TCU: Wahitimu wa vyuo 2024, fani za Biashara, Elimu na Sayansi za Jamii zaongoza kuwa na wahitimu wengi, matazizo ya kifedha sababu kukatisha masomo

TCU: Wahitimu wa vyuo 2024, fani za Biashara, Elimu na Sayansi za Jamii zaongoza kuwa na wahitimu wengi, matazizo ya kifedha sababu kukatisha masomo

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Wakuu,

Katika pitapita zangu mtandaoni, nimepitia tovuti ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) nimekutana na takwimu hizi za wahitimu wa vyuo nchini kwa mwaka 2024 ambapo fani za Biashara, Elimu na Sayansi za Jamii zinaongoza kuwa na wahitimu wengi, Pia usawa wa kijinsia unaimarika kwani idadi ya wanaume ni sawa na 50.1% huku wanawake ikiwa, 49.9%

Wanafunzi wa mwaka wa kwanza wanaongoza kwa kukatisha masomo, ambapo Sababu kubwa za kuacha chuo ni ukosefu wa fedha, mimba, matatizo binafsi, na kufeli mitihani. Wanawake wanaongoza kwa kuahirisha masomo, hasa kutokana na mimba na uzazi.

Wahitimu kwa Jinsia na Aina ya Umiliki wa Chuo (2024)


Umiliki wa ChuoWanawakeWanaumeJumla
Umma19,63321,03640,669
Binafsi11,01810,88321,901
Jumla30,65131,91962,570

Hii inamaanisha nini?

  1. Vyuo vya umma vinatoa wahitimu wengi zaidi. Zaidi ya 65% ya wahitimu wametoka vyuo vya serikali. Hii inashihira kuwa bado serikali ndio mtoaji mkubwa wa elimu ya juu nchini.
  2. Usawa wa kijinsia: Hakuna tofauti kubwa kwenye Idadi ya wahitimu wanaume na wanawake (50.1% wanaume, 49.9% wanawake). Hii ni hatua muhimu kwenye ukuaji wa usawa wa kijinsia katika elimu ya juu.
  3. Vyuo binafsi viko nyuma: Hata kama vipo vingi kwa idadi, havitengenezi wahitimu wengi. Ada kubwa, ubora wa programu au vikwazo vya kiuchumi kwa wanafunzi vinaweza kuwa sababu ya kuwa na idadi ndogo ya wahitimu kwa vyuo binafsi.

Wahitimu kwa Ngazi ya Elimu (2024)

Ngazi ya ElimuIdadi ya Wahitimu
Shahada ya Awali (Bachelor)42,889
Diploma8,328
Cheti (Certificate)6,051
Shahada ya Umahiri (Masters)4,851
PhD (Shahada ya Uzamivu)367
Stashahada ya Uzamili84
  • Wahitimu wa Shahada ni wengi zaidi (68% ya wote). Inaonesha kuwa shahada ndiyo lengo kuu la wanafunzi wa vyuo vikuu, pia ni kiwango cha msingi kinachohitajika kwenye soko la ajira.
  • Elimu ya cheti na diploma bado ni chaguo la wengi: Pamoja zinachangia zaidi ya 14,000 ya wahitimu. Hii inaonyesha bado kuna nafasi kubwa kwa mafunzo ya kati.
  • PhD na Stashahada ya Uzamili ni nadra sana: Wahitimu 367 kwa PhD ni chini ya 1%. Hii inaweza kuashiria changamoto za muda, gharama, au umuhimu wa kiwango hicho kwa sasa.

Ngazi ya Elimu kwa Kulinganisha tasisi za Umma vs Binafsi (2024)

Ngazi ya ElimuVyuo vya UmmaVyuo Binafsi
Cheti3,0652,986
Diploma3,7784,550
Shahada (Bachelor)29,68113,208
Stashahada ya Uzamili3945
Shahada ya Umahiri3,7571,094
PhD34918
  • Vyuo vya umma vinaongoza kwa shahada za kwanza na za juu (Masters na PhD). Hii inaonesha uwekezaji wa kwenye tafiti, walimu wabobezi, na miundombinu.
  • Vyuo binafsi vinaongoza kwenye diploma: Huenda ni kwa sababu vinajikita zaidi kwenye mafunzo ya kitaaluma na ya haraka kwa soko la ajira.
  • PhD kwenye vyuo binafsi ni wachache sana (18): Inaonyesha ama vyuo binafsi havina uwezo au havipei kipaumbele masomo ya utafiti na uzamivu.

Wahitimu kwa Fani ya Elimu (2024)

Fani ya ElimuIdadi ya Wahitimu
Biashara14,321
Elimu13,834
Sayansi za Jamii8,216
Afya na Tiba7,568
Sheria5,008
TEHAMA (ICT)2,722
Uhandisi1,953
Sanaa na Lugha (Humanities)1,887
Kilimo1,317
Habari, Mawasiliano1,125
Utalii na Ukarimu856
Sayansi Asilia na Hisabati837
Mazingira na Misitu759
Maktaba na Utafiti wa Kumbukumbu700
Usanifu Majengo na Mipango Miji598
Sayansi ya Maisha515
Madini na Sayansi ya Dunia354
  • Biashara na Elimu zinatawala, Hii inaashiria mahitaji makubwa ya walimu na watu kwenye biashara, lakini pia uelekeo wa wanafunzi kutafuta fani "rahisi kuajiriwa"
  • TEHAMA, Uhandisi, Sayansi na Mazingira ziko chini, Inaonesha changamoto za kufundisha fani ngumu, gharama za maabara, au upungufu wa wataalamu.
  • Sayansi ya Maisha na Madini ni nadra: Wanafunzi wengi hawachagui fani hizi, huenda kwa sababu ya ushindani mdogo wa soko au ukosefu wa uhamasishaji.

