Inanishangaza kuona kuwa msimamizi wa mawasiliano Tanzania, TCRA, yuko kimya na hachukui hatua zozote dhidi ya huduma za kiudanganyifu zinazotolewa na baadhi ya hizi online TVs.
Kuna udanganyifu mkubwa na kutokuwa na uweledi unaohusisha hizi online TVs, ambao kwa kweli, lazima hatua stahiki zichukuliwe.
Udanganyifu huu unahusisha uwekaji wa vichwa vya habari ya clips ambazo haziendani na story zenyewe kwenye habari husika kwa minajili tu ya kudanganya watu wafungue hizo clips. Huu ni uharamia na ugaidi wa habari ambao unabidi uchukuliwe hatua. Kama online TVs zimesajiliwa na TCRA zinatakiwa ziwe na weledi kama vile magazeti and radio zingine zinavyofanya kazi. Haiwezekani kichwa cha habari kiwe ni kuhusu 'mbuzi' lakini ukifungua hiyo clip story inayoongelewa ni ya 'ngombe'.
Pili online TVs zinachochea sana chuki na maadili mabovu kwa jamii. Natambua ya kwamba hiyo ndio content watanzania wanafurahia nayo, lakini lazimia kuwe na weledi wakuileta hiyo content kwa jamii. Mfano, haiwezekani habari zote za wasanii ni kuhusu ugomvi au kutukanana kama vile hamna habari zingine zozote za kurusha. Yaani mtu anapata nafasi yakupata story kama anamtukana msanii mwenzake.
Tatu online TVs zina 'waandishi' ambao ni mbumbumbu kweli kweli. Ni muda sasa, hata hawa 'waandishi' wawe na vigezo vya elimu ili kuruhusu wawe wanarusha habari niweledi zaidi. Basi hata cheti tu cha uandishi wa habari. Wengi wao hawana weledi kabisa wa kujua habari gani iletwe kwa jamii na ipi isiletwe au hata tu kuuliza maswali.
Kwa kweli TCRA acheni uvivu na fanyeni kazi yenu kama mtavyotakiwa kisheria. Upuuzi huu wa baadhi ya online TVs umefika mahali ambapo sasa hatua stahiki lazima zichukuliwe