Tatizo hilo la kweli, makosa huanzia kwa waandishi na kama wahariri hawakupitia vizuri taarifa hiyo basi ndo hayo uliyoyaona yanajitokeza.
Tatizo la taarifa ya Rais wa Brazil kuwasili nchini na wakati huohuo kuwa atapokelewa na Rais Kibaki ni la Mpangilio ambayo wa kulaumiwa ni mhariri aliyepanga na si mtangazaji kwasababu yeye analetewa labda alichopaswa kufanya ni kurekebishia hewana kama naye alipitia kabla ya kuingia studio.
Jambo la Msingi hapa kinachoonekana pale waandishi wa TBC wanajiona wako juu ya wenzao wa vyombo vingine kwahiyo wanasahau mambo ya msingi kikazi hadi taarifa ya habari wanasoma kama vile Clause FM wanavyofanya, hawajui kuwa ile ni chombo cha Taifa. Zamani RTD ilikuwa inaajiri waliofunzwa pale lakini siku hizi kujuana bwana, mtu analeta kijana wake aajiriwe, wanasiasa nao wasumbufu nasikia ikitanagzwa ajira wanapeleka watoto na vimemo hata wasipokuwa na uwezo wataajiriwa.
Naomba kuwasilisha wana jamii.