white wizard
JF-Expert Member
- May 18, 2011
- 8,618
- 13,880
kulingana na sheria ambayo inawalazimisha hawa wenye makampuni yanayotoa huduma ya ving'amuzi hususani(TING)ni kwamba utakapolipia yale malipo ya mwezi ambayo ni elfu kumi,utaona local chaneli zote zilizo kwenye package yao(tbc1,itv,chanel ten,star tv, Atn,na clouds tv)na nyingine za nje.Sasa cha ajabu ukiacha kulipa hayo malipo ya mwezi,sheria inasema wao watakuwa na haki ya kusitisha we kuona zile chanel za kulipia kama sentanta afrika,cnn,muv tv nk.sasa wao wanakata hata Atn na clouds tv!hazo huwezi kuona hadi ulipie!achilia mbali aljazeera,press tv japo nazo ni ft(flee 2 air)nazo wanazifunga!na juzi kwenye kipindi cha malumbano ya hoja itv,walisisitiza kuwa chaneli zote ambazo ni FT,ziwe zinapatikana muda wote,wao watakukatia zile ambazo ni za kulipia 2,sasa toka lini Atn,na clouds tv zimekuwa za kulipia,wakati kwa wakazi wa dar wanazipata kwa kutumia antena za kadawa?na majuzi niliwapigia simu hawa tcra,kulalamikia hili suala,cha ajabu nao wanashangaa kama ni kweli wanafanya hivyo!mi ndio huduma nayoitumia,baadaye wakasema ngoja walifuatilie kama ni kweli eti nao hawa jui!Huu mfumo wameudandia 2 bila maandalizi ya kutosha,na nyie ngojeni ifike hiyo dec 31,patakuwa hapatoshi,itakuwa mvulugano tu.hata haya makampuni bado hawajajiandaa,mf. Hawa TING,unalipia cku 30,lakini unaweza kuona ikiwa imetulia labda siku 15!cku nyingine zote signal weak,na hapa ni maeneo ya dar!wito wangu kwa ambaye hajajiingiza huko bora asubiri ili ushindani wa haya makampuni uongezeke,na huduma wataboresha,ili mtu uwe na chaguo zuri.