TCRA Hii ni Haki kufanyiwa Uhuni Huu na Makampuni ya Simu? Mimi mtumiaji nina haki zangu za Msingi

Sodoku

JF-Expert Member
Feb 3, 2016
1,095
2,429
Kumeibuka mtindo wa Makampuni ya Simu hasa Airtel na tigo kuingilia simu za watumiaji. na wakati mwingine unapopiga kwa mtu unajikuta badala kwanza ya simu huita kwa mhusika wanaanza kwanza kukupa matangazo yao. kukweli hii tabia inakera. binafsi napopiga simu kwa mtu nataka instantly simu ianze kuita na pengine kupokelewa na mhusika pasipo kupoteza muda. bahati mbaya nayi mnataka mtumie muda huo huo kunipa matangazo yenu ambao mimi sikuwa nimeyaomba. ni wakati mwingine unakuta ni simu ya dharura au ya haraka sana. hii tabia TCRA tunaomba mtusaidie kuikomesha

tatizo lingine naliona hasa kwa AIRTEL wao wanakupigia simu kwa namba zao mbalimbali. ukipokea wanawaanza kukueleza huduma zao kupitia Mashine. imagine ulikuwa na kikao muhimu unapoona namba mpya kwenye simu yako na kama ulishafanya applications za kazi sehemu nyingi. unapopokea wanakuuliza kaam utapenda wakuwekee call tone/tune. huu ni uhuni wa hali ya juu sana.

suala lingine ni kutumiana msg za promotions kwenye simu. hata kama natumia mtandao wenu haimaanishi sasa ninyi mna icontrol simu yangu na mnaweza kutuma chochote mnachojisikia. na mengine mnayotuma hayaendani na imani yangu. hamwoni kuwa mnakwaza watumiaji wa simu?lakini kwa nini pia mnijazie simu yangu kwa msgs zenu kila siku?huu ni uhuni ambao sikubalian nao kabisa na naomba TCRA mliangalie jambo hili. lakini pia sidhani KAMA TRA wanafuatilia aina hii ya matangazo na kuchukua kodi. hili nalo liangaliwe.

lakini mimi mwenye simu nahitaji privacy. kuna kipindi nahitaj kusikia simu moja au msg moja toka kwa mtu muhimu. hivyo siwezi zima simu ingawa wengine naweza waambia nipo busy au kuwa block temporarily lakini mnapoanza kunipigia au kunitumia msg mnaniharibia utaratibu wangu

imagine upo kwenye shughuli nyeti flan hivi ukijishughulisha sana kwa umakini. mara simu yako inaita. kwa sababu ulikuwa unategeme simu kutoka kampuni au kwa mteja flan unamtegemea. inapopigwa simu unawah kupokea. unapopokea unakuta sauti inakwambia karibu mteja flan tuna huduma ya wimbo flan kama unataka subscribe ... au inaingia msg ya kipuuzi kuhusu gulio/bazaar la simu mliman city. stimu yote inakatika ukirudi inabidi ukanze upya
 
Back
Top Bottom