TCRA: Kasi ya internet inasababisha kifurushi kuisha haraka

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,014
9,883
1645608296278.png

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetaja vitu vitatu vinavyosababisha kuisha kwa bando haraka ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa kasi ya internet, uwezo wa simu janja na kuwa na application nyingi kwenye simu.

Pia imesema gharama za kupiga simu kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine nchini ni nafuu ukilinganisha na nchi nyingine duniani.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Jabiri Bakari ameyasema hayo jana Jumanne Februari 22 wakati wa mkutano wake na Jukwaa la Wahariri nchini (TEF).

“Tafiti mbalimbali duniani zinaonyesha kuwa, gharama za kupiga simu kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine nchini Tanzania, zipo chini tofauti na nchi nyingine duniani, gharama za kawaida bila kujiunga na kifurushi, pamoja na gharama zilizounganishwa na kifurushi nazo zimeshuka,” amesema.

Amesema Tanzania inaongoza kwa kuwa na vifurushi rahisi na salama Afrika na duniani, hivyo kila mtoa huduma anauwezo wa kubadilisha vifurushi kila baada ya siku 90.

Mkurugenzi huyo amesema kabla vifurushi havijabadilishwa, mtoa huduma kuleta mapendekezo yake TCRA kwa ajili ya kuangalia kama inaendana na utafiti uliofanya ili kutomuumiza mlaji au mtumiaji wa huduma za mawasiliano nchini.

Amesema watumiaji wa simu janja nchini ni asilimia 27 ambao wanaonekana kutumia muda mdogo kusoma habari ndefu, hivyo wengi wanaotumia simu hizo hupoteza data bila kujua.

Naye Mkurugenzi Masuala ya Sekta TCRA, Dk Emmanue Manasseh akizungumzia kifurushi katika simu amesema kumekuwa kukisemwa kuwa vifurushi hivyo vinaisha kwa haraka lakini Mamlaka hiyo imekuwa ikifanya majaribio mbalimbali ili kuhakikisha watoa huduma wanatoa huduma sawa na walichowaahidi watumiaji.

Ametaja vitu vinavyosababisha kumaliza kifurushi kwa haraka kuwa ni kuongezeka kwa kasi ya mtandao kwenye simu janja mfano kutoka 3G hadi 4G.

Pia, ubora wa video na picha unavyoongezeka maana yake matumizi nayo yanaongezeka.

"Tuna “application” mbalimbali kwenye WhatsApp zinaboreshwa mara kwa mara nazo zinatumia data. Watumiaji wengi wa simu kuna vitu vinaendelea kwenye simu yake lakini mtumiaji hajui. Uwepo wa application nyingi, nyingine hazitumii hivyo zinamaliza bundle,” amesema.

Amesema TCRA imeelekeza watoa huduma kutengeneza ‘application’ ambazo watumiaji wanaweza kufuatilia matumizi yao.

MWANANCHI
 
Hongera Tanzania kwa kuwa nchi ya kwanza Afrika nzima kufanya modern installation ya 5G! Ndiyo maana kumbe UVIKO-19 ilitusumbua sana last year!

Naomba msiishie hapo. Twende tusonge mbele hadi 100G huko!
 
Wako sahihi. GB moja uganda ilikuwa ikiuzwa ugsh 5000 na inadumu kwa wiki hapo nimwaka 2019 kwenye mtandao wa MTN. Hapo ukiileta tanzania kwa wakati huo nisawa na tsh 3400.

Wakati aliyekuwa na gharama za juu za bando tanzania alikuwa ni vodacom na alikuwa akiuza mb 2048 kwa tsh 3000 kwa wiki sawa na gb2 kwa mahesabu hayo gharama za internet zilikuwa zaidi ya asilimia 210 kwa tanzania
 
Mimi ni mtumiaji mkubwa sana wa Internet, nimewahi kupitia kila aina ya changamoto za internet hapa Tanzania. Hayo maelezo nayaunga mkono asilimia 100. Na tujiandae ikija 5G watu watalia zaidi. Kitu msichokijua ni kwamba 4G ya Tanxania ni xaidi ya 4G ya nchi nyingi barani Africa. Tuna 4G+

Iundwe tu hiyo app kuwasaidia wasioweza kudhibiti data.
 
