TECNO CAMON C9 yaingia sokoni kwa kishindo

TECNO Tanzania

Senior Member
Jul 6, 2016
192
216
Simu kali ya Tecno Camon C9 yenye uwezo wa hali ya juu katika kupiga picha ikiwa na Camera mbili (Mbele na nyuma) za Megapixel 13, uwezo wa 4G LTE na teknolojia mbali mbali za kisasa imeingia rasmi sokoni. Simu hii ni miongoni kwa simu za kisasa kuingizwa nchini, na inapatikana kwa bei ya kawaida ya Tsh.400,000





Wateja wamefurika kwa wingi dukani ili kujipatia simu hii mpya ambayo ina sifa kede kede iwe ni kwa wale wanaopenda selfie au wale wenye uhitaji wa simu yenye uwezo wa kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja.

IMG_2736.JPG

Kwenye Picha: Wateja wakipata ufafanuzi kuhusu Camon C9 katika duka la Tecno kabla ya kujipatia C9

Wateja walipata bahati ya kushinda zawadi mbalimbali kufuatia droo iliyochezesha katika ofisi za Tecno. Wateja wengi waliweza kujishindia zawadi zikiwemo Microwave, feni, subwoofer huku zawadi kubwa kabisa ikiwa ni TV ya nchi 43.

IMG_2734.JPG


SIFA ZA CAMON C9


Baadhi ya sifa za Camon C9 inayouzwa katika maduka ya Tecno ikiwa katika rangi 3 tofauti ni hizi;


Camera ya hali ya juu

Kama mpenzi wa picha Camon C9 imekupa Camera unaihitaji kwani inaweza kutambua sura na kupiga selfie kali hata ukiwa gizani. Pia Camera yake ina urembo wa kweli (make-up) ambayo itafanya picha zako kuwa na mvuto wa asili.

IMG_2741.JPG


Pia Tecno Camon C9 itaondoa issue za selfie kutokuwa kati kwa kutumiacamera iliyo katikati ya simu ambayo inaitwa ‘The Perfect Selfie camera’. Simu hiyo ya Camon C9 inakuja na kifurushi cha 10GB kutoka Vodacom Tanzania ambao hivi karibuni wameboresha mtandao wa 3G nchi nzima na kuzindua 4G kwa maeneo ya Dar es Salaam.


Watu wengi ndani ya selfie moja

Tecno Camon C9 ina uwezo wa kujaza watu wengi kwenye selfie moja kuliko simu yoyote duniani. Camera ya C9 inachukua angle kubwa zaidi hivyo kukuwezesha kupata selfie nzuri hivyo kuchukua watu wengi zaidi.

IMG_2735.JPG


Simu hii inapatikana katika Exclusive Showroom yetu iliyo karibu yako

· Mbeya - Boaz Mwakyama

· Mwanza - Nyerere Road Round About Pamba Mwanza

· Arusha - Block H , Area F - Makongoro Street

· Dar Es Salaam - City Mall, iliyopo kona ya Bibi Titi, Morogoro Road..


Unaweza kutembelea kurasa zetu kujua zaidi.

· Facebook: TECNO Mobile

· Instagram: TECNO Mobile Tanzania (@tecnomobiletanzania) • Instagram photos and videos

· Twitter: TECNO Mobile TZ (@TECNOMobileTZ) | Twitter
 
Mmetaja tu sifa ya camera..
Bado sifa hiyo haiwezi kumvutia sana mteja!!
Weka full specification....
 
Hajaweka phone specifications kakomalia camera mara selfie,, weka full specification ueleweke
 
Safii tecno...japo mp 13 kwa front camera ni zaidi ya kawaida.
 
Kuna rafiki yangu aliwahi kuniambia Tecno ni simu ya kununua wakati wa mapito mfano kama simu yako imeibwa, imepotea au imeharibika wakati ambao hujajipanga vizuri kununua simu nyingine:rolleyes:
Kabisa ndg ingawa bado siamin hata huo muda wa mupito nitakuwa comfotable
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom