CCM: Magufuli yupo tayari kwa Midahalo; tuna kila dalili ya Ushindi

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
709
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinatarajia kufanya mazungumzo na waandishi wa habari leo siku ya jumatano saa saba mchana katika ukumbi wa mikutano uliopo Ofisi ndogo za Makao Makuu ya CCM zilizopo Lumumba jijini Dar es salaam.

Katika maongezi hayo, CCM itazungumzia mambo makuu matatu (3) ikiwemo tathimini ya mwenendo mzima wa kampeni za uchaguzi mkuu tangu siku ya uzinduzi wa Kampeni tarehe 23rd August 2015, Jangwani.

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali mnakaribishwa katika Press Conference hiyo.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.


Mkutano huu wa CCM na waandishi utarushwa moja kwa moja (Live) na kituo cha Azam TV, pia kupitia redio Uhuru, TBC taifa, Clouds n.k

============================== =====




Updates
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tumewaita kuwaomba mtusaidie kufikisha ujumbe ufuatao kwa Watanzania:

MWENENDO WA KAMPENI ZA CCM

Hadi jana, tarehe 16 September 2015, Mgombea Urais wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli, alikuwa amekwishafanya kampeni katika mikoa 12 na Majimbo 94. Amekwishafanya mikutano mikubwa ya hadhara 76 na mikutano ya barabarani 381. Amekwishatembea, kwa gari, jumla ya kilomita 13,720. Kwa ujumla amekwishakutana, moja kwa moja, na asilimia zaidi ya 30 ya wapiga kura. Kwa kuwa baadhi ya mikutano yetu inatangazwa moja kwa moja na redio za kijamii na luninga, wapiga kura waliopata nafasi ya kumsikia wanakadiriwa kufikia asilimia 70.

Tunafarijika na idadi kubwa ya watu wanaokuja kwenye mikutano ya kampeni zetu. Tunafarijika pia kwamba karibu Watanzania wote wanaopata fursa ya kumuona na kumsikia wamemuelewa na wamepata matumaini ya Tanzania Mpya kupitia kwake. Utafiti wetu wa ndani, tulioufanya kwa kipindi cha siku kumi zilizopita katika majimbo 246 kati ya majimbo 269, unaonyesha kwamba Dr. Magufuli atapata ushindi wa asilimia 69.3 Tunaamini kwamba asilimia hizi zitaongezek kadri Watanzania wengi zaidi wanavyopata fursa ya kumsikiliza Dr. Magufuli na kusikiliza Ilani na sera za CCM.


Kwa upande wa kampeni zetu za Ubunge, zaidi ya robo tatu ya wagombea Ubunge wa CCM wamekwishazindua kampeni zao na wanaendelea vizuri. Sekretarieti ya Kampeni ya CCM inaanda program maalum ya kampeni katika majimbo yenye changamoto mahsusi.

Napenda kuchukua fursa hii kuwajulisha wana-CCM kwamba viongozi na makada wengine wa CCM, waliopo madarakani na wastaafu watapita tena, jimbo kwa jimbo, nchi nzima katika siku 30 za mwisho katika jitihada za kuongeza ushindi wa CCM na Dr. Magufuli.

MIDAHALO YA WAGOMBEA

Wiki tatu zilizopita, CCM, na kwa hakika vyama vingine pia, ilipokea mwaliko wa Mgombea Urais wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli, kushiriki kwenye mdahalo wa wagombea Urais uliondaliwa na Baraza la Habari Tanzania (Media Council of Tanzania) kwa kushirikiana na taasisi nyingine kadhaa, ikiwemo Twaweza. Dr. Magufuli amekubali kushiriki katika mdahalo huo. Kwa msingi huo, kauli ya UKAWA iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Ndugu James Mbatia, kwamba UKAWA inaomba mdahalo ni njia ya kuwahadaa Watanzania tu kwa kuwa mwaliko wa mdahalo ulikwishatolewa mapema kwa vyama vyote na wanaotakiwa kushiriki ni wagombea Urais wa vyama.

