Wapendwa habari zenu.
Leo nimeona niwaletee vi story vyangu na vitakuwa vinapatikana humu kwa mtindo wa picha za zamani na matukio yake.....
1. story namba moja
Hapo chini nakumbuka ilikuwa event moja miaka hiyo!!!!
Mimi nilibahatika kupata kazi nikiwa mdogo sana huku sina uzoefu wa aina yoyote siku hizi mnaita fresh from school. na kiukweli nikitaja hiyo nafasi ni ndogo sana lakini majukumu yake ni makubwa.
Nakumbuka sijui kilitokea nn lakini kwenye ile nafasi tukawa wawili, mwenzangu ni mzoefu mimi sijui lolote kuhusu ile kazi.
Bwana ee!!! nakumbuka baada ya kuanza kazi wikiend iliyofuatia kukawa na event!!!! ilikuwa kuchangia sijui maendeleo ya nini mi nilishasahau.
Dada nikaupura jifanyia service kama picha hapo chini inavyosema
.
Ukafika muda wa michango jamaaniii!!!!!!
Mi badala ya kuwa naandika jina na amount au ahadi niko bize kushangaa matajiri maana wengi wao sikuwa nawafahamu wala kuwajua,, mishangazi niliyoikuta ofisini ikawa inanionyesha tu unamuona fulani? unamjua yule...
Ghafra ile iliisha usiku sana basi boss wangu akatuma dereva kuniuliza kama naenda nyumbani aunaendelea kushereheka maana walikuwa wameandaa na sehemu ya ku party. niliamua kuondoka
Jumatatu ikafika na mrejesho wa ile ghafra ulikuwa unatakiwa
Bwana bwana yule mwenzangu (utamuona kwenye picha hapo anaenifuatia baada ya mimi kwenye mstari wa chakula)
Akaingia kwa mikwara huku anajigamba kaandaa ripoti na hapo si alikuwa anajigamba kwa sababu anajua sijui kitu. yaani sisi wanawake pepo tutaisikia motoni!!!!
Boss wetu akafika baada ya muda kidogo simu tukaitwa mmoja mmoja,,,, mwenzangu akawathirisha ripoti yake.
Mi naitwa sina hili wala lile nikafika nikakaa nikwambia ndio boss!!! ripoti iko wapi??? full confidence nikamjibu sikuandika sina!!!!! akaniangaliaaa akatabasamu akaniambia next time kuwa makini.
Narudi ofisini kila mtu ananiuliza vp?? mie hakuna kitu boss anasemaje na mie sijui???
Bi dada alinuna sana kuanzia siku hiyo akaanza kunichukia na kunisema vibaya. nilisemwa mimi sikuwa napumua mule ndani.
Kupitia kwa yule dada kuwa ananisema vibaya nilianza na mimi kujifunza kazi kwa nguvu..
Hasa walionisadia sana ni vijana wa kiume tuliokuwa nao pale!!!! nilipambana mpka kikaeleweka na mimi nikajua kazi na taratibu zote za pale.
Baada ya miezi Sita yule dada alihamishwa kazi akapelekwa sehemu nyingine.
Nikakabidhiwa ofisi na mimi rasmi nikakalia kiti katika nafasi niliyokuwa nayo.
Tukutane wiki ijayo.
BN; Hizo picha ni miaka 18 iliopita na kwa sasa ni bibi mmoja hivi waja hamkawii kuanza kuropoka.