technical college vs A-level | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

technical college vs A-level

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by deni, Feb 15, 2012.

 1. deni

  deni Senior Member

  #1
  Feb 15, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 182
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  hello wana jf.
  mimi nimemaliza form 4 mwaka jana.
  matokeo yangu ni mazuri nna dvn 1.11 na AAA PCM.
  nilichagua tech colleg(DIT) first choice.nadhani engineer aliyesoma diploma halafu BA ni safi zidi ya alietoka A-level halafu akachukua BA.tatizo watu wengi wananikatisha tamaa na kusema huko colleg si kwa watu wenye ufaulu kama wangu wanasema huko ni kwa waliofaulu kwa kiwango kidogo.....yaani wengi wananiona wa ajabu wanasema kupitia huko ni kujiharibia kwani ajira zinasumbua kwa waliopitia huko.
  najisikia vibaya naona kama nibadilishe baada ya matokeo kutoka.sio kwamba siwezi A-level bali nahisi njia ya ttech colg kwa engineerig ni nzuri zidi.

  kwa hiyo naomba anayefahamu zaigi anielezee hili swala la A level na tech colg.je mimi nipo sawa au wao wapo sawa
   
 2. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #2
  Feb 15, 2012
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,407
  Likes Received: 3,737
  Trophy Points: 280
  Asikudanganye mtu.............. hebu fikiri hili........... Nimesoma Ifunda Tech, nikapiga wani ya 16, Nikaenda Mbeya Tech nikapiga za kuniwezesha kuingia versity, na baada ya hapo nikaunga Faculty Of Engineering ya UDSM na ajira ya kwanza niliipata nikiwa bado chuo (mwishoni mwishoni). We nenda na interest yako, ukiangalia nani alipata nini kwa kupita alikopita utapotea...... KILA FANI NA KILA NJIA INA WALIOLOST NA WALIOBUTUA........... inategemea tu wewe rolu modo wako ni nani kwenye fani hizo na alipita wapi. Kimsing FTC utasoma miaka 3 wakati form 6 miaka 2. Mimi nakushauri pita TECH COLLEGE. ANayekueleza huko wanaenda waliofeli hajui kitu. Kwa taarifa yako na hao wengine...... KUTOKA TECH COLLEGE KWENDA UNIVERSITY ENZI ZETU ILIKUWA LAZIMA UWE NA AVERAGE YA B KATIKA MASOMO SITA UNAYOFANYIA MTIHANI WA MWISHO, NA LAZIMA UPATE B YA HESABU.............
   
 3. +255

  +255 JF-Expert Member

  #3
  Feb 15, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,908
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Sipo mbali sana na mawazo ya Ngali, nenda Tech auanze kuwa professional mapema, unaweza kwenda A'level af mwisho wa siku matokeo yakawa mabovu ukaja kukosa qualificati za kujiunga na chuo.
   
 4. mchambuzixx

  mchambuzixx JF-Expert Member

  #4
  Feb 15, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 1,294
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  wewe nenda chuo siku hizi necta hakueleweki hapo kachukue diploma yako cku hzi kuna uhaba wa technician then unaweza kujiunga chuo baada ya kupata diploma yako ...A-LEVEL ni bahati nasibu mambo mengi mda mchache na ni moja ya elimu NGUMU kuliko zote tanzania unahitaji sana kutulia ukiwa A-LEVEL bora uende DIT hao wanaokwambia wanakupa mawazo mgando
   
 5. Eghorohe

  Eghorohe JF-Expert Member

  #5
  Feb 15, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 222
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Dogo uko sahihi kabisa nenda DIT nani kakudanganya eti wanaenda wasio na ufauru hebu chukua hatua fanya utafiti matokeo ya mwaka huu utaona zaidi ya mamia ya watu wenye Division ONE & TWO wanachaguliwa DIT,mimi Nimehitimu pale mwaka juzi Bachelor of Engineering kwa sasa nasoma Masters UD ndo nawafundisha wenzangu hesabu kisa nimetoka DIT, tulitoka O-level Musoma Tech watu 15 division one zilikuwa 9 wote tukaingia DIT tena ulizia jina la Wambura Matiko aliingia DIT na Division one point 8 nani anasema wanaenda wasio na ufauru mzuri, wiki chache kabla hatujamaliza Diploma makampuni yalikuja kufanya booking tumemaliza tu Barrick,TBL na mengine wakatuajiri tumekusanya hela faster tukawajengea wazazi wetu wakaachana na nyumba za nyasi wengine tukarudi DIT wengine wakaenda Udsm tukapiga shule,nab ado tunapiga shule tukiwa na kazi zetu nzuri na biashara pia bado mayanki huko nje kila mara tunafunga mikanda tunakwea pipa kwenda majuu! Hayo ni matunda ya DIT. Nakumbuka mwaka Fulani tulienda kufanya Field sehemu mwanafunzi wa mwaka wa NNE Electrical Udsm hajui kutumia Mita(Multimeter),hajui kupima hata Diode,kwenye Engineering Udsm wanauza chai tu DIT iko juu!
   