CCM inafurahishwa na utamaduni wa midahalo ambao unaanza kujitokeza katika chaguzi zetu. Na inaamini kwamba midahalo ya Wagombea Urais ni
sehemu muhimu ya kuwashirikisha wapiga kura katika mchakato wa uchaguzi na kuwasaidia waamue nani wamchague kwa misingi ya hoja na sera na sio kwa ushabiki, kwa mihemko, na kwa propaganda. Mdahalo unatoa fursa ya wagombea kuulizwa maswali ya moja kwa moja na kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu sera na ahadi zao, fursa ambayo hawaipati kwenye mikutano ya hadhara kampeni.

Hatukubaliani na kauli ya UKAWA kwamba mdahalo usiwe baina ya wagombea bali uwe baina ya Wenyeviti wa Vyama. Tunaamini hoja hii ni kichekesho. Haijawahi kutokea popote duniani kwenye utamaduni wa midahalo, kwamba wagombea wasishiriki bali watu wengine ndio wafanye midahalo kwa niaba yao. Tunaamini mdahalo huu unapaswa kuwa baina ya wagombea. Wao ndio wanaoomba dhamana. Wao ndio wanaopaswa kujibu maswali na kufafanua kuhusu ahadi zao.

CCM inaamini kwamba ili mdahalo huu uwe na tija, wagombea Urais wote, hasa wa vyama vikuu, wawepo na washiriki. Mdahalo hautakuwa na maana
kama mgombea mmojawapo wa vyama vikuu atatengeneza kisingizio ili asishiriki.

UCHAGUZI WA AMANI

CCM inasikitishwa na kauli zinatolewa na baadhi ya viongozi wa UKAWA zenye kuashiria fujo na vurugu. Kauli kwamba kura zitaibiwa hazina msingi wowote. Kauli hizi zinaashiria maandalizi ya kushindwa na maandalizi ya kufanya vurugu baada ya matokeo ya kushindwa.

Utaratibu wa uchaguzi wetu unajulikana na umekubalika na vyama vyote. Kura zinapigwa kituoni na kuhesabiwa kituoni mbele ya mawakala wa vyama vyote, wasimamizi wa uchaguzi na waangalizi wa uchaguzi wa ndani na nje ya nchi. Baada ya kura kuhesabiwa, matokeo yanajazwa katika fomu ambayo kila wakala anasaini na kupewa nakala. Nakala ya matokeo hayo pia inabandikwa nje ya kituo cha kupiga kura. Kila Chama, na kila Mtanzania, kina fursa ya kujumlisha matokeo yake kwenye kila kituo na kupata jumla kuu. Matokeo ya nchi nzima yanajumlishwa mahala pamoja huku kukiwa na waangalizi wa uchaguzi wa ndani na nje ya nchi, pamoja na wawakilishi wa vyama vyote na wao wakiwa na fomu zao za kila kituo nchi nzima.

Tunapenda kuwasihi Watanzania wasikubali vishawishi vya kufanya vurugu. Mara nyingi, viongozi wanaohamasisha vurugu wanakuwa na ulinzi au walinzi au uwezo wa kukimbilia pahala penye utulivu zaidi huku wakiwaacha wafuasi wao katika wakihangaika.

UCHAGUZI NA UMOJA WA KITAIFA

CCM pia inapenda kusisitiza imani yake kwamba uchaguzi haupaswi kutugawa kama taifa. Uchaguzi ni tukio la kupita. Kuna maisha baada ya uchaguzi. Kuna taifa baada ya uchaguzi. Lazima taifa liendelee kubaki moja, tuendelee kubaki wamoja. Tusitoe kauli za kupitiliza zenye mrengo wa kujenga chuki katika jamii na kuhatarisha umoja na amani ya nchi yetu.

