TCRA inapokea mlungula toka Star Times?

VIVIANET

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,129
2,918
Nimefikia hatua ya kuuliza swali hili kutokana na vitendo vya TCRA kunyamaza kimya wakati star times wakiweka tozo kwenye channels za ndani au local channels kama TBC ITV CHANNEL 10 Star tv wakati tuliahidiwa zitaonyeshwa bure.

Ukipiga simu star times wanakuambia siku hizi hizo channels zinalipiwa kwa sababu kuna tatizo fulani hivi ambalo halielezeki kwa kina na TCRA wanataarifa zote je wanakula mlungula au kuna nini?
 
hata mm nashangaa

Hivi sasa huwezi kupata local channels kama ilivyoanishwa katika sheria lakini chombo kinachosimamia sheria ya mawasiliano kimenyamaza kimya...ukiwapigia star times wanakuambia hadi ulipie
 
Hivi TCRA na EWURA ni ndugu wa damu?
Suala hilo nadhani Magu hajalipata, ama nusanusa wake wanatumia Zooku zinazo-scramble chanel zote ukiishiwa kifurushi.
Undava kama huu, lazima kuna mtu tena mkubwa kabisa serikalini anayeishi kwa kutumia kivuli hicho. Haiwezekani wenye mamlaka ya kusimamia hayo mambo kujifanya hawaelewi.
Wale wafuite na midomo yao ili wasieleweke walichokula. Ole wao wenye madaraka wanaoendelea kutusumbua chini ya utawala huu, wamekalia kuti lililooza.
Wawaulize maboss bodi ya korosho juzi huko sijui Songea! Wakati wanaswagwa kwenye karandinga kwenda kukojolea zululu,mibaba na vitambi vyao, walinywea kinyama, kama watoto wadogo. Ujanja wa mtu hajabanwa.
Sasa na hao waendeze hiyo dhulma na huo ushenzi wao lakini ipo siku kitaeleweka tu.
 
Tena ndugu wa damu. hii nchi inatia uchungu sana
 
Even king'amuzi cha Azam nao ni hivyo hivyo kifurushi kikiisha na local channel zinaenda likizo it's not fare... akafu bei zao kidogo zipo juu kimtindo
 
Hivi sasa huwezi kupata local channels kama ilivyoanishwa katika sheria lakini chombo kinachosimamia sheria ya mawasiliano kimenyamaza kimya...ukiwapigia star times wanakuambia hadi ulipie
kuna haja ya kununua satelite dish ama satelite antenna hd
 
Startimes ni wasanii sana coz wakati tunanua hivyo ving'amuzi vyao walikuwa na vya aina mbili.

1.Kile cha 22,000 ambacho utakuwa unalipia kila mwezi
2.Cha 89,000 ambacho channel za ndani ni bure

Binafsi nikaona isiwe shida nikachukua cha 89,000 lkn sahivi wamenikatia channel zote nikiwauliza kulikoni wanasema nilipie tu baadae wataondoa hayo malipo
 
Local channels zilikuwa hazikatwi kwa sababu serikali ilikuwa inalipia lakini JPM kakataa hayo malipo so kama kuna king'amuzi bado kinaonyesha free hizo channel basi hiyo ni bahati tu
 
Wataalamu wa madishi hivi yale madishi ambao si ya makampuni yanayouzwa madukani je yakiwekewa LNB za kutosha yanaweza kunasa bure hizi channel? maana watanzania tusiwe wajinga kiasi hicho kulipa fedha kwa channel ambazo unaweza kuzinasa free on air bure.
 
Local channels zilikuwa hazikatwi kwa sababu serikali ilikuwa inalipia lakini JPM kakataa hayo malipo so kama kuna king'amuzi bado kinaonyesha free hiz
channel basi hiyo ni bahati tu
M

Mambo ya ajabu sana haya kwa hiyo tumehujumiwa na serikali yetu basi sawa
 
Local channels zilikuwa hazikatwi kwa sababu serikali ilikuwa inalipia lakini JPM kakataa hayo malipo so kama kuna king'amuzi bado kinaonyesha free hizo channel basi hiyo ni bahati tu

Sina uhakika kama ni JPM ndie kasababisha, labda tupate ufafanuzi wa ziada.
Kumbe wanyonge na maskini wanazidi kupigika
 
Startimes ni wasanii sana coz wakati tunanua hivyo ving'amuzi vyao walikuwa na vya aina mbili.

1.Kile cha 22,000 ambacho utakuwa unalipia kila mwezi
2.Cha 89,000 ambacho channel za ndani ni bure

Binafsi nikaona isiwe shida nikachukua cha 89,000 lkn sahivi wamenikatia channel zote nikiwauliza kulikoni wanasema nilipie tu baadae wataondoa hayo malipo
Na Wewe ukaendelea kulipa tuuuu? Kwani huwezi kuishi bila star TV? Tumia nguvu yako Kama mteja.. Waambie Kama hawakurudishii hizo Chanels Wewe na wao basi.. Unakata uhusino wa kibiashara.. Watakurudishia
 
Local channels zilikuwa hazikatwi kwa sababu serikali ilikuwa inalipia lakini JPM kakataa hayo malipo so kama kuna king'amuzi bado kinaonyesha free hizo channel basi hiyo ni bahati tu
Mm niliwapigia azam tv wakaniambia kua wanakata ili ulipie kwasababu na wao wameaza kutozwa kodi ya local channel na serikali
 
Wataalamu wa madishi hivi yale madishi ambao si ya makampuni yanayouzwa madukani je yakiwekewa LNB za kutosha yanaweza kunasa bure hizi channel? maana watanzania tusiwe wajinga kiasi hicho kulipa fedha kwa channel ambazo unaweza kuzinasa free on air bure.
Ukinunua dekoda ambayo ni mzur..mm nilinunua laki na ishirini unaona chaneli zote za local na dini..ukimpata mtaalam anakusetia frequecy adi za startimz unaziona free..za azm cjajalibu
 
Mimi nahitaji hizo local tuu kwani hata hizo tunazouziwa na star timez si ni free on air za nchi nyingine?
 
Hawa startimes bado sijawasoma mimi binafsi king'amuzi nilikiacha kwa muda mrefu wakafyeka channel zote isipokuwa tbc1 na Tv1 nikalipia 6,000 wakanipatia kifurushi cha nyota na local channel nyingine,sasa nina mwezi wa pili sijalipia tena wamekata kifurushi cha nyota ila local zote wameniachia
 
Back
Top Bottom