TBS Kupatiwa cheti cha Umahili kutoka Kampuni ya SADICAS

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
TBS KUPATIWA CHETI CHA UMAHILI KUTOKA KAMPUNI YA SADICAS

Shirika la viwango nchini Tanzania (TBS), linatarajiwa kupatiwa cheti cha umahili kutoka kampuni ya sadicas May 12,2022 jijini Dodoma kutokana na kukidhi vigezo vya kimataifa.

Akizungumza mapema leo jijini Dar es salaam, Kaimu Meneja wa Kitengo cha Usimamizi wa Mifumo ya Ubora (TBS) Bi.Magdalena Sedemaki amesema kuwa utolewaji wa cheti hicho ni uthibitisho wa utoaji wa huduma bora na kuifanya kampuni hiyo kuwapatia cheti hicho ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Uwezeshaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud S. Kigahe.

Aidha utolewaji wa cheti hicho ni uthibitisho kuwa TBS inatoa huduma kwa kuzingatia mifumo ya kimataifa.

Pia amesema cheti hicho kitasaidia kupunguza gharama kwa wadau wakati huu wa UVIKO 19 sababu huduma hii itapatikana hapa nchini kupitia Shirika la Viwango Tanzania (TBS)

IMG-20220510-WA0308.jpg
 
Back
Top Bottom