Tbc tbc tbc aibuuuuu jamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tbc tbc tbc aibuuuuu jamani

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Mtazamaji, Sep 16, 2011.

 1. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Wakuuu

  Nimeandika mara nyingi hapa na nitaendellea kuandika labda kuna siku wahusika wataaambiwa. Zaidi ya kuandika kuna siku nilishwapigia simu. Hili ni shirika shirika la TBC linalotakiwa kuwa mfano bora wa matumizi ya ICT. Siweiz kuyasema mashirika kama ITV au startv sababu ni ya watu binafsi.

  Sasa TBC Wana tatizo gani?
  Kwa muda wa siku kama nne au tano tovuti ya tbc haikuwa hewani. BAsi nikadhani wako kambi watakuja na kitu bomba zaidi. Leo najaribu naona kwenye tovuti walichoongeza ni Slider . Kwa weli kwangu ni kichekesho na aibu kwa shirika la habari la taifa . Sijui nyie mnasemaje...........

  Sasa naijiuliza.

  • Haya mabadiliko ya hii slider yamefanywa inhouse . na watalamu wa ndani au kuna kampuni imelipwa mijifedha kadhaa?........
  • hata iwe ni kampuni au wafanyaazi wa ndani je is that the best TBC have achiived for five days after beiing offline ?
  • Hivi TBC youtube ya bure imewkosea nini wanshidnw akuweka clip japo za taarifa ya habari na hotuba za viongozi mbali mbali.( Tazama mwenyewe Hizo video za youtube hazijawai kuwa updated toka hii toviuti ianzishwe). hata aliyokuwepo Tido hakuuwa na mabadiliko
  Jamani anayejua number ya mkurugenzi ( ya ofisi) wa TBC animbie maana number nyingine nikipiga majibu unapewa ya ajabu......
   
 2. M

  Megawatt B JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2011
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Usisumbuke, pale TBC wote ngumbaru na dhambi ya kumtoa TIDO itawatafuna wanaousika na wasohusika
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  They will never be serious!
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  usisahau ishu ile
   
 5. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #5
  Sep 16, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  LAkini kwa mmbo ya ICT hata Tido hakuleta mabadiliko yeyote. Hiyo Tovuti yao iko hivyo hivyo kabla na hata baada ya Tido kuondoka. Alivyoikuta ndivyyo alivyoiacha. Sasa sidhani kama hata TIDO angebadilisha kitu. Nakumbuka mara ya kwanza nawapigia simu huyo TIDO ndio alikuwa kashika usukani.

  Majibu niliyoyapata kutoka kwa muhusika mmoja ni kuwa ndio wametoka kwenye kikao kujadili baadhi ya mambo niliyowaambia.. teh teh teh

  Yaani mashirika yetu kila mtu ni mwanasiasa
   
 6. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Kuchamba kwingi waswahili husema mwisho ni kushika kinyesi
   
 7. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #7
  Sep 16, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Leo wamesema wamepongezwa na SMZ kwa kutangaza vizuri lile janga la Zanzibar. Halafu hizo sliders ziko fast kweli. Kwa pale juu kulia wameweka link ya kusikiliza TBC live lakini hakuna kitu. Wasije wakaweka na Google adsense.
   
 8. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #8
  Sep 16, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Nachoshanaga ni kuwa kuna template nzuri za joomla zinazozofaa mashirika ya utangazaji. zipo za bure na ipo nzuri zaidi za kununua kwa $50.

  Sasa wewe anagalia eti TBC haina clip au archive za video au Audio hata moja ya hotuba si ya JRais wala wa kiongozi yeyote. Haina clip ya video ya latest news. Sasa tovuti ya TBC inatofautihswa vipi na Tovuti ya Dailynews. Yaaani maudhui ya TBC ni nini?

  YAaani hata huo mpangilio wa Tovuti ulivyo mhhh . Then ukite una mtu anakula milioni kadhaa kila mwezi kuwa yeye ndio webmaster wa hii tovuti..
   
 9. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #9
  Sep 16, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kwa nini wasitumie hata CMS ambazo ni specific for news site? Wala hazihitaji customization. Kama hii: Vivvo CMS :: Online Demos
   
 10. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #10
  Sep 17, 2011
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Nadhani TBC kuna mgomo baridi kwa Tido Muhando kuondolewa ,kwa hiyo watu hawafanyi kazi kwa kujituma tena
   
 11. KIBURUDISHO

  KIBURUDISHO JF-Expert Member

  #11
  Sep 17, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 955
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Jamani achilieni mbali maswala ya hiyo tovuti yao usikivu wa matangazo yao jamani yapata wiki ya pili sasa hawapatikani nchi nzima kwa njia ya satellite wanapatikana kwa shida saaaana na hii ni mara ya pili toka warudi hewani baada ya kipindi kirefu kupotea hewani, jamani nilishawahi kusema hapa kama ni mtu alipewa kitita kwenda kufuatilia spea kazama nayo moja kwa moja wasione aibu watuambie tu maana hizo ni kodi zetu.Inashangaza sana na kunipa maswali mengi kama ni hivi kwa satellite sasa kwa mfumo huo wa digitali hiyo wanayoikimbilia kama mtoto aliyetumwa dukani na kuahidiwa kuwa mara ukirudi tu nakununulia viatu wataweza kweli!!!!!!!!????????
   