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetaja vitu vitatu vinavyosababisha kuisha kwa bando haraka ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa kasi ya internet, uwezo wa simu janja na kuwa na application nyingi kwenye simu.

Pia imesema gharama za kupiga simu kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine nchini ni nafuu ukilinganisha na nchi nyingine duniani.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Jabiri Bakari ameyasema hayo jana Jumanne Februari 22 wakati wa mkutano wake na Jukwaa la Wahariri nchini (TEF).

“Tafiti mbalimbali duniani zinaonyesha kuwa, gharama za kupiga simu kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine nchini Tanzania, zipo chini tofauti na nchi nyingine duniani, gharama za kawaida bila kujiunga na kifurushi, pamoja na gharama zilizounganishwa na kifurushi nazo zimeshuka,” amesema.

Amesema Tanzania inaongoza kwa kuwa na vifurushi rahisi na salama Afrika na duniani, hivyo kila mtoa huduma anauwezo wa kubadilisha vifurushi kila baada ya siku 90.

Mkurugenzi huyo amesema kabla vifurushi havijabadilishwa, mtoa huduma kuleta mapendekezo yake TCRA kwa ajili ya kuangalia kama inaendana na utafiti uliofanya ili kutomuumiza mlaji au mtumiaji wa huduma za mawasiliano nchini.

Amesema watumiaji wa simu janja nchini ni asilimia 27 ambao wanaonekana kutumia muda mdogo kusoma habari ndefu, hivyo wengi wanaotumia simu hizo hupoteza data bila kujua.

Naye Mkurugenzi Masuala ya Sekta TCRA, Dk Emmanue Manasseh akizungumzia kifurushi katika simu amesema kumekuwa kukisemwa kuwa vifurushi hivyo vinaisha kwa haraka lakini Mamlaka hiyo imekuwa ikifanya majaribio mbalimbali ili kuhakikisha watoa huduma wanatoa huduma sawa na walichowaahidi watumiaji.

Ametaja vitu vinavyosababisha kumaliza kifurushi kwa haraka kuwa ni kuongezeka kwa kasi ya mtandao kwenye simu janja mfano kutoka 3G hadi 4G.

Pia, ubora wa video na picha unavyoongezeka maana yake matumizi nayo yanaongezeka.

"Tuna “application” mbalimbali kwenye WhatsApp zinaboreshwa mara kwa mara nazo zinatumia data. Watumiaji wengi wa simu kuna vitu vinaendelea kwenye simu yake lakini mtumiaji hajui. Uwepo wa application nyingi, nyingine hazitumii hivyo zinamaliza bundle,” amesema.

Amesema TCRA imeelekeza watoa huduma kutengeneza ‘application’ ambazo watumiaji wanaweza kufuatilia matumizi yao.

MWANANCHI
Mimi ni mhitimu wa CCNA, naelewa vizuri haya mambo ya mawasilano ya mtandao yanavyofanyika hasa kwenye upande wa data, ukihusianisha na kasi ya mtandao wenyewe. Hapa sijaelewa kitu, unless kama taarifa hii ilitolewa na mtu ambaye ni mtawala na si mtaalamu.

Ukiniambia kuwa kasi inapokuwa kubwa halafu ikatokea kwa bahati mbaya mtumiaji akawa ameaacha application nyingi ambazo zina-RUN kwenye AUTO UPDATE MODE, hapo kidogo naweza kuelewa. Still, hata aliye na application za aina hii, bado hawezi kuwa anamaliza bando haraka kila wakati anapokuwa amenunua bando kwa sababu SI KILA ANAPOKUWA AMENUNUNA BANDO, APPLICATION HIZI ZITAKUWA ZINA -RUN AUTO-UPDATE kwa sababu AUTO-UPDATE huwa inakuwepo tu pale ambapo kunea NEW UPDATES. NEW UPDATES huwa hazipo kila siku, zinaweza kuwepo mara moja kwa wiki au kwa mwezi kutegemea na aina ya aplication. Still, haipo applicationa ambayo INA UPDATES ZA KILA SIKU, na kama zipo ni chache sana na watu walio wengi watakuwa hawazitumii

