Ni nani au nini kinaifanya "Star Times" iendelee kuihujumu Serikali ya Rais Magufuli?

Mjimwematz

New Member
Mar 17, 2018
1
0
Hivi karibuni TCRA ilitangazia umma ya kuwa wameipiga star times faini ya shilingi mil 100; kwa kosa la kukaidi kuendelea kulipisha Chanel za Local (free to air channels): lakini pamoja na faini hiyo mpaka hivi sasa wamekaidi agizo hilo! Na channels tunalipishwa kama kawaida!

Swali la kujiuliza; hivi TCRA hawajui haya?na kama hawajui hawa watu wanatuibia kodi kiasi gani?? Hivi kuna nchi yeyote duniani mwekezaji anaweza kukaidi maagizo ya serikali atakavyo akapona??

Ukifika katika office zao, wanadai 'eti ulipe sh. 24.000 ili uweze kuunganishiwa. Wanadai wanakupa kadi nyingine wakati kadi tunazotumia siku zote ukilipia channels zote zinakuja. Hii ni hujuma na haikubaliki!!

Jambo hili ni uovu na fedheha kubwa kwa serikali inajitahidi kuwatumikia wanyonge!! Ni wakati viongozi wa wizara zinazohusika waone huruma na kujionea aibu kuishi maisha ya kifahari kwa kodi za mlalahoi ambaye hawamsaidii!!!
 
Kwanini unasema inaihujumu?

Startimes (Wachina) ndio marafiki wakubwa wa CCM na Serikali yake.
 
akuna kiongozi yeyote anaeweza kukemea udharimu wa hawa wachina,hata mkulu mwenyewe anawaogopa richa ya kujinasibu kuwa upande wa wanyonge,wachina wahuni sana walitusainisha mikataba yenye masharti magumu impact yake inaonekana sasa,Hawa ndio viongozi wetu tulionao hawana huruma kwa wazawa wakishapatiwa kiasi fulani na wawekezaji wanatokomea msala wote unawaangukia wananchi wa kawaida
 
Back
Top Bottom