TBC ni chombo cha serikali au ni mali ya CCM?

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Imekuwa ni kawaida kabisa kwa chombo hiki cha habari kuhodhiwa na kufanywa mali ya CCM.Hiki ni chombo cha umma na mmiliki wake ni Watanzania bila kujali itikadi za kivyama.Lakini cha ajabu kinachofanywa na chombo hiki ni upendeleo dhahiri ambao tusipokuwa makini ipo siku nacho kitaporwa kama vilivyo porwa viwanja vya michezo nchini kote na kufanywa mali ya CCM.Imekuwa ni desturi ya chombo hiki kutumika kama jukwaa la kisiasa kunadi sera za CCM na kuacha kunadi vyama vingine kama maslahi fulani.

Tunamtaka bwana Mshana aachane na ushabiki wa kivyama na kujikita zaidi kwenye mambo ya kitaifa bila kujali upendeleo ambao hauna tija wala mashiko.Chombo hiki cha umma kitumike kwa mambo yanayohusu umma wa Watanzania ikiwa ni pamoja na kutoa fursa sawa kwa vyama vyote na asasi za kiraia.Tumeona jinsi chombo hiki kikitumika kwa upendeleo kuonyesha mkutano wa CCM ikiwa ni pamoja na kuutangaza zaidi.

Hatukatai CCM kukitumia chombo hiki bali tunachotaka haki iwe sawa kwa wote kuliko uhuni unaofanywa hivi sasa.Vyama vyote vina haki sawa katika kutoa habari zao kwa chombo hiki lakini ajabu kinatumika zaidi kuyanadi mambo ya CCM zaidi.Hiki ni chombo cha walipa kodi,tuna uhuru nacho na uhuru nacho na uhuru huo utumike ipasavyo kuliko kukigeuza kuwa cha mrengo mmoja.
 
Hao wamegeuka wasemaji wa mafisadi na wamepeana ajira kifisadi

kama mshana kapewa ajira na fisadi ataweza kumwedea kinyume na kumvua nguo huyo fisadi?

Nimatokeo ya madaraka ya kupeana na umbumbumbu wa watawala kudhani chama tawala kinawamiliki watanzania na hakizao zote.

Usitegemee lolote la maana Baba fisadi, watoto mafisadi hata kinana ni fisadi, sembuse mshana ???? nae atakuwa fisadi hivyo wanabebana.
 
Tbccm ni mali ya chama cha magamba, ukusikia kwenye moja ya taarifa ya habari walitangaza kesi ya lema imearishwa kwa sababu wakili alute mughwai alifiwa, ila tbccm wakavunga wakili Tindu lisu hakupata msiba, ingekuwa ya taifa TIDO MUHANDO asingefukuzwa kazi
 
Tbc siku zote ni ya ccm haijawahi kuwa ya umma wa Wtz isipokuwa enzi za Tido Mhando.Mwisho waTbccm ni 2015. Saa hizi tangazeni propaganda za mafisadi.Wtz hatudanganyiki tena!
 
TBC ni ya CCM,
TPDF ni ya CCM,
POLICE ni tawi la UVCCM
hatuna budi kuvirudisha hivi vyombo kwenye mikono ya UMMA
 
Ukikuta mbwekaji akikibwekea kivuli chake, basi usihangaike naye bali jihadhari. Kama TBC ikitangaza utekelezaji wa Serikali kwa mujibu wa Ilani ya Chama Tawala basi kumbuka kwamba inao wajibu huo kwani TBC ni chombo cha Serikali na Serikali ni chombo cha wananchi nacho kiliundwa na CCM.
 
Ndio ni chombo cha serikali na ninavyojua kupata airtime lazima ulipie kusema tbc ni mali ya ccm je ccm walipewa bure kutangaza mkutano wao? Je kwani vyama vingine vya siasa vilishakataliwa kutanganza mikutano yao tbc? Tukishajibu hayo maswali tutajua kama ni mali yao au ni mali ya umma.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Imekuwa ni kawaida kabisa kwa chombo hiki cha habari kuhodhiwa na kufanywa mali ya CCM.Hiki ni chombo cha umma na mmiliki wake ni Watanzania bila kujali itikadi za kivyama.Lakini cha ajabu kinachofanywa na chombo hiki ni upendeleo dhahiri ambao tusipokuwa makini ipo siku nacho kitaporwa kama vilivyo porwa viwanja vya michezo nchini kote na kufanywa mali ya CCM.Imekuwa ni desturi ya chombo hiki kutumika kama jukwaa la kisiasa kunadi sera za CCM na kuacha kunadi vyama vingine kama maslahi fulani.

Tunamtaka bwana Mshana aachane na ushabiki wa kivyama na kujikita zaidi kwenye mambo ya kitaifa bila kujali upendeleo ambao hauna tija wala mashiko.Chombo hiki cha umma kitumike kwa mambo yanayohusu umma wa Watanzania ikiwa ni pamoja na kutoa fursa sawa kwa vyama vyote na asasi za kiraia.Tumeona jinsi chombo hiki kikitumika kwa upendeleo kuonyesha mkutano wa CCM ikiwa ni pamoja na kuutangaza zaidi.

Hatukatai CCM kukitumia chombo hiki bali tunachotaka haki iwe sawa kwa wote kuliko uhuni unaofanywa hivi sasa.Vyama vyote vina haki sawa katika kutoa habari zao kwa chombo hiki lakini ajabu kinatumika zaidi kuyanadi mambo ya CCM zaidi.Hiki ni chombo cha walipa kodi,tuna uhuru nacho na uhuru nacho na uhuru huo utumike ipasavyo kuliko kukigeuza kuwa cha mrengo mmoja.

Kimuonekano ni chombo cha habari cha tanzania kinachomilikiwa na Serikali kwa kuendeshwa na kodi zetu wanachi,ila kimatendo ni tofauti kabisa kinapotosha(kinatetea)Serikali ya ccm.
 
cha msingi ni kuikataa TBC KWA VITENDO KWA MAANA YA KUTOANGALIA VIPINDI VYAO KAMA MIMI NILIVYOKWISHA AMUA
 
Tatizo kubwa la Tanzania ni nguvu ambazo CCM imejikita nazo au chama chochote kitakachoingia madarakani kama mambo yatabakia hivihivi, njia pekee ya kuziondoa hizo nguvu ni kupitia katiba. Ambayo haikuwa na muundo wa democracy kwenye taasisi ya uraisi na nguvu za ajabu ambazo zinawapa viongozi wa serikali (executive branch kwenye maamuzi).

Hata kama katiba mpya ikitoka kesho without removing those unnecessary powers ni kutwanga maji kwenye kinu tu.

CCM wanataka jenga jengo jipya dodoma, who the heck is paying for that let me guess kwakuwa hawana miradi ya kutengeneza pesa independently gharama ni kutoka kwa taxpayers purse, where on earth do u see such bunkum in countries where there are multi-political parties.

Ukweli ni kwamba changes are needed kwa watu ambao wanaotakiwa kuikosoa serikali ya CCM mengi yanapita tu bila ya kujadiliwa surely it has to be said pengine ni kutokana kuwa na uelewa mdogo kutoka kwa viongozi wa upinzani. Ni sasa maana ya siasa za upinzani hiwapo wenzao wanauwezo wa kuchota hela za walipa kodi at will, ukitoka nje za wimbo wa ufisadi ukweli ni kwamba amna uelewa.
 
Tatizo ni kwanini chombo hiki kihodhiwe na chama badala ya kuwa chombo cha umma.Pia pamoja na kuwa chombo cha umma wakati mwingine kimekuwa kizusha mgogoro mkubwa ndani ya jamii kwa taarifa ambazo wakati mwingine hupelekea kuwagawa Watanzania kiitikadi na kusahau umoja wao wa kitaifa,mfano mzuri walipotoa takwimu za sensa kuhusiana na idadi ya waislamu na wakristo bila kufanyiwa utafiti,lakini serikali ilikaa kimya na kutokuifungia lakini gazeti la mwanahalisi lilipo kemea maovu ya viongozi wa serikali lilionekena likieneza uchochezi.
 
Dawa yake tuiweke kwenye katiba kisha tuiundie sheria na kanuni za uendeshwaji wake vinginevyo tukivunje tuunde chombo kingine ambacho kitakuwa kwa ajili ya umma na hakitofungamana na upande wowote,hapo tutakuwa tumekomesha.Lakini kama rais ataendelea kuwa na power of appointee basi tutegemee madudu zaidi ya TBC,TAKUKURU,TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI,MAHAKAMA na mengineyo yenye kutenda kwa kulipa fadhila za kuteuliwa.
 
Back
Top Bottom