Maswali 4 kwa TCRA kuzuia urushwaji wa chaneli za umma

Rahel2018

New Member
Aug 10, 2018
2
8
Hivi karibuni, Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekuwa kwa nyakati tofauti ilitoa nyaraka za nia ya kutengua leseni za baadhi ya watoa huduma za matangazo ya televisheni kama vile Startimes, DStv na ZUKU​

Kwa uelewa wangu mdogo binafsi nimejikuta nikijiuliza maswali mengi sana hususan baada ya kusoma nyaraka hizo. Maswali hayo pia nimeyaona yakiulizwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii. Bila shaka hili ni suala pana zaidi kwani linawagusa moja kwa moja wananchi wengi.

Pamoja na maswali hayo mengi, mimi nina maswali matano tu kwa TCRA:
Je, wanachokifanya TCRA ni kuwapa watu au kuwanyima haki ya kufikiwa na mawasiliano?

Je, TCRA ni dhaifu katika kutekeleza majukumu yake?
Je huu ni utashi wa TCRA ama kuna mkono wa mtu?
Je TCRA inafahamu madhara ya maamuzi yake katika sekta ya Biashara na uchumi wa nchi?

Napenda niyachambue maswali haya matono kwa kina ili sisi wazalendo na walipa kodi wa nchi hii tuyaelewe bayana;

Haki ya kupata Habari
Haki ya uhuru wa kutoa maoni inalindwa na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 18 inayomhakikishia kila raia haki ya kupata habari, kutoa habari na kutoa maoni yake ilimradi tu havunji sheria

Sehemu ya 13 ya mkataba wa kimataifa wa haki ya mawasiliano (Universal Communications Service Access - UCSA Act 2006) inabainisha matakwa ya msingi ya huduma zinazotolewa na warusha matangazo ambapo pamoja na mambo mengine, wanatakiwa kuhakikisha kuwa huduma za matangazo ya msingi zinayotolewa na zinapaswa zipatikane kwa urahisi kwa watu wote kote nchini kwa usawa popote wanapoishi au kufanua shughuli zao.

Wakati nchi yetu ilipoamua kuhama kutoka kwenye mfumo wa analojia kwenda mfumo wa digitali, serikali, kwa nia njema kabisa iliweka mkakati wa kuhakikisha kuwa wananchi hawanyimwi haki yao ya msingi ya kupata habari na mawasiliano. Katika kufanikisha zoezi hili, ilitoa leseni za (Network Facility License – NFL) utangazaji kwa kampuni tatu – Star Media, BTL na AGAPE na kuwapa jukumu la kuweka mfumo utakaowawezesha wananchi kupata huduma za mawasiliano hususan matangazo ya televisheni popote walipo.
Kwa nia njema kabisa, serikali iliamua kutoa ruzuku kwa kampuni hizi kwa lengo la kuhakikisha kuwa ndani ya muda ziwe zimekamilisha uwekaji wa miundombinu itakayowawezesha watanzania popote walipo kupata huduma za mawasiliano bila kikwazo.

Zaidi ya hayo, kwa nia hiyo hiyo njema, serikali iliidhinisha mkataba wa TBC na Star Media kwa madhumuni hayo hayo ya kufikisha huduma za habari kwa wananchi tena kwa gharama nafuu.

Ikiwa kuna kampuni zilipewa hela za watanzania maskini walipa kodi, ili ziwapelekee mawasiliano, na kwakuwa baada ya muda ambao walipaswa kutekeleza hilo wameshindwa, Je ni kwanini TCRA leo hii inazinduka na kutaka makampuni ya setelait yasitishe kuonyesha chaneli za umma na kuwaachia wale ambao walitumia hela za walipa kodi na bado hawajawafikishia huduma hiyo?

TCRA watueleze, serikali ilitoa ruzuku ya shilingi ngapi kwa kampuni husika? Na hizo fedha za walipa kodi wamezipeleka wapi?

TCRA watueleze, walikubaliana zoezi hilo lichukue miaka mingapi? Na je makampuni hayo yametekeleza?? Kama yametekeleza, iweje leo bado kuna maeneo hawawezi kupata huduma hizo? Hii TCRA ni kwa maslahi ya nani? Ya uma au ya wajanga wachache wanaokula kuku kwa mrija kwa kutumia hela za walipa kodi wavuja jasho wa nchi hii?
Ni kina nani hao ndani ya TCRA wako nyuma ya hili pazia? Na wanafanya haya kwa maslahi ya nani??? Kwa mtazamo wangu, hapa maslahi ya wananchi yamewekwa kando na badala yake kuna maslahi binafsi.

Ifahamike kuwa chaneli za umma zimekuwa na mchango mkubwa sana kwa maisha ya kila siku ya wananchi. Katika nchi zinazoendelea kama Tanzania, chaneli za umma zimekuwa nguzo muhimu sana katika kutoa habari, elimu, burudani, utamaduni na Zaidi ya yote kuijenga na kuimarisha ushirikiano kati ya wananchi

Udhaifu wa TCRA katika kutekeleza majukumu yake;
Kwa mtazamo wa TCRA, zuio hili la kuonyesha chaneli za uma kwa baadhi ya watangazaji ni kwa mujibu wa sheria. Sheria husika ni sheria yenye mapungufu makubwa ya mwasasiliano yaelekroniki na posta (Electronic and postal Communications Act)
Kwanza ili kuonyesha kuwa hata hao TCRA wenyewe waliona madhaifu katika sheria hiyo, kwa mara kadhaa wamekuwa wakiwashurutisha watangazaji (DTH) kurusha matangazo ya FTA bila malipo kwa wateja. Mbali na uwepo wa sheria husika, TCRA wakati huo iliona sheria hiyo haifai na haina maslahi kwa uma hivyo ikawa inawasisitiza DTH kurusha chaneli hizo bila kuwalipisha wananchi.

Kwa mujibu wa Jamii forum – Juni 11, 2013, sehemu ya taarifa ya Statimes ilinukuliwa “…tulijaribu kuwasiliana na TCRA ambao waliamuru chanel zote za nyumbani zipatikane katika ving’amuzi vyote bila malipo…”
Baada ya muda, TCRA haohao wakabadili gia angani, wakawataka DTH waache kuonyesha chaneli za FTA. Swali hapa ni Je, kama kweli TCRA wanasimamia sheria, na wanaamini kuwa sheria hiyo ni nzuri, kwanini wamekuwa wakitoa maelekezo kinzani ka watangazaji wa DTH?

Kama hiyo haitoshi, mara TCRA hao hao, mwaka 2017, wakaja na rasimu ya kubadili kanuni za sheria ya mwasasiliano ya elekroniki na posta .
Kifungu cha 8 cha rasimu hiyo kilidhamiria kuzuia kurushwa kwa chaneli za FTA katika DTH.

Kifungu hicho kinasema (kwa tafsiri ya kawaida) "Mtoa huduma anayetaka kutoa huduma ya kurusha matangazo ya moja kwa moja ya setelaiti (Direct To Home - DTH) hapaswi kurusha matangazo ya chaneli za FTA katika vifurushi vyake.". swali hapa ni je, kama sheria hiyo ilikuwa inajitosheleza, ni kwanini TCRA walikuja na rasimu hii ya marekebisho na kusisitizia kipengele hicho kwa nguvu kubwa?

Wakati huo huo, TCRA ilitoa waraka kwa waendeshaji wa DTH ikimanisha (Azam, DStv, Wananchi - ZUKU) kuwaelekeza kuacha kurusha matangazo ya chanel za FTA katika mifumo yao. Waraka kama huo pia ulitumwa kwa chaneli za FTA

Pamoja na kujikanganya huko, nilishangaa sana nilipoona kampuni moja ambayo TCRA ilitangaza nia ya kufuta leseni yake, ikatoa taarifa kuwa suala hilo lipo katika Mahakama ya Usuluhishi wa Kibiashara (Fair Competition Tribunal). Hivi kweli TCRA hawajui kuwa kama suala lipo mahakamani inabidi uamuzi wa mahakama usubiriwe kwanza ndiyo hatua zichukuliwe? Huu ni udhaifu mkubwa na wa kutia shaka. Sisi wananchi tunatarajia taasisi kubwa kama TCRA ziwe mfano wa kuigwa katika kuheshimu sheria na taratibu. Badala yake wanakuwa wa kwanza kuzikengeuka. Hili ni la bahati mbaya kweli au kuna mkono wa mtu??

Je, huu ni utashi wa TCRA?
Nimetathmini matukio ya siku chache hizi, nikahisi kabisa hapa si bure. Nadhani kuna kitu kikubwa kinaendelea. Ni wiki moja tu imepita tangu TCRA watoe tishio la kufuta leseni ya Star Media kwa madai ya kushindwa kurusha bure channel za FTA!. Hivi, hawa Star Media si ndio waliopewa mabilioni ya walipa kodi ili iweze kuweka mfumo wa mawasiliano nchi nzima? TCRA watuambie kwanza, Je Star Media walipewa ruzuku ya shilingi ngapi? Na kwa ajili gani? Na walipaswa kutekeleza hilo kwa muda gani?

TCRA watujuze sie walipakodi, je hela zetu walizopewa Star Media, wamezipeleka wapi?kwanini hadi hii leo kuna maeneo hayawezi kupata huduma za matangazo ya DTT?
TCRA watuambie, ni kwanini muda wote huo Star Media walikuwa wanawalipisha wateja kulhali walipewa ruzuku ya serikali kwa ajili ya kusambaza mtandao nchi nzima?
TCRA watuambie kuhusu ving’amuzi vya teknolojia ya T1 vilivyosambazwa na Star Times, Je ni kweli TCRA walibariki Tanzania kuwa dampo la teknolojia iliopitwa na wakati? Walifanya hivyo kwa maslahi ya nani?

