Technically Inawezekana? Online Whatsapp but Mtu Kalala

Lady Ra

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2014
Posts
886
Reaction score
1,010
Wadau,

Happy New Year,

Msaada unahitajika please, Last night nilistuka usiku usingizini kama kawaida maana sio mara ya kwanza.

Then hupenda kuangalia saa ngapi kwenye simu, then whatsapp, Jamiiforums, Facebook vyote hupitia kutafuta usingizi.

Sasa basi nilishangaa kumuona Shemeji Yenu yuko "online" kwenye whatsapp muda huo then nikaamua kumpigia kumuuliza kulikoni.

Simu haikupokelewa kabisa, na kwa ushahidi nikarudi kwa whatsapp namba au conversion yake ku-screenshot ile "online" status then nikamtumia although ilionyesha double tick zisizo za bluu kwamba Imefika ila haijasomwa!!

Sasa basi asubuhi alikuja na utetezi kua alikua amelala kweli, ila ile online status ni kwa vile tu alikua akiandika kitu kwa whatsapp then hakumalizia Wala hakuondoka hapo kwenye writing board ndio maana alionekana online.
 
Sasa nachouliza hii kitu inawezekana? Mtu awe kalala lakini whatsapp ionyeshe online Kisa tu aliiacha simu ikiwa kwenye whatsapp sehemu ya kuandikia?
 
Duh. Kweli madogo mna kazi. Sio ajbu mnakuja huku kuuliza namna ya kutongoza
 
inawezekana mtu akawacha whatapp online na ukamtumia messege na kwako ikaonyesha tiki mbili za blue,hata kama hajasoma inawezekana alipitiwa na usingizi wakati anachati kutumia whatsapp.
 
Natumia whatsapp 2 kweny simu yangu,nimejaribu ku fanya kama jamaa alivyosema,ni kweli mtu ukiacha ktk writing board inaonesha upo online
 
Sasa nachouliza hii kitu inawezekana? Mtu awe kalala lakini whatsapp ionyeshe online Kisa tu aliiacha simu ikiwa kwenye whatsapp sehemu ya kuandikia?
usijali kwa maelezo yake yanaonesha bado yupo njia kuu na wala hakuzarau call yako.
 
Ina maana unataka kumtawala hata kuingia mitandao ya jamii akuombe ruhusa? Acha upuuzi hata aliyemzaa hajawahi kufanya hiyo. Kwanza hujamuoa ndo maana hata hamkuwa pamoja japo unasema semeji yenu!!!. Jirekebishe na aina hii ya wivu. Utaachika saaana. Hakuna tena wanawake wa kukuomba ruhusa kabla ya kuingia mtandaoni. Aaaibu !! Hata wewe !!!!!!
 
Anyway, Naona umeandika kwa kunikandia ila nitakujibu kistaarabu tu.

Kwanza kutokua pamoja haina maana sijamuoa au hajanioa. Pengine amesafiri kikazi au likizo za mwisho wa mwaka hajarudi bado.

Pili, Si kwamba namtawala au nampangia kuingia kwa whatsapp, bali nilishangaa nashtuka saa nane usiku yuko" online". Nimeuliza tu simple kua technically hii inawezekana?

Swali haliko kimahusiano zaidi ndio maana sikulipeleka MMU, Bali lipo ki-teknolojia zaidi kwa wataalam wa Whatsapp!!
 
Natumia whatsapp 2 kweny simu yangu,nimejaribu ku fanya kama jamaa alivyosema,ni kweli mtu ukiacha ktk writing board inaonesha upo online

Si kwamba unapoingia kwenye whatsapp SENDER kuangalia status ya RECEIVER basi ndio unakua online pia kwa hiyo RECEIVER?

Kwamba kabla hujafungua SENDER basi zote zilikua offline? Nafikir labda ingefaa kuangalia kwenye simu tofauti!!
 
Inawezekana, obviously WhatsApp haijui kuwa umelala au upo macho. Ukiwa ndani ya App yenyewe ndo inasema Online, pia hizi ni program tu ziba bugs kibao so usishangae ikasema online wakati hata simu haipo on.

Kuhusu swala lenyewe naona mnajitafutia stress za ajabu sana, sasa angekwambia anachat na mtu ungereact vipi? tupeane space jamani!!!
 
inawezekana mtu akawacha whatapp online na ukamtumia messege na kwako ikaonyesha tiki mbili za blue,hata kama hajasoma inawezekana alipitiwa na usingizi wakati anachati kutumia whatsapp.

Akiiacha hivyo tuseme hata kwa siku mbili kama chaja na bundle inaruhusu, lakini bila kuigusa simu hata kidogo,

Nami nitaendelea kumuona online tu muda wote huo?
 
Mtoa Mada Hata Hueleweki, Kwanza Kilichokufanya Kushangaa Ni Nini Kama Wewe Uliweza Kuwa Online Hiyo Usiku Mwingi Kwanini Yeye Ashindwe!? Nikiliacha Hilo, Jibu Ni 'Ndio Inawezekana' Mimi Binafsi Whatsap Iko Online Muda Wote Ikiwa Sija Switch Off Apps.. Hata Kama Nimelala, Apps Hailali.
 
Yap inawezekana kabsa....kua mpole bbie
 
Wivu utawaua jamani, kama huamini fanya experiment nawewe utajua ukweli
 
Anyway, Naona umeandika kwa kunikandia ila nitakujibu kistaarabu tu.

Kwanza kutokua pamoja haina maana sijamuoa au hajanioa. Pengine amesafiri kikazi au likizo za mwisho wa mwaka hajarudi bado.

Pili, Si kwamba namtawala au nampangia kuingia kwa whatsapp, bali nilishangaa nashtuka saa nane usiku yuko" online". Nimeuliza tu simple kua technically hii inawezekana?

Swali haliko kimahusiano zaidi ndio maana sikulipeleka MMU, Bali lipo ki-teknolojia zaidi kwa wataalam wa Whatsapp!!
sikia,ukiacha ktk writing board itaonesh upo online,just try it yourself
 
Mtoa Mada Hata Hueleweki, Kwanza Kilichokufanya Kushangaa Ni Nini Kama Wewe Uliweza Kuwa Online Hiyo Usiku Mwingi Kwanini Yeye Ashindwe!? Nikiliacha Hilo, Jibu Ni 'Ndio Inawezekana' Mimi Binafsi Whatsap Iko Online Muda Wote Ikiwa Sija Switch Off Apps.. Hata Kama Nimelala, Apps Hailali.

Kilichonifanya kushangaa ni yeye kudai alikua amelala ndio maana hakupokea simu wakati whatsapp yake ilikua inaonyesha yuko online
 
Back
Top Bottom