Hitimisho muhimu kutokana na tawimu hizi
  1. Vyuo vya serikali bado vina mchango mkubwa kuliko binafsi, hasa kwa elimu ya juu (Shahada na kuendelea).
  2. Usawa wa kijinsia umeboreshwa sana. Wanawake na wanaume wanahitimu kwa uwiano wa karibu.
  3. Shahada ya kwanza ndio njia kuu ya kuingia kwenye ajira. Wahitimu wengi zaidi wako hapa.
  4. Fani zinazopendwa sana ni Biashara, Elimu na Sayansi za Jamii. Fani ngumu kama Madini, Sayansi Asilia, na ICT zinapewa mgongo.
  5. PhD bado ni safari ngumu kwa wengi. Kuna wahitimu wachache sana, hasa vyuo binafsi.



Wanafunzi Wanaokatisha Masomo Katika Taasisi za Elimu ya Juu (Students' Dropout in University Institutions)

Dropout kwa Jinsia, Mwaka 2024

Mwaka wa MasomoWanawakeWanaume
1st Year~3,300~4,600
2nd Year~1,800~2,200
3rd Year~800~900
4th Year~400~300
  • Wanafunzi wengi hukatisha masomo mwaka wa kwanza na kupungua kadiri miaka inavyosonga. Hii inaonesha changamoto za awali kama:
    • Kukosa ada
    • Mabadiliko ya mazingira ya chuo
    • Kukata tamaa
    • Matatizo ya kiafya au kifamilia

Dropout kwa Aina ya Taasisi (Public vs Private)


UmilikiWanawakeWanaume
Public~4,500~5,000
Private~2,000~3,000

  • Vyuo vya umma vina kiwango kikubwa zaidi cha dropout ambapo huenda ni kutokana na
    • Idadi kubwa ya wanafunzi
    • Changamoto za ufadhili au msongamano wa wanafunzi
  • Vyuo binafsi pia vina kiwango kikubwa, hususani kwa wanaume.

Sababu za Dropout


SababuIdadi
Sababu za kifedha~4,600
Sababu binafsi (afya/mimba)~1,400
Utovu wa nidhamu~900
Kufeli mitihani~700
  • Sababu za kifedha ni kubwa zaidi (karibu 60% ya wote). Hii inaonyesha ugumu wa kumudu gharama za elimu.
  • Mimba na matatizo ya afya ni changamoto kubwa hasa kwa wanawake.
  • Nidhamu na kushindwa mitihani pia vinachangia lakini si sana.

Dropout kwa Ngazi ya Elimu

Ngazi ya ElimuWanawakeWanaume
Shahada (Bachelor)~5,000~6,000
Diploma~1,000~1,500
Cheti~500~800
Masters & PhDWachache mno

  • Shahada za awali zina dropout kwa kiwango kikubwa zaidi kwa sababu ndizo zenye wanafunzi wengi.
  • Ngazi za juu (Masters/PhD) hazina dropout kubwa — huenda ni kwa sababu wahusika wanakuwa wameshajitambua, ufadhili wa kifedha nk.

Uahirishaji wa Masomo kwa Wanafunzi katika Taasisi za Elimu ya Juu (Students’ Postponement in University Institutions)

Sababu za Kuahirisha Masomo (Postponement)


SababuIdadi ya Wanafunzi
Sababu binafsi (kiafya/kifamilia)~1,800
Mimba na uzazi~1,200
Sababu za kifedha~1,000
Sababu nyingine~700
  • Wanafunzi wengi huahirisha kwa sababu binafsi — afya, familia, matatizo ya kiakili nk.
  • Mimba/uzazi ni sababu kubwa kwa wanawake.
  • Masuala ya kifedha bado ni changamoto kubwa.

Postponement kulingana Umiliki wa Chuo (Public Vs Private)


Aina ya ChuoWanawakeWanaume
Public~3,000~2,400
Private~1,000~800

  • Kama ilivyo kwa dropout, postponement ni nyingi zaidi kwenye vyuo vya umma.
  • Wanawake huahirisha zaidi kuliko wanaume, hasa kwa sababu za uzazi.

Postponement kwa Sababu na Jinsia

  • Mimba na Uzazi: Zaidi ya 95% ni wanawake
  • Sababu binafsi: Wanawake wanaongoza
  • Sababu za kifedha: Wanaume na wanawake wanakaribiana
  • Sababu nyingine: Idadi ndogo kwa wote
Mimba na uzazi ni sababu ya kipekee inayowaathiri wanawake moja kwa moja. Hii inaonyesha haja ya huduma za afya ya uzazi vyuoni, pamoja na ushauri nasaha.

Hitimisho muhimu kutokana na takwimu hizi​

  • Wengi wanaokatisha masomo ni wa mwaka wa kwanza, huenda hawakujipanga au hawakutarajia changamoto wanazokutana nazo.
  • Sababu kubwa za kuacha chuo ni ukosefu wa fedha, mimba, matatizo binafsi, na kushindwa mitihani.
  • Wanawake wanaongoza kwa kuahirisha masomo, hasa kutokana na mimba na uzazi.
  • Vyuo vya serikali vina dropout na postponement kubwa zaidi, labda kwa sababu vina wanafunzi wengi, changamoto za misaada ya kifedha, au mazingira magumu ya kujifunzia.
 
Back
Top Bottom