Fikiria kwa mfano, smartphone yangu inanionyesha LAST DATA USAGE ILIKUWA NI 500MB. Baada ya hapo nimenunua tena IGB na baada ya muda napokea ujumbe "umetumia asilimia 75 ya bando yako " na baada ya muda tena naambiwa nimetumia 100% ya bando. Nikienda kuangalia kwenye DATA USAGE inaniambia nina 750MB ambazo nimeshatumia mpaka muda huo, ukiunganisha na zile za awali 500MB; wakati kawaida ilitakiwa iniambie kuwa nimetumia jumla ya 1.5G ambayo ni 500MB zilizokuwa zimetumika kabla sijaweka bando, ukiongezea na 1GB niliyoweka.

Kwa hili swala watu tuko kimya tu kwa sababu mambo ni mengi lakini kinachoendelea kwenye swala hili NI WORST CASE SCENERIO
 
Kufananisha uchumi wa tanzania na izo nchi nyingine ni ujinga. Tuanzie hapa
1. Pato la taifa kwa ujumla
2. Kipato cha mtu mmoja

je hizi sababu ndio zinapandisha gharama au ni kasi ya internet ndio inapandisha gharama!!
 
Tanzania hakuna 4G wala 3G acheni uongo katika ku_download files speed ya mwisho niliyoishudia kwa mitandao yote ni 7MB/sc
 
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetaja vitu vitatu vinavyosababisha kuisha kwa bando haraka ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa kasi ya internet, uwezo wa simu janja na kuwa na application nyingi kwenye simu.

Pia imesema gharama za kupiga simu kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine nchini ni nafuu ukilinganisha na nchi nyingine duniani.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Jabiri Bakari ameyasema hayo jana Jumanne Februari 22 wakati wa mkutano wake na Jukwaa la Wahariri nchini (TEF).

“Tafiti mbalimbali duniani zinaonyesha kuwa, gharama za kupiga simu kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine nchini Tanzania, zipo chini tofauti na nchi nyingine duniani, gharama za kawaida bila kujiunga na kifurushi, pamoja na gharama zilizounganishwa na kifurushi nazo zimeshuka,” amesema.

Amesema Tanzania inaongoza kwa kuwa na vifurushi rahisi na salama Afrika na duniani, hivyo kila mtoa huduma anauwezo wa kubadilisha vifurushi kila baada ya siku 90.

Mkurugenzi huyo amesema kabla vifurushi havijabadilishwa, mtoa huduma kuleta mapendekezo yake TCRA kwa ajili ya kuangalia kama inaendana na utafiti uliofanya ili kutomuumiza mlaji au mtumiaji wa huduma za mawasiliano nchini.

Amesema watumiaji wa simu janja nchini ni asilimia 27 ambao wanaonekana kutumia muda mdogo kusoma habari ndefu, hivyo wengi wanaotumia simu hizo hupoteza data bila kujua.

Naye Mkurugenzi Masuala ya Sekta TCRA, Dk Emmanue Manasseh akizungumzia kifurushi katika simu amesema kumekuwa kukisemwa kuwa vifurushi hivyo vinaisha kwa haraka lakini Mamlaka hiyo imekuwa ikifanya majaribio mbalimbali ili kuhakikisha watoa huduma wanatoa huduma sawa na walichowaahidi watumiaji.

Ametaja vitu vinavyosababisha kumaliza kifurushi kwa haraka kuwa ni kuongezeka kwa kasi ya mtandao kwenye simu janja mfano kutoka 3G hadi 4G.

Pia, ubora wa video na picha unavyoongezeka maana yake matumizi nayo yanaongezeka.

"Tuna “application” mbalimbali kwenye WhatsApp zinaboreshwa mara kwa mara nazo zinatumia data. Watumiaji wengi wa simu kuna vitu vinaendelea kwenye simu yake lakini mtumiaji hajui. Uwepo wa application nyingi, nyingine hazitumii hivyo zinamaliza bundle,” amesema.

Amesema TCRA imeelekeza watoa huduma kutengeneza ‘application’ ambazo watumiaji wanaweza kufuatilia matumizi yao.

