TCU: Darasa la saba sasa kujiunga na chuo kikuu moja kwa moja

TCU: Darasa la saba sasa kujiunga na chuo kikuu moja kwa moja

Maajabu jamani haya,hopo kunamtu anatafuta nafas sio hivhv.haiwezekan
 
CCM hawaishiwi maajabu. Sasa huu ni mpango wa kuhakikisha wajumbe wao wa nyumba kumi wanapata sifa za kuwa mawaziri na wakuu wa mikoa kwa katiba mpya.....tehe tehe tehe!

Kwa hiyo aliyefika form 4 aanzie certificate, halafu wa darasa la 7 bachelor. Which means, hii dhahma ya matokeo ya kidato cha 4 kwa mwaka 2012 haina shida, ni kusubiri tu miaka igote 25 then unajitoma chuoni kuchukua Bachelor of Arts in Mining Contracts Designing
 
Elimu ya Darasa la Saba la Tanzania ya sasa (Elimu Msingi) ni duni mno tofauti na miaka ya 1961-1975 hivyo ni kioja kujiunga kusomea chuo kikuu,ikumbukwe kuwa wapo form six leavers wana disco halafu kuna form one wasioweza zile stadi tatu za KKK.
 
Kadi za CCM zinarudishwa ktk mikutano ya CUF au CDM au ...., za CDM zinarudishwa ktk mikutano ya CCM au CUF au..... na kadhalika. Digree yangu niirudishe wapi?
 
safi sana..sasa na sisi tutaanza kuringa na ka digirii ka uzeeni
 
Hakuna kitu kama hicho wewe umesikia wapi?Mbona vyombo vya habari havijatangaza?wanaJF tuwe wakweli ili tupashane habari za uhakika sio kutunga kutoka kichwani then mnaleta hapa sio vizuri.
 
Safi sana hausigeli wangu atapata elimu ya juu km yule mkuu wa mkoa ambaye alikuwa hgl then akadoma hd PhD
 
Tume ya vyuo vikuu nchini Tanzania ( TCU) imeanza mchakato kwa watu wenye elimu ya darasa la saba kuweza kupata elimu ya shahada ya kwanza katika kozi mbalimbali hapa nchini. Ofisa Uhusiano wa TCU bwana Edward Mkaku amesema vyuo vitakavyotumika ni chuo cha Tumanini cha Dar es Salaam, UDSM na chuo kikuu cha Mzumbe! vigezo mwombaji lazima awe na umri wa miaka 25 na kuendelea, barua ya mwajiri, awe ana uwezo wa kuongea na kuandika kiingereza kwa ufasaha na utayari wa kusoma elimu ya juu.Alimalizia kwa kusema wameanzisha program hii kubaini vipaji vya watu walioshia darasa la saba.

Mtazamo wangu mie tofauti-naona wanalofanya TCU ni kama mimba kutunga kupitia mdomoni! Kuna mapungufu gani katika system iliyopo? Hizi degree sasa wanazifanya kama zile za waganga wa jadi )Dkt, Prof)?
 
Form four anatakiwa aanzie certificate level then darasa la saba aanze shahada ya kwanza moja kwa moja itakuwa ni maajabu ya dunia!!!!!!!!!!!!!!!!

usishange ndugu yangu serikali imejipanga kikamilifu kuboresha secta ya Elimu,kama mwanafunzi asiyejua kusoma wala kuandika japo jina lake anajuinga na elimu ya Sekondari tutashindwaje kumpeleka yule anayejua kiingereza chuo kikuu? Viongozi wako makini sana
 
Sina uelewa mpana wa mifumo ya elimu duniani, lakini kuna ka-harufu ka hatari kananukia nchi yetu. Yaani darasa la saba hili la Tanzania ya leo ambapo mtoto anashindwa kupata alama za kujiunga na shule za kata, then akasome chuo kikuu kwa mitihani ya masomo matatu?

Sasa practically, huyu darasa la saba wa miaka hii 25 atapata udhoefu wa kutoka wapi, na fani ipi/ Kwa sababu nijuavyo mie, Serikali na waajiri wengi wanachukua kuanzia form 4, hawa Darasa la 7 wengi ni ma-house boy na house girl ambao hata hivyo wengi nao hawawataki siku hizi. TCU mnataka kutupeleka wapi, hebbu tunaomba wekeni hadharani utafiti mlioufanya ili tuone ikiwa kweli mko sahihi, lakini kama mnafanya kazi kwa ki-memo; kwa kweli Taifa laelekea kubaya sana.

Nadhani ingefaa kuimarisha mfumo wa QT na VETA na kuifanya iwe lazima kwa anayeshindwa kuendelea na Kidato cha kwanza, badala ya hii mnayotaka kufanya, ni msiba huu. Kama watoto wadogo wa drs la saba na kidato cha 4 wanaiba mitihani, mnadhani hawa watu wazima wenye hela zao waliokimbia shule na sasa kutaka kuwa na veti vya chuo kikuu watashindwa kuiba mitihani?

Lakini pia Kwani utalaam na kulitumikia Taifa mpaka uwe na cheti cha elimu ya chuo kikuu pekee. Mbona tunao wasio na na vyeti vya chuo kikuu lakini wako vema kwa utambulisho wao huo wa Darasa la saba n.k. Whats motives behind this move? Jibu la watanzania kimya
 
Back
Top Bottom