 12. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #12
  Sep 17, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,014
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Bora TVT.
   
 13. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #13
  Sep 17, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mkuu mwakalinga tatizo la TBC ni zaidi ya Tido mhando.
  Hii issue ya Tovuti haina uhusiano na Tido mhando. Kama nilivyosema TIdo mhando aliikuuta hii tvuti iko hivyo na akaiacha hivyo hivyo hivyo. ukiangali sehemu yenye picha za Youtube hawajawai kubadilishwa kitu chochote. Sasa hata Huyo Tido aliyetoka majuu naye Sijui kama alikuwa hajui umuhimu wa update ya Video clip na audio kwenye tovuti .

  Mhh unaweza ufafaua ubora upi unaoogelea kamanda.....

  Ebu jaribu kuchukua hatua za awali. Mimi nikipata tatizo kwanza huwa napiga simu kwa wahusika nisikie majibu yao. Najua hauna utakachoamabwa cha maana lakini we jaribu. Jibu watalokupa lilete hapa Na mimi baadae nitawauliza nisikie kama majibu yanayotoka ni yale yale.. Alafu tutajua................

  But ni kweli tuna matatizo sana taasisi zetu nyingi sijui kama zina mfumo na utaratibu maaluma wa indicet o problem management. Sijui hata kama na logs au vifaa vya kumonitor kuwanyesha perfoemce yao kwa Tanzania ikoje......

  Ukipiga simu ya matatizo inakuwa kama ni maongezi ya mtu barabarani . Uikata simu matatizo uliyoyaongea hayak o kwenye official records. Yako kichwani mwa mtu........... Hakuna probem reporting system
   
 14. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #14
  Sep 17, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Tatizo la mashirika yetu ya umma ni kwamba hawabadiliki na kwenda na wakati, kazi kugombania vyeo tu hata kama uwezo hawana, si hilo tu hawataki kabisa kuajili watu weledi wanasahau kwamba mambo ya sayansi ni facts and figures siyo siasa wala ngojela ukiyapuuzia yatakuja kuku-haut - unayoshuhudia sasa hivi ni matokeo ya kupuuzia ukweli kwamba mambo haya ya modern technology yanaitaji watu weledi mkubwa na siyo wababaishaji au kusubiri wachina ndio waje kuwasaidia as if hakuna watanzania wenye huwezo wa kuzifanya hizi kazi.

  Wakati mwingine wanashindwahata kurekebisha kitu kinacho julikana kama "Lip Synch" ukisikiliza sauti na kulinganisha na mdomo wa mtangazaji unaona havilandani kabisa, je naiyo inaitaji mchina kuirekebisha! Serikali yetu isipokuwa makini kwa recruit watu wenye ujuzi wa kweli na ubunifu kwa kutafuta consultant wa kuwafanyisha usahili wataalamu bila kuleta mambo ya kujuana/urafiki/undugu, shirika hilo la TBC na mashirika mengine ya umma yataishia kuchukuwa ruzuku chungu mzima kutoka Serikalini kuziendesha vile vile wakurugenzi wa Board nao wanachangia sana katika ukosefu wa ufanisi katika mashirika yetu ya umma wanasoma board papers siku moja kabla ya mkutano ni wachache sana wako makini kuona mashirika yetu yanaendeshwa kiufanisi. Kuzolota kwa mashirika haya kunatokana vile vile na kubweteka kwa management ambayo haina incentive ya kuchakalika au kuwa wabunifu maana wanajuwa wawe wabunifu wasiwe wabunifu mshahara huko pale pale - kwa nini wangaishe vichwa vyao - na hiki ndicho kimemaliza mashirika yetu ya umma, ukienda kwenye kampuni za watu binafsi mambo ni tofauti kabisa kule huwezi kuleta mambo ya umangimeza ukavumiliwa hawana mchezo kabisa wanabadirisha wafanya kazi kama bolts in a machine.