MWANANCHI
Kuna Model za simu Africa zimekuja na Vi application vinavyoiba Data za wateja kwa makusudi kujipatia faida- ulaji huu wa data kiolela aupo kwenye highend phones kama Iphone,Samsung na Oppo- kuna ushaidi katika hili
 
Mimi ni mhitimu wa CCNA, naelewa vizuri haya mambo ya mawasilano ya mtandao yanavyofanyika hasa kwenye upande wa data, ukihusianisha na kasi ya mtandao wenyewe. Hapa sijaelewa kitu, unless kama taarifa hii ilitolewa na mtu ambaye ni mtawala na si mtaalamu.

Ukiniambia kuwa kasi inapokuwa kubwa halafu ikatokea kwa bahati mbaya mtumiaji akawa ameaacha application nyingi ambazo zina-RUN kwenye AUTO UPDATE MODE, hapo kidogo naweza kuelewa. Still, hata aliye na application za aina hii, bado hawezi kuwa anamaliza bando haraka kila wakati anapokuwa amenunua bando kwa sababu SI KILA ANAPOKUWA AMENUNUNA BANDO, APPLICATION HIZI ZITAKUWA ZINA -RUN AUTO-UPDATE kwa sababu AUTO-UPDATE huwa inakuwepo tu pale ambapo kunea NEW UPDATES. NEW UPDATES huwa hazipo kila siku, zinaweza kuwepo mara moja kwa wiki au kwa mwezi kutegemea na aina ya aplication. Still, haipo applicationa ambayo INA UPDATES ZA KILA SIKU, na kama zipo ni chache sana na watu walio wengi watakuwa hawazitumii

Fikiria kwa mfano, smartphone yangu inanionyesha LAST DATA USAGE ILIKUWA NI 500MB. Baada ya hapo nimenunua tena IGB na baada ya muda napokea ujumbe "umetumia asilimia 75 ya bando yako " na baada ya muda tena naambiwa nimetumia 100% ya bando. Nikienda kuangalia kwenye DATA USAGE inaniambia nina 750MB ambazo nimeshatumia mpaka muda huo, ukiunganisha na zile za awali 500MB; wakati kawaida ilitakiwa iniambie kuwa nimetumia jumla ya 1.5G ambayo ni 500MB zilizokuwa zimetumika kabla sijaweka bando, ukiongezea na 1GB niliyoweka.

Kwa hili swala watu tuko kimya tu kwa sababu mambo ni mengi lakini kinachoendelea kwenye swala hili NI WORST CASE SCENERIO
je ukizima data(au set net iwe 2G only), MBs zinaisha? jibu ni hapana

hauibiwi

pahala flani kwenye simu yako panavuta MBs bila wewe kujua
kutokua na elimu juu ya kitu flani usisukumie mpira mitandao na kusema unaibiwa, iyo ccna yako haina maana
 
Hii si kweli, naona watu mnashabikia pasi kufikiri nje ya box.
 
Nimeweka "kidhibiti data" tangu juzi najua apps zipo zinakula data na ni kiasi gani cha data nafahamu tofauti ya bando nililonunua na matumizi yangu. Mitandao inayoongoza kuiba bando langu hadi sasa hivi ni Vodacom na Halotel! TCRA endeleeni na mapambio yenu pumbavu!
 
Nimeweka "kidhibiti data" tangu juzi najua apps zipo zinazokula sana data na ni kiasi gani cha data nafahamu tofauti ya bando nililonunua na matumizi yangu. Mitandao inayoongoza kuiba bando langu hadi sasa hivi ni Vodacom na Halotel! TCRA endeleeni na mapambio yenu pumbavu!
 
je ukizima data(au set net iwe 2G only), MBs zinaisha? jibu ni hapana

hauibiwi

pahala flani kwenye simu yako panavuta MBs bila wewe kujua
kutokua na elimu juu ya kitu flani usisukumie mpira mitandao na kusema unaibiwa, iyo ccna yako haina maana
Ok auto-update nimeweka off! Where else ambapo data zinaweza kuwa consumed?

Uko sahihi kabisa unaposema "pahala flani kwenye simu yako panavuta MBs bila wewe kujua" na hapo ndipo tunapopatafuta
 
Back
Top Bottom