Naomba kwa anayejua namna ya kusitisha hizi sms za BIKO maana zimekuwa kero nilicheza siku moja tu sijarudia tena lakini wao kila dakika wanakutumia txt. Mwenye kujua namna ya kuzisitisha msaada tafadhali.
Ningependa kuwakilisha kero inayo nikumba mimi pia hata watu wengi tu.
Haya makampuni ya michezo ya bahati nasibu kutuma SMS kila wakati pasipo option ya Usubscribe.
Mimi nimecheza mara moja tu, sasa kwann kila siku asubuhi, mchana, usiku mnanitumia SMS zenu..... kwani nimeji subsribe for news & updates?????.... hizi message zinaboa kweli kweli pia ni usumbufu kabisa.
Tena sikuhizi hadi wanakutaja jina kabisa.
OMBI KWA TCRA
Wekeni mikakati ambayo hawa makampuni waweke namba ya kutuma neno ONDOA ili waweze kujitoa na SMS za kinafiki
Pia kwanini wamtumia SMS pasipo makubaliano baina ya mteja?
Naimani maofisa wa TCRA mmeliona hili. Nawatakia utekelezaji mwema.
Aiseeee
Nimechoka kila baada ya muda mfupi napata jumbe toka biko sport ikinikumbusha habari za betting
Huu ni usumbufu kwa watumiaji wa voda, najua hii itakuwa ni kero kwa wengi bila shaka, naomba njia naiepuka vipi
Halafu sijui wanatoa wapi idhini ya kuchukua namba zetu na kuanza kututumia ujumbe wa usumbufu muda wote
Inakera sana kwa na sijui ni namna gani tutakuja!
Jumapili niliwapigia Vodacom kuwaeleza huu kero na ushenzi wa meseji kutoka kwa kampuni za kubashiri i.e BIKO, Tatu mzuka, mkekabet kuja kwa simu yangu nikaomba wanitoe kabisa na sitaki tena kutumiwa hizo jumbe, eti wakasema wao hawahusiki kwa chochote na kama kutoa niwapigie kampuni husika za kubashiri au niwapigie TCRA na kutoa malalamiko yangu.