Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,564
- 7,973
Kama umemaliza kibaha special xul na umepata A tatu na B nne(wani ya 11) basi utakua kilaza sana,wengine tumepiga Aza boy(One ya 9) tukaenda huko kibaha tukalamba one ya 3,jipange mkuu,achana na tek nenda mzumbe au ilboru ukapige tatu yako chuo ukachukua(UDSM) CIT au Telecomm Eng zen piga GPA yako above 4.5 ubakizwe pale ule maisha,tech hakuna kitu kuanzia DIT,MTC,ATC kote famba elimu rahisi sana na ukija chuo umetoka tek yani unakua mweupe sana! Soma dogo one ya 11 isikuchanganye max ndogo sana hizo!!!
Mkuu naona sasa hapa unatafuta kufanya mashindano yasiyokuwa na tija yoyote kwako, kwa huyo dogo na wanajf wote kwa ujumla.
Nataka nikuhakikishie kwamba usijaribu kui underate elimu ya FTC hata kidogo, ile kitu ni kiboko yake. Lakini kwakuwa unaamini kwamba A level ndio kiwango, basi baki ukiamini hivyo hivyo na sisi tuliopiga FTC tubaki tukiamini kwamba ndio kiwango. FTC anaingia aliyefaulu tu na unaanza kujengwa katika taaluma yako mapema na hata ukienda chuo kikuu unakuwa unaongezea tu ujuzi.
Kwani mwisho wa siku wote ni wahandisi right now, na maisha tunayasongesha bila matatizo hadi unaona sasa tuko hapa jf kubadilisha mawazo na kupigania ukombozi wa watanzania toka kwa mkoloni mweusi ccm.