TBC mnamtukuza Rais Magufuli mpaka mnakera

Huwa nakaa najiuliza, hivi tulitegemea tuchague Rais ili afanye nini? Kwanini anapotimiza majukumu yake hivi sasa imekuwa kama vile ni msaada mkubwa sana kwa nchi yetu. TBC kutwa nzima ni vipind vya kumtukuza Magufuli. Muda wote mnarudiarudia tu vimiradi alivyofanya. Kwani waliomtangulia hawakufanya miradi mizuri na mikubwa kwa taifa? Je TBC haikuwepo?

Mi binafsi nakereka hata kwangu siwezi weka TBC nikaangalia hata dakika 5. Nikikuta labda bar au sehem yoyote wanaangalia TBC huwa natamani kuondoka muda huo huo.

Hii TV ni ya TAIFA au ya Magufuli????
Mimi nahisi wanafanya hivyo kwa lengo la kufikiriwa sehemu nyingine za teuzi. Kusema ukweli hawa jamaa ni kero na wanaboa mpaka wenzi wao wa ndoa, michepuko yao na hata ndani ya familia zao.
 
Huwa nakaa najiuliza, hivi tulitegemea tuchague Rais ili afanye nini? Kwanini anapotimiza majukumu yake hivi sasa imekuwa kama vile ni msaada mkubwa sana kwa nchi yetu. TBC kutwa nzima ni vipind vya kumtukuza Magufuli. Muda wote mnarudiarudia tu vimiradi alivyofanya. Kwani waliomtangulia hawakufanya miradi mizuri na mikubwa kwa taifa? Je TBC haikuwepo?

Mi binafsi nakereka hata kwangu siwezi weka TBC nikaangalia hata dakika 5. Nikikuta labda bar au sehem yoyote wanaangalia TBC huwa natamani kuondoka muda huo huo.

Hii TV ni ya TAIFA au ya Magufuli????

ulitaka wakusifie wewe
 
Mkuu pamoja na hii mitandao yote ya kijamii bado unaangalia TBC kweli. Kwenye mitandao unapata kitu roho inapenda na unachangia utakacho, sio hizo redmade programmes. Hiyo TBC wanaangalia wazee wa ccm na watu wa vijijini wasiojua lolote.
 
Kuna kipindi kinaitwa Tanzania Mpya, yule jamaa sijui hata kama huwa anamsifia mkewe kama anavyomsifia 'mzalendo namba moja'.
 
Huwa nakaa najiuliza, hivi tulitegemea tuchague Rais ili afanye nini? Kwanini anapotimiza majukumu yake hivi sasa imekuwa kama vile ni msaada mkubwa sana kwa nchi yetu. TBC kutwa nzima ni vipind vya kumtukuza Magufuli. Muda wote mnarudiarudia tu vimiradi alivyofanya. Kwani waliomtangulia hawakufanya miradi mizuri na mikubwa kwa taifa? Je TBC haikuwepo?

Mi binafsi nakereka hata kwangu siwezi weka TBC nikaangalia hata dakika 5. Nikikuta labda bar au sehem yoyote wanaangalia TBC huwa natamani kuondoka muda huo huo.

Hii TV ni ya TAIFA au ya Magufuli????
Wewe utakuwa siyo mzalendo kabisa. Kuna shida gani Television ya Taifa ikimpa airtime mkuu wa nchi??? Unataka airtime apewe nani?
 
Wewe upo kama mimi huwa nakerwa na hiyo TBC hasa nikimsikiaga huyo wanaye mtukuza jinsi alivyokoswa zile Swagga za kukufanya uvutike kumsikiliza.kila kitu ni ukali ukali tu halafu kitendo cha kuwadharau waliomtangulia na kujiona yeye ni Special.
 
Huwa nakaa najiuliza, hivi tulitegemea tuchague Rais ili afanye nini? Kwanini anapotimiza majukumu yake hivi sasa imekuwa kama vile ni msaada mkubwa sana kwa nchi yetu. TBC kutwa nzima ni vipind vya kumtukuza Magufuli. Muda wote mnarudiarudia tu vimiradi alivyofanya. Kwani waliomtangulia hawakufanya miradi mizuri na mikubwa kwa taifa? Je TBC haikuwepo?