 6. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #6
  Feb 15, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  We dogo,ukipata dit pachangamkie,achana na mambo ya pcm hayo!utapoteza muda thn mwsho wa cku waja kuandikiwa dv iv.
   
 7. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #7
  Feb 15, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Swadakta mkuu, kuna tatizo kubwa sana la uelewa wa watu juu ya tofauti ya hivi vyuo vya ufundi mchundo-DIT, TCA, MIST, NIT, RWI na Karume cha Zanzibar na vyuo vya ufundi stadi VETA.
  Nadhani hii inachangiwa na VETA kuwa kimbilio la waliofeli sekondari, na kwakuwa watu wengi hawaelewi tofauti kati ya ufundi mchundo na ufundi stadi, basi wanajikuta katika mtazamo potofu kwamba anayekwenda kupiga ufundi mchundo (FTC-sasa OD) amefeli wakati ukweli wa mambo ni kinyume chake.

  Kweli aisee huyo wambura nadhani bado yupo DIT kama Tutor, aliajiriwa hapo chuoni mara tu baada ya kupata mchundo (FTC), baadae alisoma bachelor of engineering hapo hapo DIT. Kuna mtu kaniambia anasoma masters sasahivi. Hata performance yake ya FTC na B.Eng ilikuwa ya juu sana, nadhani alikuwa overall best student.
   
 8. A

  Aaron JF-Expert Member

  #8
  Feb 15, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 2,122
  Likes Received: 2,721
  Trophy Points: 280
  Tuko pamoja' me nataka kuchukua IT hapo dit.. inalipa?? Plz ushauri wenu.
   
 9. Eghorohe

  Eghorohe JF-Expert Member

  #9
  Feb 15, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 222
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  @ Aaron Wengi wanachanganya kati ya IT na Computer Engineering,kama sijakosea au hakuna mabadiliko kozi ya IT ni certificate ya mwaka moja tu haina ugumu wowote sio lazima Physics na hesabu hata history nadhani ni poa tu ukimaliza hauna sifa za kujiunga na digree, tofauti na Computer Engineering ambayo ni Diploma miaka 3 ukimaliza na kufauru unajiunga na kufanya digrii chuo chochote utakapopenda lazima ujipinde vilivyo na lazima uwe umesoma sayansi Physics,Math n.k
   
 10. A

  Aaron JF-Expert Member

  #10
  Feb 15, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 2,122
  Likes Received: 2,721
  Trophy Points: 280
  baada ya kupata certificate ya IT unaweza kusoma diploma??
  Nisaidie pia qualification za labaratory technician hapo..
   
 11. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #11
  Feb 15, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Acha uongo wewe one ya kumi na moja usingekuja kuomba ushauri hapa,maana wengi mnaopiga max hizo mnawaza ilboru,mzumbe & kibaha,swali la kizushi kwani wewe 1st choice ulijaza nini?
   
 12. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #12
  Feb 15, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kwanza hongera sana kwa ufaulu wako mzuri. Inachotakiwa ni kutimiza ndoto zako kikamilifu, kama kweli unataka kuwa engineer kwenda Tech College ndio njia sahihi.
   
 13. deni

  deni Senior Member

  #13
  Feb 15, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 182
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  king kong acha dharau.nimemaliza kibaha pale na wengi niliomalizanao wana mawazo ya kurudi kibaha au kwenda elboru,mzumbe.....lakini mi ni wa tofauti.mimi first choice nilichagua college.
   
 14. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #14
  Feb 15, 2012
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 7,125
  Likes Received: 23,734
  Trophy Points: 280
  Deni asikuchanganye mtu hapa, wewe fuata hisia zako zinakokuelekeza; utafanikiwa tu. Ni wengi tuliopitia DIT na mafanikio yake tunayaona...tunabeba box na kula bata huku ughaibuni...sitakaa niisahau ile chuo!.
   
