TEC yamjibu Asha Rose Migiro Kuhusu Kura ya Hapana

unakumbuka pengo kuna wakati wa bmk aliunga mkono serikali mbili na akasema ndio msimamo wa kanisa je hiyo haki alipata wapi?
acha uwongo pengo hakusema kama huo ni msimamo wa kanisa ila alisema ni wake binafsi.kimsingi,wakati ule na sasa alikosea na aliropoka nje ya msimamo wa tec.msimamo wa tec ulikuwa "kukubaliana na mapendekezo ya rasimu ya warioba,ambao msingi wake ni wanachi.mwisho,unapoongea kitu brother jielimishe kwanza,usije kujifunzia humu jamvini.
 
ushoga siyo siasa ni zaidi katika maadili ya binadamu

Kwa hio wizi ni siasa? Ukiukwaji wa haki ni siasa?

Unatakiwa ujitambue unatetea nini kijana

Utatetea na visivyoteteeka

Viongozi rasmi wa makanisa yote Tanzania sio watu wa kukurupuka.TEC,KKKT na FPCT sio watu wa kukurupuka
 
Mkuu nilikuwa na refer kwenye issue ya kisiasa na kidini, hili la uzinzi ni 100% linahisiana na dhambi kidini, lakini hili la katiba linahusiana zaidi na mwenendo wa kisiasa. ni kama kuzuia kodi kwa kuwa kuna ufisadi au kukataa kuchagua kiongozi fulani wa kisiasa.

Hili la Katiba ni dhambi zaidi kwa sababu ni wazi ni mchakato ulioendeshwa kwa hila na haramu.

Pili ni mchakato uliopuuza kabisa maslahi halali ya wananchi na kuweka maslahi ya wachache

Ni mchakato unaozaa Katiba itakayoangamiza Taifa.

Sasa maaskofu kama manabii ni lazima waeleze wazi uharamia wa tukio hili ili kuliokoa Taifa.
 
Kwa kuwa Askofu Seveline Niwemugizi ameamua kujiingiza kwenye Siasa sasa twende kazi. Niwemugizi hana usafi wowote wa kumfanya awe msemaji wa Waumini wa Ki-Katoliki Tanzania kwa sababu zifuatazo:

1. Ametumia mabavu kuhamisha Makao Makuu ya Jimbo kutoka Rulenge kwenda Ngara, bila sababu za msingi na bila ridhaa za waumini. Huku ikisadikika ameamua kufanya hivyo ili kujisogeza karibu na Biharamuro alikozaliwa na kuchukua sadaka na misaada ya wahisani kwa maendeleo yake binafsi na kumuacha Mungu.

2. Jimbo limemshinda kuongoza kwa kutumia Roho ya Ki-Mungu na kuongoza Kondoo wa Mungu, Bali amesababisha mitafaruku ya Kiroho Jimboni. Mapadri wameamua kuwa na Ndoa zisizotambulika na kuongeza watoto mitaani, kama atabisha nitawataja ili kuweka mambo sasa.

3. Misaada yote inayotolewa na wahisani kwaajiri ya kusaidia watoto Yatima wanaolelewa na Masisita aliamua ipitie kwake, wahusika hupata kiasi kidogo sana au wakati mwingine hawapati kabisa.

4. Ameshindwa kumheshimu Mkuu wake Pengo! anafikiri sisi waumini tutamfuata nani?.

5. Alisababisha Dr. Mbasa, ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Biharamuro kukimbia Hospitali ya Rulenge na kukimbilia Biharamuro huku akijua ndiye aliyekuwa Dr. tegemeo katika Hospital hiyo.

Mwisho niseme ya Mungu tumpe Mungu na ya Kaisali apewe Kaisali.

Aliyekwambia kwamba Pengo ni mkuu wa Severin ni nan? Hayo yote uloyaeleza hata kama ni kweli hayaondoi credibilty ya kwamba aloyasema ni ukweli mtupu,harafu mbona unafanya personal attack? Sasa hebu tuambie alichokusema hakipo? Acha hizo hata kama ni mapenzi sio hivyo unapenda vibaya,Badilika!
 
acha uwongo pengo hakusema kama huo ni msimamo wa kanisa ila alisema ni wake binafsi.kimsingi,wakati ule na sasa alikosea na aliropoka nje ya msimamo wa tec.msimamo wa tec ulikuwa "kukubaliana na mapendekezo ya rasimu ya warioba,ambao msingi wake ni wanachi.mwisho,unapoongea kitu brother jielimishe kwanza,usije kujifunzia humu jamvini.
Nahisi hauna data mkuu..Acha kupayuka payuka Soma hapa na usirudi tena Kiazi mkubwa..Kardinali Pengo aweka wazi msimamo wa Kanisa - Kitaifa - mwananchi.co.tz
 
[QUOTE=Standalone; Alicho ongea pengo ni ushahidi kwamba, hana uchungu na kondoo! yeye ni mchungaji wa kulipwa tu!
 
