Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,278
- 25,846
Katika tovuti ya Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) kuna tangazo hili:http://www.tcu.go.tz/images/documents/TANGAZO_UHAKIKI.pdf. Kimsingi,tangazo linatoa taarifa kwa umma kuwa kuna zoezi la uhakiki wa wanafunzi waliodahiliwa kwenye vyuo vikuu mbalimbali nchini. Inasemwa kuwa wapo wanafunzi waliodahiliwa kwenye kozi mbalimbali vyuoni wakati hawakuwa na sifa husika.
Tangazo linawapa taarifa wanafunzi kuwasiliana na vyuo vyao ili kuthibitisha kustahili kwao. Orodha ya wanafunzi hao wanaopaswa kuwasiliana na vyuo vyao tayari imetumwa vyuoni. Mwisho wa mawasiliano hayo ni Jumanne ijayo, tarehe 28 Februari, 2017. Wanafunzi husika wanapaswa kufanya kadiri ya tangazo hilo hapo juu.
Jambo la kwanza ni kwamba wanafunzi hawa walidahiliwa katika vyuo mbalimbali nchini kupitia TCU au NACTE. Inajulikana kuwa wenye sifa za kidato cha sita huomba udahili kupitia TCU. Wale wa astashahada na stashahada hupitia NACTE (naweza kurekebishwa). Ndiyo kusema, TCU imeshiriki kuwadahili wanafunzi wanaosemwa sasa kuwa hawana sifa stahiki za kozi fulani vyuoni.
Jambo la pili ni taarifa kuwa wapo wanafunzi walioorodheshwa ambao tayari wameshahitimu. Gazeti la leo la Mwananchi katika ukurasa wake wa 1 na 3 linaripoti kuwa wanafunzi wengi wa SAUT ambao TCU imewataja kukosa sifa kukosa sifa wamemaliza chuo, wengine miaka mitatu iliyopita. Kwahiyo, zoezi la uhakiki limechelewa.
Katika uga wa sheria kuna kanuni muhimu kuhusu tangazo na zoezi la TCU. Hii ni principle ya estoppel. Kwa kifupi: es·top·pel əˈstäpəl/ noun Law noun: estoppel; plural noun: estoppels

- the principle that precludes a person from asserting something contrary to what is implied by a previous action or statement of that person or by a previous pertinent judicial determination.