TBS, hili la ukaguzi wa magari baada ya meli kufika bandarini sidhani kama limekaa sawa!

mr c

Member
Jan 16, 2019
14
45
Nikiongea kama Wakala wa forodha mzoefu kwa hili mmechemka kabla ya zoezi kuanza.

Swali ambalo najiuliza na hamjalitolea ufafanuzi ni kuhusu sheria ya bandari kuhusu ziku saba za mwanzo yani free day kutochaji storage je mna mkataba wowote na mamlaka ya TPA? endapo mtachelewesha ukaguzi wenu wateja wasilipe storage?

Maana sheria ya TPA now meli ikipaki tu system inaanza ku’count hata kama gari haijashuka kwenye meli gari imeshaingia au tunaita ku’carry in.

Utaratibu wenu wa zamani wa kwenda kukagua NIT kwa magari yasiyokaguliwa nje ya nchi ulikua mzuri sana! Mteja anatoa gari yake nje ya bandari na anapewa siku 21 awe ashalipeleka NIT kwa ajili ya ukaguzi na endapo halijakidhi viwango ataruhusiwa akalitengeneze ndani ya siku 21 awe ashalirudisha na anaambiwa halijafudhu hiki na hiki

Na likifudhu unapewa certificate kwa ajili ya usajiri.

Nisichoelewa ni kwamba endapo gari imefika na wakat mnalikagua likafeli je utaratibu upi unatumika kwa ajili ya kulitoa nje ya bandari na kuenda kulitengeneza?

Kwa maana magari ya local taratibu zake tofaut hapa nazungumzia ambaye bado hajakamilisha taratibu za kodi?

USHAURI WANGU
Wazo lenu ni zuri mno kwa ajili ya kuboresha uchumi wetu maana nilisikia mkisema mlikua mnapata %30 na kwa sasa mtapata %100 ila ingekua vizur zaid mngetumia utaratibu wa NIT wa zamani gari itoke awe nayo mwenyewe apewe na hizo siku kwa ajili ya inspection

Ili ipungue kero kwenu na kwa mawakala

Pamoja katika ujenzi wa taifa

P.o box 07
Dar es Salaam
 
voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
376
500
Umeshauri vizuri na ingekuwa vema hizi taasisi zetu kitaifa kuwa na utaratibu wa kuwashirikisha wadau husika kila wanapokusudia kufanya mabadiliko makubwa makubwa ya kimfumo kama haya ya sasa.

Hiyo inasaidia kuondoa usumbufu,gharama,hasara na pia lawama mbalimbali ambazo zingeweza kuepukika toka kwa jamii yetu.
 
Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
48,514
2,000
Umeongea ukweli mtupu maana hii pia itaturudisha kule tulipotoka kwa mizigo kurundikana bandarini na pia watu wataanza kuikimbia bandari ya Dar es salaam kabisa.

Kama TBS walikuwa wanajua fika kabisa hawatoongeza mikataba ya mawakala wakubwa hivyo walitakiwa kutoa taarifa mapema sana kuhusu hili jambo ili watu wajue na pia hii kazi walitakiwa kuwapa watu waifanye nje ya bandari tena mawakala wengine wa ndani.

Nilitegemea lengo la kuvunja mikataba ya nje uko ni kuhamishia hizo ajira ndani ya nchi kwa kushirikiana na sekta binafsi...lakini hii ya TBS kutaka kufanya wenyewe haitawezekana zaidi ni bandari kurudi nyuma kwa ucheleweshaji wa mizigo na mizigo kurundikana bandarini.
 
dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
14,889
2,000
Swali; kwa mfano gari by all means limeshindwa kukidhi vigezo vya kusajiliwa yaani halifai kwa matumizi hapa nchini; utaratibu utakuwaje? Kwa gharama za nani? Hayo ndio maswali ya msingi kwenye hii issue.

Ukaguzi ukifanyika nje, kama gari halijakidhi vigezo, unapewa option ya kuchagua gari lingine lenye bei sawa; kwa case ya ukaguzi wa TBS, mteja atapewa option hiyo?
 
Mtukutu wa Nyaigela

JF-Expert Member
Sep 4, 2018
3,539
2,000
Ndo maana kumbe usumbufu ulioonekana hii January. Itachukua karne nyingi sana Waafrika kustaarabika
Hapa kuna kikundi kimeona mwanya wa upigaji
 
mr c

Member
Jan 16, 2019
14
45
Swali; kwa mfano gari by all means limeshindwa kukidhi vigezo vya kusajiliwa yaani halifai kwa matumizi hapa nchini; utaratibu utakuwaje? Kwa gharama za nani? Hayo ndio maswali ya msingi kwenye hii issue.

Ukaguzi ukifanyika nje, kama gari halijakidhi vigezo, unapewa option ya kuchagua gari lingine lenye bei sawa; kwa case ya ukaguzi wa TBS, mteja atapewa option hiyo?

Hapa wakubwa wenzetu wamepuyanga hawajufanya kwa sababu ya masilahi ya watanzania wenzao,waliwaza ila hawakuwazua

Ilikua na faida kwa mnunuzi maana kulikua na uwezekanao wa kufanyiwa service kwa tatizo dogo na kubadilirishiwa gari kwa tatizo kubwa

Ipo wazi watanzania wengi uwezo wetu wa kununua gari ni USED na TRA wanachaji UCHAKAVU,sasa uchakavu unalipa na service unalipa endapo limefeli na hii itapelekea sana kuuziwa magari mabovu kwa makampuni mbali mbali za uuzwaji wa magari nje ya nchi
 
... wao walichokimbilia ni "hizo fedha zinazoenda kwa mabeberu zirudi nchini"; hawakuona athari nyingine zitakazotokana na uamuzi wao huo. Iko hivi, gari likija bovu, mteja kala hasara ya mamilioni (sijui TRA watamrudishia kodi yake?), Tanzania imekuwa dumping place kwa sababu responsibility imekuwa shifted kutoka kwa muuzaji kwenda kwa mnunuzi/Tanzania!

Kwangu, it is by far better, waache utaratibu wa ukaguzi kufanyika nje kama ilivyo, then kama wanaitamani sana hiyo USD 100 hadi 300 ya ukaguzi mteja awalipe TBS (bure kabisa bila wao kufanya kazi yoyote) ina manufaa kwa mteja na kwa nchi kuliko hicho wanachotaka kukianzisha.
 
FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
5,080
2,000
Acha ajira zirudi nyumbani.. vijana hawana ajira.. wanaletewa ajira mnalalamika.. wakaguzi wa hayo magari watakuwa mafundi wa Tanzania... wanaotakiwa kulalamika ni mafundi wa japan kwa kuporwa ajira zao
 
Hapa kama wanataka kutengeneza ajira kweli basi wawape hiyo kazi sekta binafsi hapa nchini na sio hiyo kazi kufanywa na TBS walio ajiriwa na serikali... hizo ajira watazitoa wapi hapo zaidi ya kula wenyewe?
 
Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
48,514
2,000
... wao walichokimbilia ni "hizo fedha zinazoenda kwa mabeberu zirudi nchini"; hawakuona athari nyingine zitakazotokana na uamuzi wao huo. Iko hivi, gari likija bovu, mteja kala hasara ya mamilioni (sijui TRA watamrudishia kodi yake?), Tanzania imekuwa dumping place kwa sababu responsibility imekuwa shifted kutoka kwa muuzaji kwenda kwa mnunuzi/Tanzania!

Kwangu, it is by far better, waache utaratibu wa ukaguzi kufanyika nje kama ilivyo, then kama wanaitamani sana hiyo USD 100 hadi 300 ya ukaguzi mteja awalipe TBS (bure kabisa bila wao kufanya kazi yoyote) ina manufaa kwa mteja na kwa nchi kuliko hicho wanachotaka kukianzisha.
Hakika ...halafu kama fedha kurudi nchini basi wapewe sekta binafsi wawekeze na watafute wataalam na watoe ajira kwa watanzania wengi.....na sio TBS.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom