Watu wengi kwa sasa hutunza pesa zao kwenye M-PESA, TIGO-PESA na kadhalika na kuifanya kama ndio benki (ingawa hakuna interest). Ni vema kwa kuwa unapotaka malipo ya haraka haraka au kumtumia mtu haraka ni bora sana. Sidhani kama tunafahamu juu ya risk zake:
Ushauri:
- Umeweka laki tano, ukachukua mzinga (Mola aepushilie mbali) na hukusema kwa mtu kuwa una laki tano kwenye M-pesa au Tigo Pesa, vibaka wakalamba ile simu wakanyofoa simcard wakaitupa wakabaki na simu, hivi ina maana kuwa hiyo pesa ndio imetoka hivo sio?
- TIGO au VODACOM kuna siku watakaa waseme mteja mmoja aliwekeza kwetu laki tano miaka miwili imepita na simu haipo hewani hivyo tutafute ndugu zake?
Ushauri:
- Weka pesa tu pale unapohitaji au uweke kiasi kidogo tu cha dharura au kwa ajili ya malipo ya bili au kununua vocha.
- Umtaarifu ndugu wa karibu kuwa simu yangu ina pesa kiasi fulani lolote likitokea kwangu fatilia urithi.
- Makampuni ya simu yaandae taratibu za urithi wa pesa za mtandao huu endapo baya limetokea