TCU: Darasa la saba sasa kujiunga na chuo kikuu moja kwa moja

TCU: Darasa la saba sasa kujiunga na chuo kikuu moja kwa moja

Jospina

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2013
Posts
2,421
Reaction score
1,395
Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU), imepanga kuanza kuwadahili wanafunzi wa kujiunga na masomo ya vyuo vikuu kwa kutumia uzoefu wao.

Udahili huo utakaoanza mwaka huu wa masomo 2013/14, utakuwa ukiwahusisha wale ambao elimu yao imeishia darasa la saba na kuendelea, lakini walikosa sifa ya kuendelea na masomo kwa ngazi ya chuo kikuu.

Kupitia utaratibu huo mpya, mtahiniwa atajiunga na Chuo Kikuu kulingana na fani atakayoiomba na atatakiwa kufanya mitihani mitatu na kufaulu kwa wastani wa daraja B.

Mkurugenzi wa Ithibati na Ubora wa Elimu ya Juu kutoka TCU, Dk Savinus Maronga aliliambia gazeti hili kuwa baada ya kuona kuna watu wengi wanaopenda kuendelea na masomo ya elimu ya juu, lakini wameshindwa kutokana na kutokuwa na vigezo, TCU imeamua kuanzisha mitihani hiyo maalumu.

Alisema kuwa mfumo huo unaojulikana kama ‘Recognition of Prior Learning' (RPL), utamwezesha mwombaji kudahiliwa vyuoni kupitia tume hiyo kama wanavyofanya watahiniwa wengine.

Sifa zinazotakiwa
Kuhusu sifa za kujiunga, Dk Maronga alisema kuwa mwombaji anatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 25 na kuendelea, sambamba na kuwa na elimu isiyopungua darasa la saba.

"Mwombaji anatakiwa kuwa na nia ya kujiunga na elimu ya chuo kikuu na uzoefu wa kile ambacho anakusudia kukisoma.

Awe na uwezo wa kuandika na kusoma Lugha ya Kiingereza, ambayo ndiyo inayotumika kufundishia vyuoni,"alisema Dk Maronga na kuongeza:

"Kuna watu wameishia darasa la saba, lakini wamefanya kazi katika eneo moja, mfano karani wa mahakama, mwandishi wa habari kwa muda mrefu. Hivyo mfumo huu utawawezesha kuendelea na masomo bila tatizo."

Vigezo
Mkurugenzi huyo alisema, kutakuwa na mitihani ya masomo matatu, ambayo mtahiniwa ili apate nafasi ya kuendelea na masomo ni lazima afaulu kwa wastani wa daraja B.

Alisema daraja la kwanza linaloanza na alama A ni 75-100, daraja B+ ni 60-75, B ni 50-59, C ni 40-49, D ni 35-39 na daraja E ni 0-34.

"Katika mitihani mitatu atakayoifanya, atatakiwa kupata wastani wa daraja ‘B' na somo husika la fani yake atatakiwa kupata alama B ili kuwa na vigezo vya kupata cheti kitakachomwezesha kuendelea na masomo yake,"alisema Dk Maronga.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi
 
mbona safi tu,kwanza waliomaliza fm 6 na kujiunga na vyuo ndiyo wanaoongoza kwa kuharibu mifumo ya nchi! bora tuajaribu hawa waliobaki inawezekana ni wazalendo!
 
Form four anatakiwa aanzie certificate level then darasa la saba aanze shahada ya kwanza moja kwa moja itakuwa ni maajabu ya dunia!
 
Aisee kutakuwa na shahada kibao! Kama Nigeria! Ngoja madiwani, waigizaji, wasanii, wapenda sifa n.k wapate hizi habari. Yaani katika hivyo vyuo kutakuwa na kurupushani kama mtaa wa Kongo pale sokoni Kariakoo; kila mtu akigombania shahada yake.
Sijajua kama hizo shahada zitatambulika hata hapo Kenya. Naona kama zitakuwa 'home schooling'. Wale mlio na ufahamu juu ya mifumo mbalimbali ya Elimu tunaomba ufafanuzi wenu katika hili.
 
Aisee kutakuwa na shahada kibao! Kama Nigeria! Ngoja madiwani, wapenda sifa n.k wapate hizi habari. Yaani katika hivyo vyuo kutakuwa na kurupushani kama mtaa wa Kongo pale sokoni Kariakoo; kila mtu akigombania shahada yake.

hahaaa umenifurahisha eti madiwani??
 
Iko poa lkn kwa sbb inaonekana imelenga watu wazima ningeshauri hata o level iunganishwe hapo.
 
Ndugu Revocatus Kashaga tafadhali rejea jamvini hapa utufafanulie zaidi hiyo "programme" mpya ya TCU, title na habari yako kwa ujumla havijitoshelezi. Wahitimu hao wa darasa la saba watajiunga na vyuo hivyo katika ngazi gani ya masomo? Maana Vyuo vikuu mbali na shahada pia hutoa mafunzo ya cheti na stashahada. Tafadhali tufafanulie hiyo "programme" ambayo mwenzetu umebahatika kuisikia/kuiona.
 
Last edited by a moderator:
Kama ni hivyo, je kwa nini mfumo wa mature entry examination uliondolewa? Je watapewa ule mtihani wa majaribio (matriculation examination)? Aisee meku, je hao waajiri si watalazika kuwalipia, takribani, wafanyakazi wote mishahara ya ngazi ya shahada? (ikiwama kama wengi watasoma). Maswali ni mengi kwa kichwa. Baada ya sekondari za Kata, Tanzania yaja na shahada za 'Kijiji'. Yaani kila sebule ya mwenye uwezo wa 'kununua' shahada itakuwa na shahada na picha ya joho ukutani.
 
Kama ni hivyo, je kwa nini mfumo wa mature entry examination uliondolewa? Je watapewa ule mtihani wa majaribio (matriculation examination)? Aisee meku, je hao waajiri si watalazika kuwalipia, takribani, wafanyakazi wote mishahara ya ngazi ya shahada? (ikiwama kama wengi watasoma). Maswali ni mengi kwa kichwa. Baada ya sekondari za Kata, Tanzania yaja na shahada za 'Kijiji'. Yaani kila sebule ya mwenye uwezo wa 'kununua' shahada itakuwa na shahada na picha ya joho ukutani
inaonekana una uroho sana! Hupendi kusikia habar njema kuhusu jirani yako? Kama hao wenye dhamana ya kutoa shahada na vingnevyo wangekuwa kama wewe, sidhani kama kungekuwepo watu walioelimika!
 
Sijui is unajua Tanzania ya maajabu inawezekani

Sent from my BlackBerry 9790 using JamiiForums
 
hii ni mpya, lakini lipo suala linalofanana na hili ambapo watu hutunukiwa shahada kwa juhudi zao na mafanikio waliyopata katika maisha. Mfano kwa wenzetu Wachaga, wapo ambao elimu yao ni darasa la saba lakini wameweza kuanzisha biashara na zimekua na kuwa kampuni kubwa tu, mtu kama huyu ameonesha uwezo, juhudi na maarifa katika usimamizi na uendeshaji wa biashara yake, watu kama hawa hupewa digrii za heshima siyo phD la hasha ni digrii ya awali katika tasnia aliyofanikiwa na hutunukiwa tu na siyo kukaa darasani na kuanza kuhudhuria mihadhara.
 
Back
Top Bottom