Hili la Katiba ni dhambi zaidi kwa sababu ni wazi ni mchakato ulioendeshwa kwa hila na haramu.

Pili ni mchakato uliopuuza kabisa maslahi halali ya wananchi na kuweka maslahi ya wachache

Ni mchakato unaozaa Katiba itakayoangamiza Taifa.

Sasa maaskofu kama manabii ni lazima waeleze wazi uharamia wa tukio hili ili kuliokoa Taifa.

Umeandika vizuri sana Molemo.....Maaskofu ni Manabii...Ni mdomo wa mungu....Ole wake atakayepinga.
 
Nchi imefika mahala sasa inataka tuache kudanganyana. Kulazimisha mambo hakutayafanya yawe mazuri...kutayaharibu zaidi. Tukumbuke kuna leo na kesho.
 
Nyie ndio kama yule Jamaa aliyemuua Yohane Mbatizaji kisa tu hataki ukweliManabii katika kanisa hua hawapindishi maneno wanakupa ukweliWalimpa Ukweli Mfalme Daudi baada ya kutembea na mke wa Urio.......walimwambia live kuwa umekosea na Mungu atakuadhibuKanisa kama nabii lina haki zote za kuelekeza
Niliyoyasema ni kweli tupu, sema tu sisi Waumini wa Ki-Katoliki tunaamini kuwa wa mwisho kuhukumu Nafsi au Roho na matendo ya mtu ni mungu tu. Usiwe mvivu fuatalia yote niliyoelezea hapo juu kwa kujiaminisha zaidi.
 
makamu wa rais wa baraza la maaskofu wa kanisa katoliki tanzania (tec) ambaye pia ni askofu wa jimbo katoliki la rulenge mkoani kagera, seveline niwemugizi amesema, viongozi wa dini wana haki ya kuwaelimisha waumini wao waweze kujua kinachoendelea wanapoona kuna mambo hayaendi sawa katika jamii.

Askofu niwemugizi ametoa kauli hiyo siku moja baada ya waziri wa katiba na sheria, dk asha-rose migiro kuwataka maaskofu wasiwafundishe wananchi jinsi ya kupiga kura bali wawaache watumie haki yao ya katiba kupiga kura kulingana na utashi wao wenyewe.

"nimeshangaa kusikia kuwa waziri anasema viongozi wa dini hatuna haki ya kuwaambia waumini kuipigia kura ya hapana katiba inayopendekezwa, mbona serikali imewaambia wananchi waipigie kura ya ndiyo, haki hiyo wameitoa wapi," alihoji.

Namnukuu "sisi ni viongozi wa dini hatuwezi kuwaona kondoo wa bwana wanapotea halafu tukakaa kimya au kuwaacha, tutakuwa hatujatenda haki, lazima tuwaambie waweze kuondoka kwenye kundi hilo na waweze kujitambua,"

niwemugizi alisema pia wanayo haki ya kuwaambia waumini wao kuipigia kura ya hapana, katiba inayopendekezwa kwa sababu ni wajibu wao kufanya hivyo. Viongozi wa dini ni viongozi wa jamii hawawezi kuona waumini wao wanapotea halafu wanakaa kimya maana kufanya hivyo kutasababisha waingie kwenye uovu.

chanzo:
mtanzania

kauli hii imenifurahisha sana.askofu huyu ni genius!
 
Niliyoyasema ni kweli tupu, sema tu sisi Waumini wa Ki-Katoliki tunaamini kuwa wa mwisho kuhukumu Nafsi au Roho na matendo ya mtu ni mungu tu. Usiwe mvivu fuatalia yote niliyoelezea hapo juu kwa kujiaminisha zaidi.

Ninaweza kuapa wewe siyo muumini wa Kanisa Katoliki.Kama ni Muumini basi ni mfu kabisa na hustahili kabisa hata kuzikwa kikatoliki ukifa.
 