 15. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #15
  Feb 15, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Kwanza hongera kwa kufaulu vizuri pcm. Mimi nakushauri kama inawezekana nenda a-level. Kama uwezo unao na lengo ni baadae kuwa engineer sioni ni kwa nini upoteze mwaka mzima kupita college. Naamini kwa kusoma pcm utakuwa na flexibility au choices za engineering na kwengineko wakati college unaweza jikuta unajikita zaidi kwenye fani moja na kukuwia vigumu kubadilisha kama ukitaka. Sijui kwa sasa, lakini miaka ya nyuma kidogo ilikuwa rahisi zaidi kwa watu wa a-level kwenda chuo kuliko wale wa college.
   
 16. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #16
  Feb 15, 2012
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 7,125
  Likes Received: 23,734
  Trophy Points: 280
  Unaweza ikawa na isiwe kweli, kuna watu nawafahamu walisoma DIT FTC za Electrical Eng na walipoenda mlimani wakabadilisha na kusoma Mechanical Eng. Kuna mwingine alisoma FTC ya Lab Tech na baadae huko apoenda akabadili na sasa hivi ni Dentist, kwa hiyo ni vipi unaplan mambo yako!.
   
 17. Nyaluhusa87

  Nyaluhusa87 JF-Expert Member

  #17
  Feb 15, 2012
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 1,288
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Kwa sheria ya sasa ya TCU ukimaliza diploma lazima ufanye kazi kwanza kwa muda muda wa mwaka 1 ndo uende ukachukue degree so,kama unampango wa kuunganisha baada ya kumaliza dip hapo itakusumbua kidogo...hio njia ni nzuri 2 na wengi 2 wanafanikiwa kupitia hio njia.cha maana jipange na uamue ni wapi upite.good luck
   
 18. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #18
  Feb 16, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Upo sawa tu...lakini kwa sehemu kubwa hizo unazosema zaidi ni isolated cases...wengi (I will dare to say over 80%!) wanasoma kile walichosoma FTC au kinachoendana nacho kwa karibu....lakini nakubaliana na wewe suala kubwa ni juhudi katika kila unachofanya na kimsing hata huyu Deni anaweza kuwa mmojawapo wa hizo ninazosema isolated cases. Sehemu nzuri ya kuanzaia kwa vijana hawa kama wanapata nafasi ni kusoma prospectus za vyuo mbalimbali na kuona sifa zinazohitajika kujiunga na fani mbalimbali ambazo wana interest/wanaweza kujenga interest nazo!
   
 19. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #19
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Kama umemaliza kibaha special xul na umepata A tatu na B nne(wani ya 11) basi utakua kilaza sana,wengine tumepiga Aza boy(One ya 9) tukaenda huko kibaha tukalamba one ya 3,jipange mkuu,achana na tek nenda mzumbe au ilboru ukapige tatu yako chuo ukachukua(UDSM) CIT au Telecomm Eng zen piga GPA yako above 4.5 ubakizwe pale ule maisha,tech hakuna kitu kuanzia DIT,MTC,ATC kote famba elimu rahisi sana na ukija chuo umetoka tek yani unakua mweupe sana! Soma dogo one ya 11 isikuchanganye max ndogo sana hizo!!!
   
 20. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #20
  Feb 16, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Labda nikusaidie tu kwamba hivi vyuo vya elimu ya juu tunavyovizungumzia hapa vya calibre ya DIT (Tertiary institutions) haviko chini ya TCU, hivi viko chini ya NACTE.

  Jambo la pili, kama kweli TCU wanayo sheria ya kuwalazimisha waliomaliza diploma wafanye kazi walau mwaka mmoja kabla ya kuendelea na degree ningependa kuifahamu ni sheria namba ngapi na kama utanisaidia kuipata nitashukuru sana, lakini kuna watu ninawafahamu vizuri,labda niseme hata mdogo wangu amemaliza diploma na akaingia chuo kikuu moja kwa moja bila kufanya kazi mahali popote.

  Kama itakuwepo sheria ama kanuni ya namna hiyo, basi TCU watalazimika kuwahakikishia ajira wahitimu wa diploma, kwakuwa suala la uhaba wa ajira nchi hii kila mtu analifahamu.

  Ninachokumbuka ni serikali kuingiza kinyemela kigezo cha kutowapatia kipaumbele cha kupata mikopo kwa wanafunzi waliomaliza diploma kwa kisingizio kwamba wengi wanakuwa wameajiriwa kwahiyo watumie waajiri wao na mifuko ya pensheni kupata ufadhili, kitu ambacho si kweli na hiyo imepelekea wanafunzi wengi kukosa ufadhili kwa "umbumbumbu" huo wa watu wa wizara ya elimu.
   
Loading...