TCU na wizard ya elimu siwaelewi

Waliosoma diploma ya maabara, au Pharmacy hawaruhusiwi kusoma MD, Kwa wakati huo huo aliyemaliza kidato cha sita anaruhusiwa hivi nini hoja yao kuhusu hili?
Nadhani umejikanganya hapo.
Vigezo vya kusoma degree zote hapa Tanzania viko vya namna mbili. Kuna kigezo cha moja kwa moja (direct entry) hiki kinamuhusu mwanafunzi aliyemaliza kidato cha Sita na kufikia ufaulu wa kuingia chuoni kwa kozi husika. Kwa kozi zote za afya kwa sasa ni lazima awe kidato cha Sita awe amesoma PCB (ukiondoa Environmental health science ambapo hata CBG inakuruhusu). Na kuna kigezo cha kuzunguka (indirect entry) kinamhusu mhitimu wa diploma wa kozi ile ile ya degree anayotaka kusomea.

Kwanini Diploma ya Maabara, Famasia au Uuguzi nk haziwezi kuruhusu kusomea MD? Jibu ni moja tu, Diploma hizo hazikumuandaa mhusika kuja kusomea au kufanya kazi za fani ya MD.

Hali ni hiyo hiyo pia ikiwa mtu kasomea diploma ya Medicine halafu akataka kuja kusomea degree ya Maabara, Famasia au Uuguzi, hataruhusiwa.
 
Kwani wenye diploma hawajasoma form six boss?
 
Hawajasomaa ndio na kama walisoma basii walifelii na kama walifelii ni sawa na haakusomaa
Kuna waliofaulu wakachaguliwa vyuo vikuu kozi ambazo hazina soko,mtu anaona bora akasome kozi ya afya ngazi ya diploma sababu ya ajira. Nina jamaa yangu alisoma degree ya ualimu mpaka kamaliza,akaamua kwenda kusoma diploma ya Afya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…