Baada ya miaka nenda rudi, hivi majuzi Star Media wamekuja na mchapo mpya wa kitapeli. Katika tangazo lao kwenye vyombo vya habari mapema mwezi huu wa Agosti, wamesema kuwa kuna ving’amuzi vya aina mbili. Vile ambavyo vina chanel za bure, na vyenye chanel za kulipia. Lakini ujanja waliofanya, vya chanel za kulipia vinauzwa bei chee, vya chanel za bure bei maradufu… sasa hawa si ndio wale wale walipewa ruzuku na serikali? Tena leo hii waje kuuza ving’amuzi vya FTA kwa bei ya dhahabu? Na TCRA imekaa kimya inawatazama tu…. Hii ni kwa maslahi ya nai??

Namshukuru sana rais wangu. Hivi majuzi aliwatolea uvivu kuhusu ndoa yao na TBC. Watu gani wanafanya biashara eti miaka nenda rudi hawatengenizi faida? Lakini wakati huo huo hawafungi biashara?? Je hii inaingia akilini??

Maadhara ya maamuzi ya TCRA kwa Biashara, Uwekezaji na Uchumi kwa ujumla
Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi sana tangu nilipoanza kuliona sakata hili wiki chache zilizopita. Lakini kilichonishangaza zaidi ni pale niliposoma kuwa eti suala la TCRA imetishia kufuta leseni wakati shauri lipo kwenye makakama ya usuluhishi wa kibiashara likisubiri maamuzi. Hili ni suala la kutia wasiwasi na mashaka makubwa.

Mimi binafsi sipingani na TCRA, ikiwa wanasimamia sheria,. Lakina katika kila soko, na kila nchi kote ulimwnguni, kuna mamlaka za udhibiti – kama ilivyo TCRA, EWURA, SUMATRA na kadhalika. Lakini pia, kwa hali halisi ya biashara, kutokea kwa kutoelewana kati ya pande moja na nyingine – iwe ni kati ya kampuni na kampuni, au kampuni na mamalaka ya udhibiti, ni vitu vya kawaida kabisa. Kwa msingi huo ndiyo sababu kote duniani kuna mamlaka za usuluhidhi. Kwa Bahati nzuri sana sisi hapa tanzania kwenye masuala ya biashara na uwekezaji kuna tume ya Ushindani huru wa Kibiashara (Fair Competition Commission) na pia kuna Mahakama ya Ushindani wa Kibiashara (Fair Competition Tribunal). Hizi ni mamlaka zilizoundwa kwa mujibu wa sheria

Nimeshangaa sana kuona kuwa TCRA inadharau uwepo wa taasisi hizo na diyo maana wanaweza kutoa waraka wa nia ya kufuta leseni wakati shauri hilo lipo katika mahakama ya usuluhishi wa kibiashara. Hili linatia shaka na kupunguza uaminifu kwa TCRA.
Tabia kama hizi kwa mamlaka zetu za udhibiti ni kitisho kikubwa kwa uwekezaji wa ndani nan je na ni saratani ya ukuaji wa uchumi wa nchi. Hili si suala la kufumbiwa macho hata kidogo. Katika zama hizi za kujenga tanzania ya viwanda, vikwazo kama hivi ni sharti viondolewe. Kama kuna sharia zenye walakini zibadilishwe! Lakini zibadilishew kwa manufaa ya wananchi walio wengi.

Nilipata Bahati ya kuona rasimu ya TCRA ambayo nadhani ilikwama. Kilichonishangaza zaidi, ni pale nilipoona nia ya TCRA ya kutaka pia iwe inafanya usuluhishi! Huenda nsiyo sababu hata inadharau Mahakam ya Usuluhishi wa Kibiachara kwa kutoa matamko wakati shauri lipo mahakamani.

Lakini kwanini TCRA inataka iwe kila kitu? Iwe Kepteni wa timu, Refa, na Kamisaa wa mchezo kwa wakati mmoja. Hii inawezekanaje???

Ninaamini kuwa TCRA italitafakari tena suala hili kwa kina na kukaa meza moja na wadau na kuangalia njia bora ya kulitatua badala tu ya kutishia au kutengua leseni za watangazaji. Hivi leseni ya Azam, au Zuku, au DStv ikitenguliwa ni watanzania wangapi watakosa ajira? Serikali itakosa mapato kiasi gani? Watu wangapi watakosa huduma ya mawasiliano ambayo ni haki yao ya kikatiba?
Bila shaka TCRA na serikali kwa ujumla italiona hili na kuhakikisha kuwa sisi wananchi hatuadhibiwi kwa kunyimwa haki ya habari kwa sababu zozote zile.
 
Duh.. Hongera kwa makala ndefu na ufafanuzi murua. Ila nna mashaka kama wale watu wa tcra wana uwezo wa kuelewa hii dossier!
 
Naona yametimia mkuu.. Kwa channel za ndani tayari wamebakiza tbc1 pekee kwa ajili ya kunadi utukufu wa sisiemu!

Sasa upende usipende, kusikiliza propaganda ni lazima. Labda kama unakwepa habari za home.

Ajabu ni kuwa za nje zote zinaonekana
 
Nani anajali ndugu? Kwani hata hizo chanel za kibongo zikibaki kuna kipi cha maana kinachooneshwa humo au ccm kufanya Gulio Nashauri ndugu usipoteze muda wako kudai hizo chanel ni upuuzi tu ulioko huko
 
Back
Top Bottom