TBS kwa nini mmeifumbia macho Rungu?

E2BK

Senior Member
Jul 8, 2012
153
183
Habari za muda huu wakuu? Poleni kwa msiba wa mzee wetu.

Naomba niende kwenye hoja yangu, kuna hii dawa ya kuua wadudu aina ya Rungu imekua kimeo sana sijui kama TBS wanaliona hili.

Nimekuwa mteja wa dawa hii kwa muda kidogo na pale mwanzo ilikuwa vizuri sana lakini kadri siku zinavyoenda hakuna kitu kabisa.

Unapuliza dawa mbu hata hawafi wala kulewa badala yake inakuwa kero kwa harufu yake kali na mbaya.

TBS na wote mnaohusika kusimamia hebu tusaidieni kwa hili pengine hawa ndugu zetu wamejisahau wanaangalia faida wamesahau kuangalia ubora wa bidhaa yao.
 
bora umeweka huu uzi na wao waone, maana ni kero kwa kweli...

nikifika mara ya kwanza mkoa fulan, kwa kuwa nikipata shida ya usumbufu wa mbu, nikajaribu Rungu kwa kuwa dawa zingine hazipatikan...

niliitupa dawa ya Rungu, mikiwa nimetumia mara tatu tu
 
Wabongo kwa lawama, lawama, lawama, lawamaa hatujambo. Kila kitu mpaka mtu kakosana na mpangaji wake utasikia serikali, serikali, serikaliii.

Hili ni soko huria, kama RUNGU haifanyi kazi nunua HIT kwani umeshikiwa bastola kununua RUNGU.

Kila mmoja akiona haifai akaamua kununua BRAND nyingine RUNGU itajifia tu NATURAL DEATH au watarekebisha, basi.
 
Mkuu kwanza harufu yake imekuwa kali mno lakini utendaji wa kazi hamna kabisa.

Mwanzoni ulikuwa ukipiga dawa unawaona mbu chini lakini sasa hivi wanadunda tu.
 
Wabongo kwa lawama, lawama, lawama, lawamaa hatujambo. Kila kitu mpaka mtu kakosana na mpangaji wake utasikia serikali, serikali, serikaliii.

Hili ni soko huria, kama RUNGU haifanyi kazi nunua HIT kwani umeshikiwa bastola kununua RUNGU.

Kila mmoja akiona haifai akaamua kununua BRAND nyingine RUNGU itajifia tu NATURAL DEATH au watarekebisha, basi.
Yaan we ndo pimbi kweli mdau kaleta hii mada ili hata wengine wasaidike kwa kujua kuwa bidhaa ya rungu kwa sasa haina ubora
 
Ingekuwa hivyo hata wale vifaranga kutoka Kenya tungewaacha ili mtu akila akipata shida ataacha mpaka wakose soko.

TBS, TFDA na mamlaka nyingine zipo kisheria na zinatakiwa kuwajibika kwahiyo kukaa kimya sio suruhuhisho sahihi.

Bora lawama.....
 
Yaan we ndo pimbi kweli mdau kaleta hii mada ili hata wengine wasaidike kwa kujua kuwa bidhaa ya rungu kwa sasa haina ubora
Wewe takataka, mtu kama haoni ubora wa bidhaa haihitaji kushawishiwa kuona bidhaa fulani haifai.

Vichwa mnafugia nywele tu.
 
Hii dawa ina athari kwa kweli. Tulitumia nyumbani tuliumwa mafua makali na asubuhi tuliamka miili inauma Kama tumepigwa. Tulivyoacha kuitumia tukapona, dawa ya rungu ni majanga
 
Binafsi nilikuwa mteja sana wa hii dawa ila nimeiacha kwanza haifanyi kazi km zamani pili inaharufu kali kiasi kwamba inapelekea koo kukauka wakati unapuliza na kukohoa bala.
 
Mafua ni uhakika kupata ukitumia dawa yao
 
Back
Top Bottom