TEC yamjibu Asha Rose Migiro Kuhusu Kura ya Hapana

Hongera TEC kwa kusimamia ukweli..

Dini zimehusishwa kwenye mchakato wa Katiba kama hawajaridhika kwanini wasitupe maelekezo sisi waliotuwakilisha? Hii kauli ya kaizari mpe kaizari inaonekana pale wanapotoa msimamo wao tu! ajabu sana mkuu ......kesho tutaambiwa wasijenge shule wala hospitali maana si kazi yao bali ya Kaizari siyo?

Katiba si siasa .....katiba inagusa makundi yote na wote wana uhuru wa kutoa msimamo ....
 
nahisi hauna data mkuu..acha kupayuka payuka soma hapa na usirudi tena kiazi mkubwa..kardinali pengo aweka wazi msimamo wa kanisa - kitaifa - mwananchi.co.tz
kama hujui jambo uliza kwanza,acha kutukana.kanisa katoliki lina authorities.tec ndicho chombo cha juu kabisa cha kanisani katoliki tanzania.ina kauli ya mwisho.ndo nakufundisha sasa.pengo hana mamlaka yoyote juu ya tec.hebu google (catholic church authorities).mwisho,sina haja ya kusoma mambo ya kijinga,jielimishe kwanza juu ya mamlaka ya kanisa katoliki.ndipo utakapojua kuwa pengo kachemka sana,ni utovu wa ni nidhamu ambapo anastahili adhabu.usitukane hovyo tu!!!
 
Viongoz wa dini acheni siasa fanyeni kazi ya kueneza injili....mtu mzma anajielewa ktk maamuz yake hamna haki ya kumuamulia vinginevyo itakua kuherehere na ukuda

Kwani Injili ni kitu gani? Kama haigusi maisha ya watu na ustawi wao?
 
Kama Kiongozi wa Dini alipaswa atuhamasishe tuisome Katiba iliyopendekezwa na kuilewa kisha tufanye maamuzi sahihi bila kutushinikiza. Kwani ameamua kuonyesha mapenzi ya Ki-siasa na kutupa Dini pembeni.Kama Yesu angekuwa na Mapenzi ya aina hii basi...................................... Haya aliyasema kabla ya TEC na TEC wamekuja mawazo hayohayo na msemaji mkuu akiwa yeye.

Unajifanya mkristo kumbe hata Biblia husomi..

Katafute kwenye Biblia uniambie kwanini Yesu alimfananisha Farao (Rais wao) na Mnyama aina ya Mbweha!
 
Kwa wasio juwa cheo kikubwa katika kanisa na ndicho cheo cha mwisho ambacho ni askofu kwa hiyo hata papa cheo chake halizi na kikuuu ni askofu mkuu wa roma kwa hiyo wanaodhani pengo ni mkuu wa wakatoliki wanajidanganya tu pengo mwisho wake ni jimbo la dar es salaam
 
Hatupasu kuchaguliwa maamuzi na mtu yeyote au Taasisi yoyote. Watuache tuamue wenyewe.

Kwani hao akina Kikwete na viongozi wanapotuambi tuisome na tukapigie kura ya NDIO wanakuwa hawatuchagulii maamuzi? Kaka acha double standard,labda inabidi useme wazi kama una interest fulani katika hili.
 
Mbona CCM na serikali ya CCM inahamasisha kura ya NDIYO?Wewe si ni kibaraka wa CCM? Nijibu hilo swali..
Wote wanamakosa watuache tuamue wenyewe. Hapa si uchaguzi na wala sera hazihitajiki cha muhimu tuisome katiba pendekezwa kisha tufanye maamuzi sahihi ama hapana au ndiyo.
 
Nilimsikia huyo bwana, alikuwa anapotosha bila aibu, jamaa mmoja anayemjua vizuri alimpa maswali mengi akawa anajiumauma, yote tisa ni pale alipumuuliza kwamba aliwahi kugombea ubunge? Akajifanya hajasikia vizuri lakini ikabidi akubali na aligombea kupitia ccm. Kwa mazingira hayo alikuwa ni askofu au alikuwa anatetea katiba kama kada wa ccm? Na tabia hii ya kuleta watu kupotosha imekuwa ni kilema cha ccm, na bado utaona watalipa kikundi cha waislamu kuja kujenga hofu na kupotosha jamii kwamba maaskofu wanaipangia serekali kwa faida ya wakristu kumbe wao maaskofu lengo lao ni katiba nzuri ya wananchi. Ila ninachofurahi sasa hivi wananchi wengi wamejitambua hawakubali tena hizo propaganda za kizee. Na majibu halisi watayapata kwenye box la kura.

Hata Mimi nilimpuuza palepale yule MuCCM.
 
Unajifanya mkristo kumbe hata Biblia husomi..Katafute kwenye Biblia uniambie kwanini Yesu alimfananisha Farao (Rais wao) na Mnyama aina ya Mbweha!
Alimaanisha kuwa '' utawala wa Farao si kitu kwa Mungu''. Na maandiko yanasema mtu akikupiga shavu la kushoto mgeuzie na la kulia. Maana yake '' Ukitendwa kwa ubaya usijibu kwa ubaya''
 
Back
Top Bottom