Mi binafsi nakereka hata kwangu siwezi weka TBC nikaangalia hata dakika 5. Nikikuta labda bar au sehem yoyote wanaangalia TBC huwa natamani kuondoka muda huo huo.

Hii TV ni ya TAIFA au ya Magufuli????
Ulitaka wamtukuze Lisu ndio ufurahi?
 
Wewe utakuwa siyo mzalendo kabisa. Kuna shida gani Television ya Taifa ikimpa airtime mkuu wa nchi??? Unataka airtime apewe nani?
Anataka apewe Lisu hawa ni ''wazee wa lawama na matukio''wanakuja shtuka wenzao wamechukua ushindi waaxhe waendelee kuloloma humu mitandaoni wakati wenzao wanaeneza sera
 
Baba yako ilikuwa jukumu lake kukununulia nguo ili uvae!!ina maana ulikuwa humwambii asante??kama ulikuwa humwambii basi wewe mtoto wa hovyo
Kutokana na comment yako!
Baba alikuwa ananua kwa pesa yake mfukoni,
Kinachofanyika chanzo cha pesa ni kodi yako inatumika na siyo pesa ya mtu.
Kama atahisi anatutendea mema saaana na hakuna mwingine anaweza kufanya kama yeye. Basi akae pembeni aone kama hayatonyika!!
Mazuri huwa yanajitangaza yenyewe mpaka kutumia nguvu kueleza mambo ambayo ni dhairi!!
 
Siwezi kumpa mtu kura yangu kwa kujenga shule,barabara n.k sababu ni majukumu yake aliomba kwa wananchi wamchague
 
we na wewe umeongea u K tu, aliekudanganya watumishi wa umma wanalipwa na serikali nani? nyi ndo ma zuzu msiojielewa
 
Huwa nakaa najiuliza, hivi tulitegemea tuchague Rais ili afanye nini? Kwanini anapotimiza majukumu yake hivi sasa imekuwa kama vile ni msaada mkubwa sana kwa nchi yetu. TBC kutwa nzima ni vipind vya kumtukuza Magufuli. Muda wote mnarudiarudia tu vimiradi alivyofanya. Kwani waliomtangulia hawakufanya miradi mizuri na mikubwa kwa taifa? Je TBC haikuwepo?

Mi binafsi nakereka hata kwangu siwezi weka TBC nikaangalia hata dakika 5. Nikikuta labda bar au sehem yoyote wanaangalia TBC huwa natamani kuondoka muda huo huo.

Hii TV ni ya TAIFA au ya Magufuli????
Mkuu una ujasiri wa simba ! unawezaje kuangalia TBC ?
 
Hivi hata Wewe mpaka hivi sasa humtukuzi Baba yako ambaye amesababisha uwepo hapa Duniani huku akiwa amekupa Huduma zako zote muhimu na Wewe ukiwa ni Tegemezi Kwake? Kuwalaumu TBC ni Kuwaonea kwani ' Logically ' tu huyo Mheshimiwa Kikatiba uliyemtaja hapo ndiyo Mlipaji wao Mkuu wa Mishahara na moja ya ' Policy ' ya ' State Owned Television ' ni Kuitetea, Kuilinda na Kueneza ' Propaganda ' za Serikali husika ambayo pia ni ya Chama husika. Kwa kukusaidia tu ni kwamba hata Siku ikitokea Rais wa nchi hii akawa unayempenda Wewe ( kutoka Upinzani ) basi watafanya haya haya unayoyaona wanayafanya kwa huyo Mheshimiwa Kikatiba ambaye unaonekana unamchukia kuliko maelezo kwa sababu unazozijua Wewe Kiongozi.
mi mwenyewe nategemea Tv ya Taifa itaisifia serikali iliyopo madarakani (japo ideally inatakiwa iwe neutral) ila hatuishi kwenye ideal world, lakini wanachofanya TBC nadhani imepita kiasi
vipindi vingi sana unakuta ni program za kumsifia Magufuli, wakipumzika wakweka muziki basi, ni muziki wa kumsifia Magufuli, sasa hiyo inakuwa kama ni uzezeta, sifia ila kwa kiwango
 
Niliacha kuangalia hiyo channel miaka 4 iliyopita..wanaboa
 
Kama kila mtangazaji ana ilani ya Chama unategemea watangaze na kurusha nini eti? Nasikia wanaandaa na vibonzo vya Watoto kwa Lugha ya ccm!
 
Back
Top Bottom