TCRA na NIDA: Kwanini "fingerprint scanner" zilizopo nyuma ya "smartphones" zetu hazitumiki katika zoezi linaloendelea la kusajili upya simcards?


NINAOMBA UFAFANUZI WA KINA KUTOKA KWA WATAALAM WA ICT PAMOJA NA TELECOMMUNICATION ENGINEERS.

Shikamooni wakubwa zangu wote wa humu jamiiforums. Mimi mdogo wenu Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty. Leo swali langu lipo kama ifuatavyo?

Kwanini "fingerprint scanners/censors" zilizopo nyuma ya "smartphones" zetu hazitumiki katika zoezi linaloendelea la kusajili upya wa simcards?

Kwanini mtu afunge safari kutoka point A kwenda point B kisha akawasilisha number ya NIDA pekee kisha alama ya kidole chake ikawa matched na ile alama ya kwenye computers servers za NIDA kisha akaambiwa kuwa umekamilisha zoezi?

Kwanini hakuna uwezekana wa kuwa na Android App ambayo itakuwa linked ikawa ina communicate na severs za NIDA, Service Provider husika pamoja na Fingerprint sensor ya kwenye smartphone kisha mtu akajifanyia usajili yeye mwenyewe akiwa sehemu yenye network coverage nzuri?

Au Kwanini "fingerprint censors" zilizopo nyuma ya hizi "smartphones" zetu haziwezeshwi kutumika katika kutengeneza accounts pamoja na ku-login katika mitandao ya kijamii (Twitter, Facebook, Jamiiforums) ili sasa tuachane na masuala ya mtu kusahau passwords pamoja na emails?

Unaweza ukakuta mtu anamiliki accounts kadhaa katika mitandao tofauti ya kijamii pamoja na emails pia, ila kila account ina password yake hivyo inakuwa ni rahisi sana kwa mtu kuweza kusahau moja kati ya credentials hizo.

VODACOM WAME-COPY "CONSTRUCTIVE IDEA" YANGU. NILIPENI JAMANI.
Mkuu Dp800 ameongelea ishu ya manufacturer kuweka hizi built in scanner exclusively kwa ajili ya security ya simu tu na haiwezi kushare na external apps.
Ila kiuhalisia pia inawezekana maana kuna simu zinaitwa FAMOCO hizi zimetengenezwa special kwa ajili ya usajili kwa njia ya biometric.
 
Daudi Mchambuzi,

hapana haina connections na NIDA! but nafikiri aliyetoa maada somehow yuko very logic! labda nimsaidie kumjibia!

hawa watu wanaosajili kwa alama za vidole, wanatumia simu hizi hizi android! lakini wao wana kitu kimoja cha ziada! wao wana ile external scanner ambayo wanaconnect kwa simu! Lakini pia wao huwa wanapewa software flan na service provider ambayo inko linked and NIDA, kiasi kwamba ili uweze access information toka NIDA inakulazimu "UAPLOAD" finger print yako!

sasa hoja ya mtoa maada ni kuwa, kwanini hawa service provider wasidevelop APP ambayo nikiidownload kwa simu yangu iwe linked either na wao before kuwa linked na NIDA ambayo itanilazimu niupload FINGER PRINT yangu kwa kutumia simu hizi zenye finger print.

Nafikiri hii ni nzuri na ingesaidia kupunguza usumbufu huu wa sasa!

Infantry Soldier
Wewe umejibu murua kabisa.
 
Ile fingerprint iko kwenye simu na kama unavojua simu unaweza poteza au haribika lakin simcard iko tofauti hata ikiharbika unaweza renew na matumizi yakaendelea.
Ndio maana ameongelea kuwa na network nzuri akimaanisha hizo alama za vidole na taarifa zake kiujumla zitatumwa kwenye database za Nida au whoever responsible.
 
hivi mnajua hili zoezi lilkuwa rahisi sana kabla yule mpuuzi mmoja akwapue bil 17 za fingerprint??

maana maudhui yake ni tofauti ila lengo lilikuwa ni moja.
 
Ndio maana ameongelea kuwa na network nzuri akimaanisha hizo alama za vidole na taarifa zake kiujumla zitatumwa kwenye database za Nida au whoever responsible.
Jamaa alikuwa anafikiri labda data zinatunzwa kwenye simu kisha baadae zinafanyiwa synchronization na servers
 
Fingerprint scanner kwenye Sim zetu huwezi kuzitumia sababu memory inayotumika haiwezi kufikiwa na developer hiyo imewekwa kwa ajili ya security ya sim.

Labda tusubiri hardware manufactiure watakapoona ni sawa kuruhusu hiyo feature kutumika kwa matumizi mengine.
Asante kwa kuchangia
 
Back
Top Bottom