TCU, mna nini na chuo cha Tumaini Makumira Mbeya?

May 5, 2018
7
20
Ngugu zangu,

Chuo hiki kinachoitwa Tumaini Makumira kituo cha Mbeya au SHUCO imekuwa ni tatizo katika Swala zima la elimu ya vijana wa Kitazania.

Tangu Mwaka 2017 katika kati, nimekuwa nikimwandikia Mkurugenzi Mtendaji wa TCU ili kuangalia chuo hiki kwa jicho la pembeni.

Nashukuru kwamba ukaguzi ulifanyika baada ya walimu 7 kuacha kazi kwa mkupuo mnamo February 2017 na kuondoka na course work za wanafunzi huku wengine wawili wakiacha mapema Novemba 2016.

Baada ya hapo nilishangaa kuona wanafunzi wanahitimishwa, ashukuriwe Mungu TCU iliamua kufuta uhitimishwaji ambao ungefanyika mwezi 12 mwaka.

Soma Attachements mbili uone kinachoendelea huko;

Ninaomba Serikali ifunge hiki chuo kama ilivyopendekzwa na kamati ya Quality Assurance ya TCU ili wanafunzi hao wakaendelee na masomo Tumaini Makumira Arusha.

Kwa sasa kuna wanafunzi 18 wanaotakiwa kufukuzwa chuo kwa kosa la kudai haki ya kuhamishiwa Arusha.

Serikali isifumbue swala hili macho, fedha nyingi zinatumika kusomesha wanafunzi hao.
 
Attachments

mmbangaya

JF-Expert Member
Jan 16, 2015
1,007
2,000
Niliwahi tembelea hicho chuo mwezi feb 2018. Kwa kweli hali ni mbaya wanafunzi hawasomi na kuna baadhi wanishi hostel za nje yaani wanachofanya humo hostel hawa wanafunzi wa kike ni balaa. Wanahitaji maombi kama siyo serikali kuingilia kati
 
Jephta2003

JF-Expert Member
Feb 27, 2008
5,311

Acha basi na wewe hivyo,yaani chuo kifungwe kisa una tofauti na uongozi uliopo madarakani,kikifungwa hao wafanyakazi wanaofanya kazi hapo kuanzia wafanya usafi mpaka uongozi wa juu wakale wapi?,kwa nini isiseme TCU iyafanyie kazi mapungufu yaliyopo ?
 
Oct 12, 2015
36
95
Najiuliza sana hivi vyuo vya makumira mbona vina usani usanii mwingi,mnaharibu sifa ya vyuo vingine ambavyo viko under makumira, mbeya campus kuna shida kubwa kweli,naimani mleta mada ,uongelee yote,kuhusu mitihani ilikuaje??mpaka kufikia wachungaji kutishia kuuana kwenye vikao vya senate.....
 
Makuku Rey

JF-Expert Member
Dec 31, 2013
2,440
2,000
Nshawahi kuona vyuo vya hovyo hapa nchini ila hiki namba moja "unyakyusa" umeua chuo
ha!ha!ha!ha!ha pia location ya chuo haikuangalia Wateja!kwa jiografia ya Mbeya chuo kinachoweza kukaa uyole ni kile kilichojengwa na serikali tu!sio private.
 
May 5, 2018
7
20
Hope ujumbe utawafikia wahusika
Ndicho tunachotaka,huwezi kuwaweka watoto wa watu pale halafu wakidai haki yao unatishia kuwafukuza,Fikiria tu kuna wanafunzi hawajahitimu tangu mwaka jana,kwa kifupi TCU ilizuia Graduation, fikiria waliokuwa na ruhusa kazini na walitakiwa wawe wamepeleka vyeti vya kuhitimu kwa waajiri. Unafikiri wanaelewekaje/?
 
May 5, 2018
7
20
ha!ha!ha!ha!ha pia location ya chuo haikuangalia Wateja!kwa jiografia ya Mbeya chuo kinachoweza kukaa uyole ni kile kilichojengwa na serikali tu!sio private.
Nafikiri Location is not a problem,it has a god geographical location ever seen, tena ndio ingepata wateja wengi sana. Tatizo uongozi ulifanya Extravagance then Kanisa likawaacha tu,TRA walifunga majengo ya Utawala tangu mwaka jana mwezi December mwanzoni na sijui kama walilipa hiyo kodi ya sh karibu milioni 130.
Kikubwa hapo ni baada ya kushindwa kuwalipa walimu,kwa miezi kati ya 15 kwa 9 ,ndipo walimu wakaacha kazi. Wakachukuwa wahuni wakawafanyisha wanafunzi Mtihani pasipo kuwa na Course work,,Yaani wakapika Course work na mbaya zaidi wakawafanyia wanafunzi Table Assessment wakati wa Field(Ubaya kwa first year) anahitaji really Assessment toka kwa mwalimu akiwa darasani./
Ndio maana tunaitaka TCU Iamke ikakamilishe kazi yake pale.
Mbona Makumira Makao Makuu hawana Usanii
 
