TBC1, ITV, STAR Tv NA CLOUDS FM Ni mali ya CCM?

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
7,269
675
WanaJF naomba mnisadia katika hili.

Hivi vyombo vyetu vya habari nashindwa kuvielewa sijui kwa sababu mapato yao madogo(Njaa) au ni kitu gani kinavisumbua. Mara zote nimekuwa nikifatilia nikagundua kuwa wanatumia mfumo wa Njoo karibu tule.

Wakati mwingine nimekuwa nikilinganisha hivi vyombo vyetu na Magazeti ya Udaku mara yale magazeti kila tangazo yanapokea bila kuangalia Madhara kwa Watanzania Mfano kwenye gazeti la udaku unakuata wameandika Mganga anayetibu/kukupa dawa ya mikosi, mapenzi na kurefusha U*me.

Sasa hivi vyombo nya habari namekosa imani navyo maana matanzo mengi wanayotoe hasa hasa ya CCM ni ya kupotosha Watanzania. Kama uamini sikiliza matangazo yanayotolewa au vipindi vinavyorushwa kuelekea uchaguzi. Sasa hapa ndo najiuliza kama hivi vyombo ni mali ya CCM au ccm wana shares humo??

Pia ningeomba waungwana mnijibu haya maswali

1. Hivi vyombo havina Think Tank au wataaramu wa kuchuja matangazo/ Vipindi vyao?? kuliko kupokea pumba na kuzirusha hivyo hivyo.

2.Hivi vyombo vya habari vimegeuka kuwa vya siasa au ndo njaa na kujikomba kwa sisimu

3. Wanaporusha matangazo yao wanaangalia impact kwa Watanzania??

Nawakilisha
 
...TBC, Yes! Others are just Plain Bootlickers, in capital letters... !:mmph:
 
TBC, STAR TV, CLOUDS FM wote dugu moja!...Star tv waliniboa sana pale walipoirudia mara kadha hotuba ile ya JK ya kuponda wafanyakazi!..sikuelewa nia yao, sijui walishikwa mapembe?...Clouds ndo usiseme, ni ccm in a modern 'khijab'
 
vyombo binafsi vya habari vinahaki ya kufanya chochoe ilimradi havivunji sheria. lakini vyombo vya umma lazima vitoe haki sawa kwa watanzania wote, hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi. Lakini kwa kuwa watanzania wengi ni bongolala basi wamebaki kutoa macho tu.
 
Wameshaonyesha wako upande gani. Kwa mtazamo wangu hilo ni sahihi ingawa ITV na vyombo vingine vya Mzee Mengi vinamsapoti JK tu sio CCM!
 
Star TV ya bwana Tony Diallo (mwanachama wa CCM na mbuge kwa tiketi ya chama hicho); TBC ya serikali ya CCM; ITV mmiliki wake ni mwanachama wa CCM na alitoa ushahidi huo hivi majuzi kuwa alijiunga pale tawi la Kisutu na kuamua kuamishia uanachama wake kwenye matawi ya Moshi; Clouds FM sina uhakika lakini yule marehemu Kusaga ni kama alikuwa CCM!!
 
pale clouds kuna vijana wanomba ulaji kwa nguvu kabisa na kwa maslahi binafsi wakiongozwa na KIBONDE...sina uhakika lakini nahisi kama vile simpendi kabisa huyu bana kwa mbwembwe zake....kanunuliwa kwani huwa analazimisha kuwa anasema ukweli wakati sio..............
tumestuka ...tumewasoma...tumewaweka mahali...kaeni chonjo popote mtapokuwa......tumechoka na lopngolongo......kweli mtaji wa masikini ni nguvu zake hawa akina kibonde wamepata mtaji kwa hiyo ni full lkutumia chance......
Wananiboa sana
 
Sio hivyo ilivyovitaja tu....kuna kituo kinaitwa chanel ten.....wandiriki kutuaminisha watu wote kuwa tunategemea utabiri wa sheihk yahaya ndiyo maana wanatuletea vipindi vya kijinga kabisa vya watu kusimama hadharani kuwawekea uchuro kuwa watakufa................aibu hii
 
chama hicho ulichokitaja kina fedha nyingi na kinafadhiliwa na mabilionea; hivyo
  1. ama hununua vyombo hivyo kwa kuwa kina uwezo wa kifedha
  2. au vyombo tajwa hufanya kazi kwa misingi ya biashara, yaani first money then service
  3. vyombo tajwa huogopa kuhujumiwa na serikali kwa ule mkakati maarufu wa TRA
 
Unajua mbinu inayotumika ni kuwanunua watangazi na wahariri ndio maana utaona kipindi kama cha Jahazi ambapo Kibonde yupo kazi yake ni kuipigia debe CCM na kujifanya anajua kila kitu na anachokisema yeye ndio hali halisi. Tazama siku katimu mkuu wa TUCTA alivyoshindwa kufika kutoA
a ufafanuzi wa wadai aliyotoa rais kwenye hotuba.

Walichofanya ni kumponda Mgaya na kutuaminisha kuwa Rais is everything hakuna wa kupingana naye kwa mawazo. Wanachofanya clouds ni kufanya kampeni chini ya uratibu wa CCM ndio maana baada ya gazeti la mwananchi kutangaza mawaziri kutakiwa kueleza mafanikio ya wizara zao kwa kipindi cha miaka mitano Gerald alijidai ametoa wazo la kuwaida mawaziri kuelezea mafanikio na changamoto.

Uchaguzi uliopita mtangazaji mmoja aliwahi kukiri kuwa walikatiwa fedha... kwahiyo yanayofanyika clouds msishangae kabisa ni Tawi la CCM....we still have long way to go ili tuweze kujitambua na kuacha kutumiwa
 
Mimi hili linanikera sana hasa pale TBC inapokuwa domo la CCM, na pale ninapokumbuka kuwa mkurugenzi wake ni moja ya waandishi aliyepata great exposure na kuvifunza jinsi vyombo vya umma katika nchi za wenzetu zinavyothamini umma, lakini bado kwa njaa yake au sijui analipa fadhila yeye ndio yuko mbele kuratibu propaganda za CCM kupitia TBC bila kujali kuwa wananchi ndio wanoiendesha na sio kila Mtz ni CCM! hawa Clouds tokeas walivyofanikiwa kudhulumu Joseph Mbilinyi haki yake, wakijifanya eti wanapiga kampeni ya kitaifa juu ya malaria na JK kuwa nao pamoja siku ile ya onesho basi ndio wameona ni loop hole ya wao kuwa karibu na muungwana, sasa wanapiga kampeni za wazi kabisa, na mbaya zaidi kwa kuwa hawana hata shule basi radio yenyewe imekuwa kama "kijiwe" flani hivi cha umbeya!
 
chama hicho ulichokitaja kina fedha nyingi na kinafadhiliwa na mabilionea; hivyo
  1. ama hununua vyombo hivyo kwa kuwa kina uwezo wa kifedha
  2. au vyombo tajwa hufanya kazi kwa misingi ya biashara, yaani first money then service
  3. vyombo tajwa huogopa kuhujumiwa na serikali kwa ule mkakati maarufu wa TRA
Minda
Naunga mkono hoja yako, hivi vyombo naona haswa ni fedha kwa kipindi hiki cha mavuno wenyewe wanasema, wanajua kabisa jamaa wana hela hivyo wanajitahidi kuipata.
TBC wao ni kazi yao kwa uelewa wao !! na watangazaji wengine ni kujaribu kuona kama watakumbukwa na mafisadi (opportunists)
Hivi vingine ndo kama unavyosema kuogopa kuhujumiwa.
 
Star TV ya bwana Tony Diallo (mwanachama wa CCM na mbuge kwa tiketi ya chama hicho); TBC ya serikali ya CCM; ITV mmiliki wake ni mwanachama wa CCM na alitoa ushahidi huo hivi majuzi kuwa alijiunga pale tawi la Kisutu na kuamua kuamishia uanachama wake kwenye matawi ya Moshi; Clouds FM sina uhakika lakini yule marehemu Kusaga ni kama alikuwa CCM!!
Hivyo vyombo ambavyo vipo bold ni vyombo binafsi na vipo kwa ajili ya kuijpatia maslahi popote yatakapo patikana, kwa hiyo si busara kuvilalamikia sana wakati vipo kibiashara.
...sina uhakika lakini yule marehemu Kusaga ni kama alikuwa CCM!!
Huyu jamaa kumbe ameshafariki!!?
 
Back
Top Bottom