Kama Chama kilichoasisi umoja wa taifa letu, tunaendelea kuasa kwamba wanasiasa wasijinadi kwa misingi ya udini, ukabila wala ukanda. CCM haina mpango kuendeleza mjadala wa kauli ya Mgombea wa UKAWA Ndugu Edward Lowassa aliyoitoa kanisani Tabora tarehe 6 September 2015
kwamba nchi ilishapata viongozi Wakatoliki na kwamba sasa ni zamu ya Walutheri kuchukua nafasi hiyo. Tunaamini mjadala huo hauna tija. Tunaamini kwamba Watanzania wengi, wa dini na madhehebu yote, hawaamini katika siasa za namna hii. Tuliamini kwamba UKAWA ingetumia fursa ya mkutano wao na waandishi wa habari jana kuomba radhi kwa Watanzania. Kwakuwa hawakufanya hivyo, tunapendekeza mjadala wa jambo hili ufungwe. Itoshe tu kwamba Ndugu Lowassa amesema hivyo, Tume ya Uchaguzi imemuonya, na yeye hajajitokeza kuomba radhi wala kufafanua. Watanzania wamemjua ni kiongozi wa aina gani na watatoa hukumu yao tarehe 25 Oktoba 2015.

Imetolewa na:-

January Y. Makamba,

MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM
MJUMBE WA KAMATI YA KAMPENI YA CCM
16/9/2015



attachment.php
Januari Makamba ameingia ukumbini anatoa tathmini fupi ya kampeni, anasema watanznaia waliomuona wanadadiriwa kufikia asilimi 70 na wanamuelewa na kuielewa ilani ya Chama.

Tathmini yao fupi inaonyesha kuwa atashinda kwa asilimia 69.3, anasema upande wa kampeni za Ubunge wanaendelea vizuri na Sekterieti ya CCM itaandaa utaratibu wa kutatua changamoto zilizojitokeza.

Amesema mwendendo wa kampeni hizo, umeenda sambamba na midahao, anasema John Mgufuli aliombwa kushiriki mdahao huo na amekubali na misingi hiyo kuna kauli iliyotolewa na UKAWA kupitia kwa James Mbatia ni kauli ambayo inashabiana na kile kinachojadiliwa na vyama vya siasa.

Makamba: CCM midahalo inatakiwa kuwa kati ya wagombea, wagombea wote washiriki na akikosekana yoyote katika vyama vikuu utapoteza maana.

Wote tunafahamu kura zinapigwa vituoni na zoezi la kuhesabu linafanyika mbele ya macho mengi na kwa uwazi na mawakala kwenye vituo wanatia sahihi na kuondoka na fomu zao, kila mtanzania ana fursa ya kujumlisha matokeo nchi nzima, kwenye tume pia wanajumlisha na kuna mawakala na sio sehemu ya siri.

Kauli kwamba kura zitaibiwa ni recless, tunapenda kuwasihi watanzania wasikubali vishawishi vya kufanya vurugu, wahamasishaji wa vurugu huwa wana ulinzi ama sehemu ya kukimbilia, huu ni uchaguzi wa tano na zote za kabla ziliisha kwa amani.

Baada ya uchaguzi kuna maisha, kuna taifa na lazima wote tuendelee kubaki wamoja. Tusitoe kauli zilizopitiliza, tunaendelea kuasa wagombea wa kujinadi kwa ukabila, udini na ukanda, CCM haina mpango wa kuendeleza mjadala wa kauli aliyotoa mgombea Rais Tabora. Tulitegemea UKAWA jana wangeomba radhi kwa kauli ile, CCM tunasema tunafunga mjadala

Mayage(Swali): Nahitaji tu ufafanuzi, unaongea kama nani ndani ya chama

Makamba: Nazungumza kama mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM vilevile mjumbe wa kamati ya taifa ya kampeni ya CCM, nazungumza kwa niaba ya CCM na ninayo mamlaka ya kuzungumzia mwenendo wa kampeni na mambo yote niliyoyazungumzia hapa. Kuhusu kumzungumzia mgombea Urais na si mgombea mwenza, kama mnavyofahamu kampeni inabeba mgombea Urais na kura anapigiwa mgombea Urais

Matutu(Matanzania): Mnafikiria mtapata asilimia 69.3, mnatumia vigezo gani?

Balile: UVCCM walisema watashinda kwa asilimia 80 leo asilimia 69 na UKAWA walisema 80 lakini sasa 70

Makamba: Tumewapa taasisi huru watufanyie badala ya sisi wenyewe, kuna metholodojia ya takwimu imetumika, margin of error kwetu ni asilimia tatu. Sina hakika UVCCM walitumia vigezo gani na siwezi kuwasemea UKAWA. Tunafurahi mgombea wetu anaonyesha energy na mikutano mikubwa, upepo upo upande wetu.

 

Attachments

  • 2015 - JANUARI MAKAMBA - PRESS CONF. - 16.9.2015.doc
    34 KB · Views: 798
Last edited by a moderator:
Na nyie kwa kuiga hamjambo,yaani jana tuu Mbatia kuzungumza leo mmekurupuka.Hivi ccm huwa hamna watu wenye akili za ugunduzi?kila kitu copy & paste from Ukawa.

Mbatia kasema yupo tayari kwa mdahalo nanyi jitokezeni acheni bla bla za kutugawa watanzania kidini, kikabila, kikanda.
 
Maongo hayo!.

Yote yatakayoogea ni hila na uwongo tu!

Mtaniambia nipo hapa.
Lakini kwanini nyie ni watu wa kulia lia siku zote, so defensive and predictable. Unajua inapofika wakati umeamua kupambana na ikafika wakati haujifanyii maandalizi bali u just observing maandalizi ya mwenzako utaishia kushindwa.

Kila mmoja anayo haki ya kuzungumza na watanzania, sio haki ya mtu mmoja ama chama kimoja, bali kila chama kina haki hiyo.

Mbona sisi huwa hatuangaiki na Press zenu, hatuzifuatilii wala hatuna haja nazo...tuko focued na jambo letu..nanyi jifunze kuwa hivyo.
 
Usikute wanataka kuanza kulalamika kuwa hoo kampeni haziendi vizuri. CCM tunatahadhalisha...... kuna watu sijui wanafanya nini. Ha ha hahaaaaaaaaaaa nitachekaje nikiona wanalalamika. Nitajua ya Banda wa Malawi yameshafika bongo. Tusubiri
 
Lakini kwanini nyie ni watu wa kulia lia siku zote, so defensive and predictable. Unajua inapofika wakati umeamua kupambana na ikafika wakati haujifanyii maandalizi bali u just observing maandalizi ya mwenzako utaishia kushindwa.

Kila mmoja anayo haki ya kuzungumza na watanzania, sio haki ya mtu mmoja ama chama kimoja, bali kila chama kina haki hiyo.

Mbona sisi huwa hatuangaiki na Press zenu, hatuzifuatilii wala hatuna haja nazo...tuko focued na jambo letu..nanyi jifunze kuwa hivyo.

Lakini mnakaribisha muache hoja za kutojua
 
Unahangaika sana wewe Mtu, na vipi mbona haupo kwenye Ziara za Mikoani na Maghufuli, au perdiem ulizolamba na Kinana kipindi kile zimekutosha??
 
Bwana Nape tumeshachoka na polojo zenu. Vipi Ile kauli yako ya goli la mkono Leo utaitengua au?
 
Copy and paste ya jana. Angalau wangesubiri kidogo! Nashauri keshokutwa mtu mwingine wa UKAWA atoe press. Mwendo uwe hivyo hadi siku 38 za uchaguz ziishe!
 
Back
Top Bottom