May 5, 2018
7
20
Nshawahi kuona vyuo vya hovyo hapa nchini ila hiki namba moja "unyakyusa" umeua chuo
Kama vile upo pale,yaani wameweka Unyakyusa Mbele badala ya Academic.
Mwanzoni Chuo kilikuwa kisimamiwe na Tumaini Makumira Makao Makuu ikiwa ni pamoja na Control of Human Resources as per Income of the College. Wanyakyusa wakakataa kwa kigezo cha watu wa kaskazini watatutawala.
From the beginning Mch.Dr. Mwankenja alianza kukiua chuo kwa kuwaondoa wanafunzi 800 wa Certificate in Primary Education (Grade III A na Diploma 300 kwa Kigezo kwamba sasa Chuo ni Chuo Kikuu,Badala ya kubaki na Capital ya hao wanafunzi. Anagalia,kulikuwa na Transition period ya Chuo cha Ualimu cha UYOLE kwenda SHUCO ,Hapo walikwama,walipata wanafunzi 30 wa Degree, utawalipa vipi walimu ? Hapo ndipo Shida ilipoanzia
 
May 5, 2018
7
20
Najiuliza sana hivi vyuo vya makumira mbona vina usani usanii mwingi,mnaharibu sifa ya vyuo vingine ambavyo viko under makumira, mbeya campus kuna shida kubwa kweli,naimani mleta mada ,uongelee yote,kuhusu mitihani ilikuaje??mpaka kufikia wachungaji kutishia kuuana kwenye vikao vya senate.....
Hapo umegonga Msumari wa 18".
Issue ni Mkopo wa Bank uliochukuliwa wa Bilioni 1.2 kutoka CBA BANK na wakaishia kutumia Milioni 600 kujenga Jengo ambalo halijaisha,Yaani ukifanya hata Evaluation ya sh 600 Milioni,haifanani na kazi iliyofanyika.
Milioni 600 zingine zilitafunwa bila kujali zilikopwa kwa kazi gani. Kwa kifupi walitafuna milioni 350 maana milioni 150 walilipana kwa vikao na kumlipa Consultant .
Hiyo ndio SHUCO/TUMAINI UNIVERSITY MAKUMIRA,MBEYA CENTRE
 
Threesixteen Himself

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
8,165
2,000
Niliwahi tembelea hicho chuo mwezi feb 2018. Kwa kweli hali ni mbaya wanafunzi hawasomi na kuna baadhi wanishi hostel za nje yaani wanachofanya humo hostel hawa wanafunzi wa kike ni balaa. Wanahitaji maombi kama siyo serikali kuingilia kati

!
!
Wanafanyaje Mkuu Nijipange Niende
 
May 5, 2018
7
20
Niliwahi tembelea hicho chuo mwezi feb 2018. Kwa kweli hali ni mbaya wanafunzi hawasomi na kuna baadhi wanishi hostel za nje yaani wanachofanya humo hostel hawa wanafunzi wa kike ni balaa. Wanahitaji maombi kama siyo serikali kuingilia kati
Ulipotembelea pale ndio kulikuwa na sekeseke la Walimu 7 kuacha kazi kwa mkupuo, nikiwakumbuka wachache( Mwl Peter Chaula,History) sasa yupo SAUT MBEYA, SAMSON KYANDO ,Sasa yupo SAUT MBEYA,(Geography), Zimkulile Very Well Mkondya)English sasa yupo TEKU, na wengine wengi. Hapo wengine waliondoka October 2016.
Shida ya wanafunzi kutofundishwa ilianzia hapo
 
May 5, 2018
7
20
Acha basi na wewe hivyo,yaani chuo kifungwe kisa una tofauti na uongozi uliopo madarakani,kikifungwa hao wafanyakazi wanaofanya kazi hapo kuanzia wafanya usafi mpaka uongozi wa juu wakale wapi?,kwa nini isiseme TCU iyafanyie kazi mapungufu yaliyopo ?
Tatizo moja tu,
You seems to have a narrow Idea about the Institution. What is better, wakae wazalishe wataalam feki na kufaidisha walioajiriwa au waondoke wakapikwe kwingine ili waje walifae Taifa?
Hata sisi tusingependa kuona watu wanaachishwa kazi ila sidhani kama kuna mtu anafurahia kuwa pale. Watu wanadai mishahara ya miezi 24,bado ni kazi? Wnafunzi hawafundishwi kutokana na kukosekana kwa ufundishaji,je huo nao uachwe?
Lets be serious kwa vitu vyenye kuhusisha Elimu.
 
theriogenology

JF-Expert Member
Oct 7, 2016
8,798
2,000
Niliwahi tembelea hicho chuo mwezi feb 2018. Kwa kweli hali ni mbaya wanafunzi hawasomi na kuna baadhi wanishi hostel za nje yaani wanachofanya humo hostel hawa wanafunzi wa kike ni balaa. Wanahitaji maombi kama siyo serikali kuingilia kati
Funguka mkuu wanafanya nini hao wanafunzi...

Au wamegeuza hostel kuwa madanguro....
 
Oct 12, 2015
36
95
[QUOTE="SAMWEL MBALASWA, aibu sana hii,alafu wanajiita wachungaji ,kumbe wachumia matumbo,GSF inatakiwa ifanyiwe formation, kuna maeneo sijui yanawatia DOA...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom