sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,682
- 1,110
Imekuwa ni kawaida kabisa kwa chombo hiki cha habari kuhodhiwa na kufanywa mali ya CCM.Hiki ni chombo cha umma na mmiliki wake ni Watanzania bila kujali itikadi za kivyama.Lakini cha ajabu kinachofanywa na chombo hiki ni upendeleo dhahiri ambao tusipokuwa makini ipo siku nacho kitaporwa kama vilivyo porwa viwanja vya michezo nchini kote na kufanywa mali ya CCM.Imekuwa ni desturi ya chombo hiki kutumika kama jukwaa la kisiasa kunadi sera za CCM na kuacha kunadi vyama vingine kama maslahi fulani.
Tunamtaka bwana Mshana aachane na ushabiki wa kivyama na kujikita zaidi kwenye mambo ya kitaifa bila kujali upendeleo ambao hauna tija wala mashiko.Chombo hiki cha umma kitumike kwa mambo yanayohusu umma wa Watanzania ikiwa ni pamoja na kutoa fursa sawa kwa vyama vyote na asasi za kiraia.Tumeona jinsi chombo hiki kikitumika kwa upendeleo kuonyesha mkutano wa CCM ikiwa ni pamoja na kuutangaza zaidi.
Hatukatai CCM kukitumia chombo hiki bali tunachotaka haki iwe sawa kwa wote kuliko uhuni unaofanywa hivi sasa.Vyama vyote vina haki sawa katika kutoa habari zao kwa chombo hiki lakini ajabu kinatumika zaidi kuyanadi mambo ya CCM zaidi.Hiki ni chombo cha walipa kodi,tuna uhuru nacho na uhuru nacho na uhuru huo utumike ipasavyo kuliko kukigeuza kuwa cha mrengo mmoja.