mimi natumia tecno f2 ya laki na nusu na age yangu ni 31
ninamiliki nyumba ya kuishi niliyojenga chanika
ninamiliki gari ndogo passo niliyoagiza mwenyewe japan
ninamiliki laundry business sehem tofaut
ninamiliki tshirt printing workshop
ninamiliki studio ya kupiga picha za kisasa na video kwenye events..
sijawai kua na hela ya kununua smartphone zaidi ya laki na nusu...
ila nimewai kununua vitu vingi sana zaidi ya laki na nusu vinanisaidia maishani kupata kipato kila siku..
kuna vijana wengi sana wa umri wangu wanakujaga kunikopa hela na wanaweka bond smartphone zao za laki 5 hadi milioni..
kama nina hela huwaga nawakopesha ila nawashangaa sana.. na wengi wao kunilipa wanasumbua..
hapa nilipo nina i phone 6 + mtu ameweka bond nimpe laki 3.. na anasumbua kulipa.. namuonea huruma tu kuiuza na akileta ujinga naiuza kweli
nilichojifunza watanzania wengi vijana hawajui kuzungusha pesa.. hela wakipata wanatumia katika vitu ambavyo haviwasaidiii
sababu mimi na tecno yangu ya laki na nusu kila mtandao maarufu nina access bila wasi wasi sawa na mwenye samsung au iphone ya milion 2