2. TBT
Muendelezo
Basi maisha ya kumiliki ofisi yakaanza rasmi.
Boss alikuwa akinipenda sana na kunidekeza sana yaani mpka nikawa raha zaidi kuwa ofisini kuliko nyumbani.
Kipindi yotee haya yanaendelea nilikuwa bikra yes nilikuwa bikra!!!!! Nilikuwa nimehaidiana ku oana na kijana mmoja hivi kwa sasa ni moja Kati ya madaktari bingwa hapa Tanzania.
Boss ikawa kila safari na mimi nimo,, akafanya mpango mpaka nikawa napelekwa na kurudishwa nyumbani na gari ya serikali japo cheo sina.
Nikahamishwa jengo na tukawa rasmi jengo moja na boss.
Basi Kuna siku boss akaja ofisini akaniwekea bahasha ndani ilikuwa na pesa kama laki5 hivi..[ ukweli mi napenda pesa niliiipokea vizuri kabisa na nilifurahi sana]
Basi kesho yake akaja ofisini kwangu akasema tutoke sikukataa nilikubali.
Jioni dereva alinipeleka sehemu husika nikatumia hapo chakula na vinywaji boss kaniimbisha!!!!
kiukweli boss wangu alikuwa ni moja ya viongozi ma handsome kwa wakati huo na pesa kwake haikuwa tatizo na ubahili ndio hana kabisaaaa.
Alihitaji kunimiliki kabisa.
Mimi nilimueleza ni bikra na nina mtu anaetakiwa kuitoa.
Boss kusikia hivyo alidata na akaniambia hajawahi kutoa mwanamke bikra na hata mkewe hakumkuta nayo.
Nilibembelezwa siku ile lakini nilikaza nikimkumbuka boyfriend wangu sikuweza.
Basi nilirudishwa nyumbani na kuanzia hapo nikaanza kubanwa,, chakula nikawa naletewa lunch box,, tukisafiri tuna lala hotel moja na vyumba vinaangaliana.
Mimi nina mama zangu wadogo mashangingi wa enzi hizo nikawaelezea hitimisho ikawa niende kwa doctor anitoe bikra then nije kwa boss.
Boss nilimshirikisha akaniambia nakupeleka mwenyewe mkamalizane tuanze mapenzi yetu
Huku doctor wangu alikuwa bugando pale anasoma na masomo yake mwenyewe.
Nilienda bila taarifa na alinipokea kilichoniumiza zaidi alikuwa tayari ana mwanamke na ana mimba.....
akaniambia ooh! nisamehe nisingeweza kukusubiri oooh! utakuwa mke wa pili!!!!!.
Aiisee hakuna kitu iliniuma kama ile........
Tulifanya mazungumzo kama masaa mawili hivi...
Mi nina misimamo yangu niliona ni bora bikra niipeleke huku kuliko kumpa mtu ambae alishindwa kunisubiri.
Kutoka zile hostel za Kiume pale bugando mpka getini nilienda namlaani.
Dereva alikuwa ananisubiri na nilikipeleka kweli hatimaye boss alinitoa bikra nakumbuka mpaka machozi yalimtoka...
Maisha mapya yakaanza ya mahusiano mahusiano ambayo sikuwahi kujutia hata kidogo...........
Mama zangu wadogo walinishauri na boss akakubali nikahamishwa ofisi na kidogo nikapata ka cheo lakini kazi na ratiba zilikuwa zinafanana sana.
Hayo yote yanatokea nilikuwa kama nina miaka 23 au 24.
Tulisafiri nilikula bata za kila aina.......
Boss alinijengea nyumba maeneo ya CINE CLUB kwa wenyejiwa dar wanapajua.
Yote haya yakiwa yanaendelea nilikuwa napenda sana kusali,, hapo katikati nilichaguliwa kuwa muhasibu vijana jimbo kitu ambacho kilinikutanisha na mrembo mmoja wa enzi hizo ambae alikuwa anatoka na mkuu wa nchi pamoja na askofu fulani hivi......
.
Nawarudisha nyuma mimi sikuomba kazi bali mjomba wangu ndio alinipeleka kwa boss siku ya interview na boss kumbe alielewa mzigo na ndio maana nilipita bila kupingwa.
Ndio maana yule dada kwenye tbt namba moja alikuwa akinichukia sana.
na pia kwa wakati huo mimi nilikuwa nasafirisha dhahabu za mjomba wangu na wenzie.
Yaani ikisha chomwa natoa kwao na kumpelekea boss ambae anawapa pesa za kununulia na ndio mdhamini mkuu.
Hiyo nimeeleza kidogo ndo uelewe connection iliyomfanya mjomba kumjua boss na mpka mimi kupelekwa kwa boss siku ya interview na kupata kazi.
Maisha yakasonga boss akaja nyumbani kutoa mahari......
Na kwa msaada wa mjomba wangu [ Apumzike kwa amani] boss alitoa ng'ombe 50 za kutembea na tulifanya mambo ya kimila hapo boss rasmi akawa mume kwa desturi za kisukuma.
Lakini hapo kwa msaada wa mama wadogo na mjomba wangu kwa boss tulikuwa kikazi zaidi.... japo nilikuwa nampenda kidogo.
Tukutane TBT alhamisi ijayo.
ya kulalia hii.
NB;
Nilipanga niwe natupia picha japo zile ambazo mimi naonekana sana mpka mwisho wa story mngeona nilivyo kwa sasa ila mmenitisha.
Twendeni hivyo hivyo bila picha.