  Nimeona humu members wanazungumzia tivoti ya TBC mimi sishangai chochote, ukienda kuhulizia hapo si hajabu ukahambiwa yuko Mkurugenzi wa ICT yaani kuna kitengo kamili kinacho shugulikia mambo hayo ya ICT kama ndiyo hivyo ni kitu gani kinawashinda kudesign, ku-host na ku-update TIVOTI yao kwani si wataalamu wanao? kama wapo kazi zao ni nini hasa! jaribu kuhuliza huyo aliye design website yao alilipwa kiasi gani utashangaa. Si hajabu hata hiyo TIVOTI hiko hosted kwenye makampuni mengine wakati wenyewe wana uwezo wa kufanikisha hilo, wahulize hizo kampuni zinalipwa kiasi gani kwa mwezi/mwaka ku-host TIVOTI yao, kama wanashindwa kulifanya hilo kwa nini wasiombe msaada kutoka kwa vijana wa humu kwenye jamii forum wakawasaidia ku-redesign TIVOTI ya TBC na kuwapa tricks za kudesign site inayolingana na hadhi ya TBC bila malipo. Tatizo hili la kutojali haliko cofined kwa TBC tu karibuni mashirika mengi ya UMMA yana udhaifu huu hawajali tax payers' money.

  Badilikeni jamani haya mambo ya kudhani miaka yote itakuwa business as usual hayatatufikisha mbali, tutabakia kulalama sijuhi Serikali haitohi fedha za kutosha kununulia hiki na kile, visingizio chungu mzima. Mwisho mnaweza kunieleza watu wa AGAPE (ATN) wametumia kiasi gani cha fedha kufanikisha mitandao ya "CUTTING AGE TECHNOLOGY" karibu TANZANIA nzima ki-mahili kweli kweli na ni watu wachache tu dedicated na kwao every PENNY COUNTS they didn't robe a bank kufanikisha hilo, je na sisi tuna spirit hiyo kweli?

  Hapa nazungumza kama mzalendo wa kweli siwalengi watu fulani, lakini hatuwezi kunyamazia mambo yanayo dhalilisha Serikali na Nchi yetu, tukiona mambo yanaenda mzobe mzobe tutasema TU, Mungu ibariki URT.
   
 15. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #15
  Sep 17, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Wewe angalia kwenye contact US . hakuna number za chummba cha habari. Eti kuna number za marketing.

  Hivi TBC kumbe biashara ni muhimu zaidi kuliko hata habari zenyewe. Sasa Piga hizo number omba washuika waeleze alafu usikie majibu yao

  Hivi Tovuti ya kisasa inakosa feedback form. Mbona web desinger yeyote hata mwenye certificate analijua hilo........ yaani wana tovuti lakini kuwasiliana nao ni mpaka upige simu..............

  Nimepiga simu 255 22 2132340 simu imekatika kabla sijapewa number ya muhusika wa haipokelewi Laini dada aliyepkea anasema na yeye hana jinsi anaandika malalamiko yote anaypkea na uwezo wake ndio unahishia hapo. This time nitatafuta number ya muhusika nisikie neno lake.
   
 16. Cestus

  Cestus JF-Expert Member

  #16
  Sep 17, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Achana na hayo mambo ya tovut ambyo c watz wote wanaingia humo,mi huwa nashangaa kwnye tarifa ya habr...mtangazaj ashamaliza kutangaza habar ndo 2nasubiria picha ili tuone kwa kina zaid unakuta hamna k2 mtangazaji amebak 2 kakodo macho na yy anasubir picha itokee...saa nyngne hamna kabisa et wanadai taarifa hyo haijawa tayar....ss cjui cku nzma walikua wanafnya nn kama wanashndwa hata kuandaa taarifa ya habar ynye kueleweka,saa ingine video ya habar inakatakata utafikiri ni live feed kumbe hata sio...yaan uozo,uozo..
   
 17. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #17
  Sep 17, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Cestus uko sahii lakini ukiona hata tovuti kitu simple kinawashinda jua basi mengine huko ni hoi kabisa . Tovuti ni itu kidogo inakfanyiwa kazi wiki nzima au mwezi basi. Tovuti Sio technical routine ya kila siku. kitakachobaki ni copy and paste ya taarifa.

  Sasa kama haya wanashindwa siahanagi kwa nini hata mpangilio na timing zao kweye utangazaji amabzo ni technical routine wanazikosea. kama unavyosema.
   
 18. Izack Mwanahapa

  Izack Mwanahapa JF-Expert Member

  #18
  Sep 17, 2011
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 497
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Mambo ya kitaalam tuwaachie wataalam, Kuondolewa kwa Tido Mhando kisiasa katika shirika hili kwa hakika kutapelekea kifo cha TBC, Now TBC kimsingi haieleweki na itatia shaka kama inatimiza sifa za kuitwa televisheni ya taifa.
   
 19. Chief-Mkwawa

  Chief-Mkwawa Platinum Member

  #19
  Sep 17, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 17,813
  Likes Received: 7,152
  Trophy Points: 280
  mi sioni kama hapa tunasolve kitu zaidi ya kutoa lawama ambazo hazijengi, nafkiri tujiulize nini kifanyike.
   
 20. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #20
  Sep 17, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Jana naangalia Taarifa ya habari, chini wameandika PM ametembelea Rukwa, huku kwenye taarifa ya maelezo wanasema ametembelea Musoma. Nikatoka kapa nisijue ni Musoma ama Rukwa
   
Loading...