Tcra na umiliki wa minara ya mawasiliano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tcra na umiliki wa minara ya mawasiliano

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Mar 15, 2011.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Mar 15, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kwa sasa hivi katika jiji la dar es salaam huwezi kupita kilomita 2 bila kukuta mnara wa mawasiliano labda juu ya nyumba za watu haswa magorofa kati kati ya jiji na pembeni kidogo au barabari kwenye viwanja vya watu walioamua kukodishia kampuni za mawasiliano haswa mawasiliano ya simu kwa ajili ya kufanyia shuguli zao .

  Kuna wakati mwingine unaweza kushangaa sana pale tunapoambiwa ghorofa lazima liwe refu ili minara iwe juu kusiwe na muingiliano wa watu au vifaa vingine lakini hili ni tofauti na jijini dar es salaam kuna minara mingi iko kwenye magorofa ya chini yaani ukikaa kwenye ghorofa refu unaona ule mnara wa mawasiliano sijui kiafya suala hili likoje na usalama .
  Ninapoona hali kama hiyo na ninavyofikiria kuhusu Mipango ya TCRA na Matangazo ya DIGITALI kwa Televisheni ifikapo mwaka 2015 , wakati mwingine nashangaa mbona miundombinu ya kizamani ya mawasiliano bado inashamiri nani anatoa leseni za kuendelea kujenga miundo mbinu hii ?

  Kama mnavyokumbuka miaka michache iliyopita kuliwahi kuwa na mjadala kitaifa kuhusu madhara ya minara ya mawasiliano kwa afya za wanadamu na mazingira kwa ujumla , kwenye mjadala huo kukatokea mawazo kwamba kampuni za mawasiliano zishirikiane katika minara kwenye kutoa huduma za mawasiliano .

  Kilichonifanya niandike suala hili pengine sina taarifa za kutosha ni baada ya kukutana na mfanyakazi wa kampuni ya SASATEL katika maongezi nilimuuliza mpango wao wa kusambaa mikoani ukoje ,akaniambia kuanzia mwaka huu katikati wataanza kujenga minara ya mawasiliano kwa ajili ya kusambaza huduma zao kwahiyo inaonekana mpaka sasa jawabu la kushirikiana minara kwa kampuni za mawasiliano hakuna .

  Mimi nadhani ni wakati sasa kwa tume ya mawasiliano tanzania TCRA kuwa na mamlaka na minara yote ya mawasiliano na yenyewe ndio iwe inakodisha kwa kampuni za simu kwa kuwapa vieneo vya kuweka vifaa vyao kwenye minara hiyo yaani kukodisha .

  Ikifanya hivi itachochea ukuaji wa sekta hii kwa sababu hata kampuni nyingine ikitaka kuwekeza haitojali kuwa na mfuko mkubwa kwa ajili ya ujengaji wa minara na miundo mbinu mengine , pia itapunguza uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na ufungaji wa minara kila sehemu na aina nyingine za mionzi na katika suala la ulinzi na usalama hapana shaka tutakuwa tumehakikishiwa usalama wetu kama minara ikiwa chini ya TCRA bila kusahau ushirikiano kwa wadau wa mawasiliano haswa kampuni .

  Tunataka mamlaka ya mawasiliano iwe na mamlaka ya juu kuhusu mawasiliano na uwekezaji nchini , tukumbuke wawekezaji hawa wanakuja na kuondoka mazingira yetu wameharibu na wakati mwingine hata kufanya hujuma , ulipaji wa kodi wanaujuwa wenyewe , utoaji wa hisa kwa watanzania wanaujua wenyewe na mambo mengine mengi - TCRA FUNGUA MENO YAKO ANZA KUNGATA .

  Yona F Maro

  0786 806028
   
Loading...