja jengo ambalo kwa chini kuna duka la top shop nafikiri ni ghoropha ya tano au ya sita.

  2. Kuna darasa la kuelimisha watu wote wanaotaka kujiunga, maelezo ni bure na yatahusisha juhudi ambazo zimefanyika ikiwa ni pamoja na kulipima eneo lenyewe na namna ya umwagiliaji pamoja na namna mradi utakavyendeshwa kwa muda wa miaka kumi. Kuna issue pia ya masoko yaliyopo ya ndani na nje ikiwemo serikali kununua kwa ajili ya akiba ya chakula nchini.

  Mimi sijapata hiyo laki tano lakini ikitimia tu nawahi mapema kwa kuwa nilielimika na nikapewa pia makabrasha yanayousiana na huo mradi. Naamini mradi huu usipoingizwa siasa unaweza kabisha kuliondoa taifa hili kwenye njaa inayojirudia mara kwa mara.
   
 10. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu angalia hesabu yako, kwa kawaida kama umelima mpunga kama mavuno si mazuri walau unaambulia gunia 15. lakini huwa unaweza pata hadi gunia 20-25. na bei ya mpunga mkuu ukipanda huwa ni kwenye elfu 70, wakati wa mavuno huwa iko chini kwenye elfu 30-45. Kama nakosea nisahihishwe wakuu, ila niliwahi ongea na mkulima wa Mpunga Moro ndo alinipa data hizo!.
  Kwa hiyo hiyo 1.5 inawezekana mkuu ukichukulia mpunga.

  Lakini bado sina hakika mkuu, siku hizi Bongo ni mwendo wa Nigeria, watu wanajua jinsi ya kukusanya pesa toka kwa walala hoi chap chap!

  Jamani leteni data mnao jua hii TEDTI, RUDIDEA, Topea? KIMUDEA? et al.. kwani ndo majina yanayo tajwa huko!
   
 11. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #11
  Jul 3, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Asante sana mkuu, hizi ndo data tunazitaka ili tujue ni kweli ama deci?

  Sasa labda mkuu ulifanikiwa kujua kama mradi umeanza tayari? je uhai wa wanachama, wana vikao wanavyofanya kujua mwenendo mzima wa project? samahani mkuu in case unajua zaidi, lakini hata hivo naamini JF jamvi nene data zaidi zitakuja!
  Na kwa kusaidiana hivi tukijuvyana wasio jua wanachangamkia, lakini kama ni kanyaboya, basi inapunguza wengine wasiuingie mkenge!

  Asante mkuu
   
 12. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #12
  Jul 3, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Mkuu,

  Heshima kwako. Kwa sababu ulihudhuria darasa...naomba utupatie yale yaliyojiri huko japo kwa juu.

  1. Mradi umeshaanza au unatazamiwa kuanza lini?

  2. Mpaka sasa wana wanachama wangapi?

  3. Nikilipa laki 5 na kuwa mwanachama, namilikishwa hiyo hekari 5 au nakuwa nimeikodi kwa kipindi cha mradi tu?

  4. Ni gharama gani nyingine nitalazimika kuingia zaidi ya hiyo laki 5?

  5. Uongozi mzima wa mradi ni wakina nani?

  Ni hayo tu kutoka kwangu, tafadhali tuelimishe kwa jinsi ulivyuelewa wewe.

  Ahsante
   
 13. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #13
  Jul 6, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Wakuu nakumbushia data wakuu.. mwenye kujua tujuvyane
   
 14. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #14
  Jul 6, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Lakini shamba usilolilima wewe na unasuburi mazao=Deci ni kupanda mbegu na kusubiri kuvuna bila kupalilia.Tutafakari!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 15. M

  Malila JF-Expert Member

  #15
  Jul 6, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Kama una nguvu za kuwekeza ktk kilimo,basi bora ujitafutie shamba mwenyewe,haya mashamba ya kutafutiana/kupeana/kuitana yanaweza kuja leta shida huko mbele. Ardhi nzuri ipo kama unataka kulima tafuta au kama wewe ni mshirika mzuri jiunge na mwenzio muingie shambani.

  Hiyo title deed ya shamba hilo ina jina la nani? Mnaweza mkawa mnaitwa ili mkalisafishe shamba,liksha kuwa safi basi hamna chenu.
   
 16. B

  Bob K Member

  #16
  Jul 6, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi hawa jammaa nishawahi kuwasililiza good idea tatizo huyu msimamiz mkuu au mwenyekiti wazere wa mjini nilipowatajia hapo hapoa wakaniambia nymaza na ishia huyu mzee ni soo sasa kivipi kuniambia huyu mzee mwenzani ni soo sijui mwenyekiti wa teted ni haji muji shangwe sasa sjui wadau faili lake la uko nyuma likoje fukueni?
   
 17. I

  Ipole JF-Expert Member

  #17
  Jul 6, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 296
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mimi mashaka yangu ni hilo jina la mwenyekiti Dr. MUGISHAGWE linatia shaka

   
 18. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #18
  Jul 6, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu linatia shaka gani? unadata zozote utumwagie zaidi mkuu? ndo maana tunauliza mkuu ili kma si mkenge tuchangamkie
   
 19. M

  Malila JF-Expert Member

  #19
  Jul 7, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Kuna kibao kimoja kimeandikwa hivi: Park on your own risk.
   
 20. Ncha

  Ncha JF-Expert Member

  #20
  Jul 7, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mimi hii kitu nimeisikia kwa ndugu zangu walioingia huko. Nilikwenda Rufiji kwa shughuli binafsi nikaambiwa hiyo TEDET haimiliki hayo mashamba ambayo watu wanaonyeshwa. Wakazi wa Wilaya si wanajua wamililki wote wa ardhi an miradi ya maendeleo iliyopo kwenye eneo lao lakini huu hata wakazi wa Rufiji wenyewe hawajui.

  Nadhani hawa jamaa wanatumia style ya Deci ya kutoa matumaini ya faida nono. Wizara ya ardhi na kilimo zitoe tamko, uongozi wa wilaya nao utoe tamko.
   
Loading...