Mkuu nilikuwa na refer kwenye issue ya kisiasa na kidini, hili la uzinzi ni 100% linahisiana na dhambi kidini, lakini hili la katiba linahusiana zaidi na mwenendo wa kisiasa. ni kama kuzuia kodi kwa kuwa kuna ufisadi au kukataa kuchagua kiongozi fulani wa kisiasa.

Kama unafikiri swala la Katiba linahusana na siasa tu kwanini viongozi wa dini kwa makundi yao wanashirikishwa hatua zote za uandishi wa Katiba? kwanini uwape mipaka kwenye hili tu?
 
kauli hii imenifurahisha sana.askofu huyu ni genius!

Nimefurahi baada ya kusoma umekubali kuwa Huyu askofu alistahili kuwa Kiongozi wa TEC....By the way....Angalia juu hapo nimekuambia na nikakupa link ukasome Kauli ya Pengo Kuunga mkono serikali 2....

Ahsante mkuu.
 
leo asubuhi kulikuwa na askofu mmoja kwenye kipindi cha baragumu live anaitwa ikongo,alikuwa anaiwakilisha serikali akikanusha kwamba tamkon lile ni la wakatoliki na si la wakristo wote.

Mkuu uko sawa hata mimi nilimsikia ila kuna jamaa alimpiga maswali ya papo kwa papo akamshushua akamwambia yule askofu anawakilisha wanasiasa na sio waumini kwakua kumbe alishagombea ubunge sehemu
 
Aliyekwambia kwamba Pengo ni mkuu wa Severin ni nan? Hayo yote uloyaeleza hata kama ni kweli hayaondoi credibilty ya kwamba aloyasema ni ukweli mtupu,harafu mbona unafanya personal attack? Sasa hebu tuambie alichokusema hakipo? Acha hizo hata kama ni mapenzi sio hivyo unapenda vibaya,Badilika!
Kama Kiongozi wa Dini alipaswa atuhamasishe tuisome Katiba iliyopendekezwa na kuilewa kisha tufanye maamuzi sahihi bila kutushinikiza. Kwani ameamua kuonyesha mapenzi ya Ki-siasa na kutupa Dini pembeni.Kama Yesu angekuwa na Mapenzi ya aina hii basi...................................... Haya aliyasema kabla ya TEC na TEC wamekuja mawazo hayohayo na msemaji mkuu akiwa yeye.
 
Watu wengi wanadhani pengo ni kiongozi wa kanisa Katoliki Tanzania...Administratively

Administratively pengo sio Kiongozi wa kanisa....Kiongozi ni Baraza la Maaskofu ambapo Pengo naye ni askofu wa kawaida tu.

Kuwa Kardinali ni cheo unachopewa na Papa katika kusimamia Jimbo kuu la kanisa katoliki

Kuna nchi zina ma cardinal zaidi ya mmoja
Asante mkuu,kwa kuongezea tu na kuna Nchi hazina kabisa Cardinal Uganda ni mojawapo.
 
Kuna wakati CCM na serikali yake walisimama kidete kuwa katiba ya 1977 haikuwa na tatizo kabisa huku wapinzani na wanaharakati wakitaka katiba mpya. Baada ya kugeuka na kuanzisha mchakato wa katiba mpya msimamo ni kuwa katiba pendekezwa ipigiwe kura ya ndio. Utafika muda tena watakuja na msimamo kuipinga katiba hii hii. huu ni ukigeu geu.
sasa watu wengi wamegundua mapungufu ya hii katiba pendekezwa, wanafanya vizuri kuwatahadharisha wanachi, sasa kosa ni nini hasa? Kwa mujibu wa Migiro kosa ni kwa sababu wanaenda kinnyume cha serikali na si kwa kutoa elimu.
 
Kama Kiongozi wa Dini alipaswa atuhamasishe tuisome Katiba iliyopendekezwa na kuilewa kisha tufanye maamuzi sahihi bila kutushinikiza. Kwani ameamua kuonyesha mapenzi ya Ki-siasa na kutupa Dini pembeni.Kama Yesu angekuwa na Mapenzi ya aina hii basi...................................... Haya aliyasema kabla ya TEC na TEC wamekuja mawazo hayohayo na msemaji mkuu akiwa yeye.

Aliyoyasema ni sahihi au si sahihi?
 
Back
Top Bottom