Team Lowassa walikuwa disorganised!

alikuwa anakomaaa tu sababu ya pesa lakini hakuwa sawa kwa kazi ya urais
 



naamini akitaka avurugikiwe aende huko nje. ni salama kwake kubaki ndani. watu wasafi na wenye wapiga kura wengi ndio huwa na ujasiri wa kutoka nje ya chama na kufuatwa na watu.

kwa yeye akifanya hivo atakuwa amejilostisha zaidi. kila mtu anamcheka na kumshangaa.

nguvu ya mwanasiasa ni watu - wapiga kura. lakini yeye hana rekodi nzuri na wapiga kura - watu wa kawaida. ukitaka kujua kuhusu hili angalia alivyoshindwa kuwabeba akina batilda na sumari.

hao wapiga debe wenyewe wakipiga kura kwa siri wanaweza hata mtosa. na walipatikana kwa kupewa mapene na kuahidiwa nafasi pamoja na kutegemea nafasi - ubinafsi. ahadi za sampuli hii huwez kuzitoa kwa wapiga kura wote na wala huwezi gawa hela kwa wapiga kura wote
 

vp ule msemo wa huwezi zuia mafuriko kwa mikono umeishia wapi?
 
Kama mwaka mmoja lowasa alishaulia kuwa Na plan b akawa mbongo kweli yaliyotokea sasa no historian hawakuwa Na mkakati mbadala
 
Kwani timu ya Membe ndiyo ilikuwa imemtuma ama kumshauri team Lowassa kufanya mbwembwe zilizozidi kimpimo hadi kuwafanya wananchi kuanza kujisikia kichefuchefu? Mimi ninafikiri mzee wa maamuzi magumu na timu yake kwa kiasi kikubwa walijichafua wenyewe. Walijitia upofu na ukiziwi wakalewa ukwasi ambao hapana shaka ulisababisha mafuriko ambayo hata hivyo yameweza kuzuiwa kwa vidole viwili tu! Tunamshukuru Muumba kwa hilo. Ninakubaliana na mJF mmoja ambaye amesema zuio hilo limetupunguzia mafisadi kadhaa.
 
Ina maana kama lowasa alikuwa chaguo la wengi,mbona haongelewi popote?
Subiri uone tofauti ya CDM na ZZK na CCM na Lowasa...mimi nitamuongelea km ccm walivyomuongelea ZZK,Lowasa anaongelewa na wana CCM na wasio CCM kwa malengo tofauti kwa sasa NChi nzima.
 
usichojua ni kwamba hiyo disorgazation dio shida kubwa kwa ccm..akiwa ndani ya ccm.Msizo usiofungwa au kuweka ktk mpangilio ktk ndege huangusha ndege
 

Ufisadi ccm upo kila kona hakuna msafi wala Mtakatifu asiye na Dhambi ccm. Lowasa hajakwisha kwani Lowasa ni Tajiri isitoshe alikuwa kajiandaa Kwa Ajili ya kampeni ana pesa za kampeni na hazikutumika zilitengwa kutumika October na hatashiriki Uchaguzi pesa inabaki , kwenye kutafuta kuna kukosa na kupata alijiandaa kwa hilo ndiyo maana yupo ccm hana mpango wa kuhama kwenda popote.
 
Lowasa alizungukwa na money mongers na si wafuasi

Tambua kuwa Lowasa hata angekuwa na Timu kutoka Mbinguni asingepenya kwani Jk na watu wake walikuwa wanataka kumpenyeza Membe , lakini dk za mwisho wakabaini kuwa watachemsha vibaya endapo wangefanya hayo maamuzi ndipo wakahamia Kwa magufuli dakika za majeruhi , lakini hii haimpi Lowasa shida kwani ana vitega uchumi vingi hawezi kulala njaa maisha yataendea Kama kawa.
 
Hawa team ya Lowasa watakiwa wameenda kujitumbikiza baharini kuogopa aibu

Aibu ipi ? Kwenye kutafuta na kupata na kukosa , Lowasa alijua njama za kumwengua mapema hivyo alijiandaa Kwa lolote lile.
 
Lowasa yupo imara Kama Raila Odinga alijua mapema kuwa kuna kukosa ama kupata hawezi kuishi maisha ya shida alishajipanga vizuri siku nyingi Timu yake sasa wapo wamehamia Kwa magufuli maisha yaendelee.
 
''ilibidi mwana wa adamu asulubiwe ili unabii utimie'' ogopa sana watu wamekiuka taratibu za uteuzi wa kamati kuu ili wamuondoe mapema, kwanini wazee wa chama walikutana kwa dharura?, ilikuaje kamati ya maadili ifanye kazi ya kamati kuu kumkata mmasai? kwa iyo unaona jinsi unabii uliotabiriwa umetimia ndio maana hata wewe umepata cha kuandika apa jf, ukawa watapata kiki ya kampaini pia hata kama lowasa akisema wafuasi waingie mtaani itakuwa mambo ya nkurunzinza. kiujumla nazidi kuendelea kumuheshimu lowasa kwa uzalendo, uvumilivu na busara yake kunyamaza kimya waswahili wanasema ''mtu mzima akivuliwa nguo huchutama''
 
Na hii disorganisation imeingia rasmi ndani ya Chadema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…