TBC wasitisha matangazo LIVE bungeni

kookolikoo

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
2,751
595
Hawako hewani si redio wala luninga. Hakuna sababu yoyote iliyotolewa zaidi ya mtangazaji wa zamu kusema anasikitika hakutakuwa na matangazo toka bungeni hadi tutakapoarifiwa tena.

attachment.php
 
Attachments

  • tbc-radhi.jpg
    tbc-radhi.jpg
    47 KB · Views: 3,093
Wanamficha waziri mkuu asiumbuke kwa ugaidi make nasikia kambi ya upinzani inatka maneno yote yaliyosemwa na mbunge wa ccm hasa mwigulu kuwa chadema ni chama cha kigaidi yafutwe kwenye harnsad za bunge, inaitajika kauli ya waziri mkuu na spika.
 
Maswali kwa PM ni leo,lakini nafikiri kama ni wizara ya afya,ishu ya ulimboka itatajwa tena,so naona hawana mpya,kifo chao kinakaribia,ni suala la muda tu.
 
Inasikitisha sana.serikali ya ccm kwa sasa imeshikwa pabaya sana.wanatekeleza lile ofisi ya bunge ilitamka kuwa inataka kuhariri matangazo ya bunge kabla ya kuletwa kwa wananchi
 
Sasa wakificha ndo inawasaidia nini? Yan hawa ni ''zile zinazopatikana baada ya kukoboa mahindi/mpunga" plus vu
 
Kuna kitu wanaficha, manake waziri mkuu leo angekuwa na wakati mgumu sana bungeni kuhusu yaliyotokea Arusha!!
 
namwona Ndugulile kwenye uzi huu, nadhani anaweza kutuambia kwanini bunge halionyeshwi.
 
Bila shaka maswali ya papo kwa papo leo hii yangelenga sana mlipuko na uchakataji wa matokeo ya kidato cha 4 2012. TBC wamepigwa pini kurusha live. Hii ndo bongo bana.
 
Inasikitisha sana Watanzania hatuna uhuru na vyombo vyetu vya umma ila vinatumiwa na watu wachache kwa maslai yao. waliopo bungeni watujuze yayoondelea huko
 
Hawana lolote nguvu ya uma ikiamua hakuna kurudi nyuma, badala wawe bize kutekeleza ahadi za Raisi na ilani ya CHAMA chao wao bize kufukuzana na upepo! SI wa uache upite tu Kama walivyoamuriwa na Mukulu!
 
hiki chombo kwa kweli akina nguvu ata kidogo TBC ina matatizo mengi sana kiuchumi kati mashirika ya serikali yalitelekezwa na kupewa watendaji vibaraka ni TBC hali yake ni mbaya sana kile kipindi cha kusoma taarifa ya habari kwa kutumia kibatari pale RTD (TBC TAIFA) NYERERE ROAD. inarudi akika.

"NI BORA KUPIGANA NA MTU ANAESIKIA KULIKO KUPIGANA NA KIZIWI KWANI ATA KAMA AMEKUZIDI NGUVU HAWEZI KUKUACHA HADI DAMU IKUTOKE"
 
Wanamficha waziri mkuu asiumbuke kwa ugaidi make nasikia kambi ya upinzani inatka maneno yote yaliyosemwa na mbunge wa ccm hasa mwigulu kuwa chadema ni chama cha kigaidi yafutwe kwenye harnsad za bunge, inaitajika kauli ya waziri mkuu na spika.

Acha kupotosha mkuu. Kwani hata kama TBC wasipokuwa hewani itazuia wabunge kumuuliza maswali waziri mkuu? Kama hiyo ndiyo sababu, mbona muda wa maswali ya papo kwa papo kwa waziri mkuu umeisha na bado hakuna matangazo?
 
hiki chombo kwa kweli akina nguvu ata kidogo TBC ina matatizo mengi sana kiuchumi kati mashirika ya serikali yalitelekezwa na kupewa watendaji vibaraka ni TBC hali yake ni mbaya sana kile kipindi cha kusoma taarifa ya habari kwa kutumia kibatari pale RTD (TBC TAIFA) NYERERE ROAD. inarudi akika.

"NI BORA KUPIGANA NA MTU ANAESIKIA KULIKO KUPIGANA NA KIZIWI KWANI ATA KAMA AMEKUZIDI NGUVU HAWEZI KUKUACHA HADI DAMU IKUTOKE"
Wakuu, mbona mnaongelea kitu ambacho hamna uhakika nacho? Ni bora tukafanya subira ili tupate ukweli juu ya nini kimetokea. Kwani ni haki ya wananchi kupata matangazo ya bunge. Wabunge tumewachagua kwa kura zetu na hivyo ni vyema tukatumia muda huu wa bunge kupima uwezo wao ili tuamua kama 2015 tuwe nao tena au tuchague wengine wanaotuwakilisha vizuri
 
Kuna kipindi watajikuta wanashindwa kutangaza chochote kwa kuhisi sasa kila kitu kiko against CCM. Manake mambo yanazidi kuongezeka kila siku. Bora waanze kuachane na matangazo yote tu kuanzia sasa, wapige taarabu manake mitaa ya pwani ina washabiki wengi.
 
Hawana lolote nguvu ya uma ikiamua hakuna kurudi nyuma, badala wawe bize kutekeleza ahadi za Raisi na ilani ya CHAMA chao wao bize kufukuzana na upepo! SI wa uache upite tu Kama walivyoamuriwa na Mukulu!
Bila shaka umetumwa kuandika hayo. Si kila kitu kuingiza siasa mkuu. Tunatakiwa kutafakari kwa pamoja na kuwa na msimamo wa pamoja. Kwani naamini hata wafuasi wa ccm pia hawafurahii hali hiyo
 
Kuna kipindi watajikuta wanashindwa kutangaza chochote kwa kuhisi sasa kila kitu kiko against CCM. Manake mambo yanazidi kuongezeka kila siku. Bora waanze kuachane na matangazo yote tu kuanzia sasa, wapige taarabu manake mitaa ya pwani ina washabiki wengi.
Mkuu, usije kuingia jehanamu kwa kusema uongo na kuwazulia watu uongo.
 
Back
Top Bottom