Tecno mobile Mega Thread


yap nimemaanisha hivyo kaka kwanza nianze na introduction maana najua kuna criticism zitakuja. simu haijalishi imetengenezwa wapi bali tunatakiwa tujali imetengenezwa na nani. manufacture kama apple na samsung wanadesign simu halafu ndio zinapelekwa china kutengenezwa kwa wingi. ule uzuri unaouona kwenye iphone hautokani na foxcon bali ni apple wenyewe waliofanya design.

design ya simu ni kubwa sana na inacost mabilioni ya hela kutengeneza prototype kabla ya kwenda kiwandani kutengeneza kwa wingi. hawa tecno na karibia manufacture wote wa mediatek wao hawadesign simu wala hawana viwanda bali wanakwenda tu china kutoa order na kueka logo zao.

sasa hivi kuna pikipiki zinaitwa mkombozi kuna nyengine zinaitwa mtanganyika zipo mitaani munataka kusema na hawa jamaa wana kiwanda tanzania cha pikipiki? hawa ni kama tecno wanaenda tu kutoa order ya simu huko.

kaka njunwa umenipa challenge ya phantom nilishawah kuonesha simu kama phantom ila sio mbaya nitarudia tu hapa. hebu tuiangalie kwa makini phantom yetu kama sio mtanikosoa

phantom ni hiyo nyeupe na hapo kwenye design ya simu tunaona
1.camera 8mp
2.design yake kuna camera hump ya duara imetokezea kidogo
3.flash nayo ni ya duara ipo pembeni ya camera
4.spika ipo kwa chini
5.juu ya spika kuna description ya maneno toka kiwandani

tumeona nyuma ipoje tuje mbele sasa

1.angalia spika ye mbele hapo juu
2. kioo ukubwa wa inch 5
3. resolution ya 1280x720

njoo internal za ndani
1.ram 1gb
2.internal memory 4gb
3. hsdpa 2100 pekee

ukimaliza hapo njoo angalia simu hizi



angalia position ya camera angalia flash, angalia spika, angalia spika ya mbele zote zina 8mp tena imeandikwa kwa nyuma zote zina 4gb zote ram 1gb zote zina hsdpa 2100 karibia kila kitu kinafanana je ni coincidence?
 
Yani humu ndani kila siku simu yenye majanga ni tecno,naww ndo kwanza unataka ukanunue tecno..buy tecno at your own risk
 

Mkuu kama ni simu kufanana mbona ziko nyingi? na za makampuni makubwa
 
Mkuu kama ni simu kufanana mbona ziko nyingi? na za makampuni makubwa

hebu taja mfano simu ya kampuni kubwa kama nokia au samsung au htc au motorola au lg inayofanana na mwenzake kuanzia design hadi internal. samsung wameiga round corner tu wakashtakiwa ije kuwa kuiga kila kitu hadi internals. na kampuni kubwa always wana vitu ambavyo vipo kwao tu mfano.
1.nokia camera yake ni pureview
2.ya motorola clearpixel
3.htc ni ultrapixel
4.isocell tunaipata camera ya samsung
5.kwa sony tunapata ois ya software

kila kampuni na tech zake zinatofautiana na kampuni moja ikitaka kutumia tech ya mwenzake inabidi ilipie.
 
wee unaangalia tu battery kweli watu wanaangalia chipset ndo kitu ya kwanza...
Hivo ujue hapa unapoongea sio watu anti-tecno bali watu anti Mediatek

Duh! Watu wanaponda mediatek wakati wanatumia laptops za celeron .. hahahaha. Tz tutengeneze basi chipset zetu wenyewe ili tuonyeshe ujanja wetu si kwa maneno tuu
 
just taja simu yoyote iwe challenge kwangu maana nikitaja mimi munaweza sema ni coincidence.

Inawezekana wamekopy . Kwani hata dell haiwezi kufanana na toshiba? This is still not a reason. Huu ni mtazamo sa fulani. May be tecno is good that is why has been copied
 
Hawalalamiki matatizo wanalalamika hawajui kutumia e.g ku-enable internet kwenye S4 ni moja ya thread ambazo nimekutana nazo

Mmh! Pitia tena. Kuna thread hapo nadhani ya jana. Mambo ya low memory. Na thread zingine zipo za kitambo za samsung, htc.....
 
Duh! Watu wanaponda mediatek wakati wanatumia laptops za celeron .. hahahaha. Tz tutengeneze basi chipset zetu wenyewe ili tuonyeshe ujanja wetu si kwa maneno tuu

kaka its not about power tu kwani snapdragon 200 na 400 zina power kubwa? zinapitwa na baadhi ya chip za mediatek ila still tunarecomend hizo sababu ya features. nimetoa mfano hapo juu even wachina wenyewe kina xiaomi, zte, huawei hawatumii mediatek kwenye simu zao nzuri wote wanaenda qualcom au custom made chip je na hawa ni haters pia?
 
Hebu pitia jf uone watu wanavyolalamikia samsung galaxy ....

kama nilivyosema hapo juu touchwiz ina matatizo ya kula ram hili linajulikana sio siri na kuna kosa kubwa watu wanafanya ambalo wanaangalia ukubwa wa ram ya simu badala ya kuangalia free ram, ila ukitaka kuona mediatek ni takataka hebu shika htc sense uone kitu kinavyoteleza au stock ya motorola au nexus, nunua samsung isio na touchwiz kama s4 version ya stock au tafuta miui au hata hio samsung toa touchwiz eka custom rom kama omni au cyanogen
 

OUT OF TOPIC BRO
Nimeona aijibiwi kwa muda mrefu nataka niflash simu yangu huawei y 300 ni ya tigo iwe multchip sasa nimejaribu kuuliza nkaambiwa kuna uwezekano wa kutokea error nyingi
Sasa naomba unipe ushauli wako kaka NIFANYEJE
 
Inawezekana wamekopy . Kwani hata dell haiwezi kufanana na toshiba? This is still not a reason. Huu ni mtazamo sa fulani. May be tecno is good that is why has been copied

haziwezi kufanana na siku mmoja akimcopy mwenzake ujue kesho yake anapelekwa mahakamani.

kaka hebu nioneshe patent hata moja ya tecno wameregister kokote kule kuwa wameinovate kitu
 
OUT OF TOPIC BRO
Nimeona aijibiwi kwa muda mrefu nataka niflash simu yangu huawei y 300 ni ya tigo iwe multchip sasa nimejaribu kuuliza nkaambiwa kuna uwezekano wa kutokea error nyingi
Sasa naomba unipe ushauli wako kaka NIFANYEJE

kaka sina experience na hilo ni vyema ukapata experience ya mtu mwenye hio simu halafu ameunlock. pia nimeskia una unlock kwa code hivyo nafkiri itakuwa haina error yoyote
https://www.jamiiforums.com/tech-ga...atumia-line-moja-itumie-line-zote-urgent.html
 

nipo nafyonza ilmu..
ahsanta sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…