TCAA kusajili ‘drones’ zote kielektroniki

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imezindua mfumo mpya wa kielektroniki ili kutoa urahisi kwa watu wanaorusha ndege zisizokuwa na rubani (drones), kutuma maombi ya vibali na usajili wa ndege zao ndani ya muda mfupi.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mfumo huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Daniel Malanga amesema lengo la kuanzisha mfumo huo ni kuondoa kero waliyokuwa wakikutana nayo warushaji wa ndege hizo hapo awali.

Malanga amebainisha kuwa kuanzishwa kwa mfumo huo kutafanya upatikanaji wa vibali kutumia takribani wiki moja hadi mbili, kutoka mwezi mmoja hadi miwili iliyokuwa ikitumika hapo awali ambapo mchakato huo ulikuwa ukifanyika kwa njia ya kawaida na ulimlazimu aliyehitaji kibali kupita katika ofisi mbalimbali kushughulikia suala hilo, jambo lililochukua muda mrefu.

“Kwa biashara hii ni changamoto ambayo inaathiri mwenendo wa biashara na leo hii utatatuliwa kwa mfumo mpya, hii ni baada ya TCAA kuamua kuwarahisishia watumiaji wa ndege hizi kwa kutekeleza mfumo utakaorahisha mchakato wa upatikanaji vibali kuanzia usajili na matumizi,” amesema.

Aidha, amesema mbali na kusajili mfumo huo pia utawawezesha watu kuwasilisha maombi mbalimbali ikiwemo ya vibali vya kuingiza ndege hizo, kutoa ndege, na kutumia ndege hizo.

“Sambamba na huduma hizo pia kutakuwapo na urahisi wa utoaji wa taarifa za uendeshaji wa ndege hizo hasa sehemu ambazo mtumiaji anatarajia kwenda kufanya shughuli zake kwa njia rahisi tofauti na awali,” ameongeza.
 
Kiswahili sahihi cha "drone" ni ndege inayopaizwa na rubani asiye ndani yake. Mtu amekaa ardhini anahangaika kuendesha ndege halafu mnasema haina rubani!
 
Hivi anga ya serikali inaanzia kimo cha futi ngapi? Duh! Kila kitu ni cha serikali, mara mamlaka, mara wakala, ila kuna vitu viko vingi tu bado serikali haijaviundia mamlaka na wakala.
 
Wataunda hadi mamlaka ya wakata viuno.
Yaani unagegedana na mkeo/pisi yako lazima uwe na kibali cha mamlaka ya wakata viuno.
 
Hivi anga ya serikali inaanzia kimo cha futi ngapi? Duh! Kila kitu ni cha serikali, mara mamlaka, mara wakala, ila kuna vitu viko vingi tu bado serikali haijaviundia mamlaka na wakala.
Swala la matumizi ya anga ni nyeti kidogo. Waulize wanaofanya kazi sekta ya usafiri wa anga watakwambia...
 
Kwa hiyo nikiwa na drone zangu za kupiga picha na kumwagilia viuwatilifu mashambani mwangu lazima nipate kibali na kusajili serikalini?
 
Kwa hiyo nikiwa na drone zangu za kupiga picha na kumwagilia viuwatilifu mashambani mwangu lazima nipate kibali na kusajili serikalini?
Wenzetu wanafikiria zibebe mizigo kabisa....kinatoka posta jamaa anapokea mzigo wake mwenge...anapakia unaokuhusu kinakuletea posta...hapo boda bye bye
 
Back
Top Bottom