Teacher (Movie)

decomm

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
726
655
Habari?

Moja kwa moja kwenye mada:

Jina la 'movie' silikumbuki wala 'sterling' wake.

Mwalimu wa shule ya msingi ama sekondari, anampenda sana mama yake (child mother love).

Kuna siku akawa yupo 'airport', akaingia maliwatoni, mara akavamiwa na maafisa waliovalia kiraia. Wakamwambia atachelewa ndege. Kabla ahajibu chochote akapewa vifaa vya kazi na maelezo ya haraka haraka kuhusu majukumu ya huko.

Akapewa '1st class ticket' Mwalimu akawa anashangaa tu maana hajui chochote...

Movie iliendelea lakini hatimaye wahusika waligundua waliyempa ile ticket na vile vifaa siye mhusika, mhusika halisi alikuwa naye maliwatoni hapo 'airport'.

Bahati nzuri Mwalimu aliifanya ile kazi vizuri. Huku wale maafisa wakimwinda ili kumuondoa kwenye jukumu ambalo si lake.

Naomba kama kuna mdau anafahamu jina ama 'sterling' sinema hii anitajie ili niitafute.

Natanguliza shukrani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom