Nilikuwa nataka kuanzisha post ya kuhusu utaratibu wa TBC siku hizi, ila naona na ww umewaamkia kwa jingine, naomba kuunganisha.
Hawa jamaa wamepoteza wafanyakazi au mwelekeo?
Taarifa zao za habari zimekua hovyo sana hadi nawaonea huruma na aibu wale wasomaji, hawana mpangilio, picha zinajichanganya, mara hazitokei, graphics zinaptiliza screen, maandishi hayaonekani, mara msomaji haonekani.
Ili mradi kero tu,
jirekebisheni hela zetu zinatuuma. Tunakatwa kodi hadi damu zinatutoka, au mnaajiri ndugu wasiojali ubora wa kazi zenu? Au mmeletewa watu na wazee wenye nchi?
Simple, wekeni delivarables in writing, kila inapotekelezeka au kushindikana toa maksi na akishuka chini mtoe.
Mnatia aibu sana
tunafungua TBC kupata basic news, balanced na sio biased, zinazowakilishwa kwa teknolojia kubwa sana mlio nayo hapo,